Jamani Oilcom ni wezi! wezi! wezi wa mafuta kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani Oilcom ni wezi! wezi! wezi wa mafuta kabisa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Cool, Feb 15, 2012.

 1. C

  Cool Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nimekuwa nasoma post mbalimbali kuhusu wizi wa hawa jamaa wa Vituo vya mafuta vya OILCOM, nikapuuza leo yamenikuta. Nimetoka na gari yangu mpaka Oilcom pale tiptop manzese, nikajaza mafuta ya 12,000 yaani lita 6. Natoka hapo nikijua hayo yatanifikisha mpaka kesho, nafika Jangwani taa ya mafuta inawaka. Nikajua tu kama hawajaniwekea hewa, basi wameweka nusu lita.

  Nakusihi mwenzangu hawa jamaa achana nao kabisa mpaka washike adabu, wamezidi kutuibia

  Jamani hawa jamaa ni wezi kabisaaa! Wahusika sijui wapo wapi. Wamekuwa wezi kama TIGO
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  mafuta nenda TOTAL
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  duh hadi we umeingizwa mujini?? kwa hiyo ikawaje?? ulirudi palepale kulalamika??ulipewa risiti ya malipo??
   
 4. rushanju

  rushanju JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 2,344
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  Vituo vingi sana hapa mjini ni wezi. Ukienda na Kidumu kuna pump yake na gari pia kuna pump yake hasa kwa petrol. Ukienda na gari hawawezi kukuuzia toka kwenye pump ya wenye vidumu. Kwenye dumu ni rahisi kumonitor. Nina imani ewura wako macho watashughulikia
   
 5. C

  Cool Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ningefanyeje sasa nishafika jangwani nawahi ofisini? hata ningerudi wangeniyeyusha, Hawa jamaa nasema dawa yao inachemka, subiri!
   
 6. C

  Cool Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kama wamezoea kiasi hiki, msingae sana, vituo vyao vyote vitatoweka, subiri
   
 7. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kuwaka taa ya mafuta kwenye dash board ya gari hakumaanishi kuwa mafuta yamekauka kwenye tank, bali ni tahadhari kuwa unahitajika kuongeza mafuta kwenye gari. Kwa kutegemea na aina ya gari, lakini nyingi, huwaka taa ya tahadhari pindi mafuta kwenye gari yanapobaki chini ya lita 10. Na kwa maelezo yako umesema ulinunua lita 6 tu, ambayo ni chini ya lita 10, lazima taa iwake.
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  pole sana
   
 9. luck

  luck JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 772
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  Kama hutaki presha nunua mafuta vituo hivi BP (hasa vituo vinavomilikiwa na bp wenyewe),Total,Engen.
  Ukikosa kabisa nenda kokote lakn sio oilkom hao jamaa sio kabisaa nilishawadiscredit kitambo sana!
   
 10. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,048
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Inabidi uwe makini wale wauzaji wajanja sana kwani kama kuna mtu aliyekuwa kanunua mafuta ya 10,000/= basi wewe wamekuwekea elfu mbili tu. Kuna siku walitaka kuniliza hivyo hivyo Kinyerezi sijui nako ni OILCOM? sikai huko. Nilitaka aniwekee ya Tsh 30,000/= kumbe kuna jamaa kawekewa ya 15,000/= jamaa akaanzai pale kuendelea (kuna jinsi wanavyo tegeshea zile pump) basi wife akashutukia dili ndo jamaa akajibaraguza na kuniwekea yote.
   
 11. l

  luckman JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  hawa jamaa ni wezi sana, wezi tena wakubwa hawa, kuna vituo vya oilcom ubungo, oilcom tabata relini pale kona, mi jumamosi waliniliza, nimeweka mafuta ya 10,000.00 nimeenda tabata kimanga kurudi hadi pale sheli yameisha niliwafata wakasema geji yangu mbovu, nikamchukua mfanyakazi mmoja tukaenda hadi engen nikatia ya 10,000.00 mshale ukapanda fasta nikamuuliza umeona akasema basi wataongea na bosi wao waone tatizo ni nini,

  nililianzisha palepale nikadai pesa yangu wala mafuta yao siyataki, moto ukawaka tena sana make mafisadi naona ni kila eneo, nawaombeni mafuta jazeni engen, total, agip au kituo kingine tofauti na oilcom!
   
 12. C

  Cool Member

  #12
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Du! Hii janja yao nilikuwa sijainyaka, kumbe..!
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Dawa ni kujaza full tank.....hawakuibii ng'o manake lita za full tank zinajulikana.........halafu gari inakula mafuta vizuri ikiwa full tank........vinginevyo nenda na galoni ujaze halafu ujimiminie.......galoni linajulikana ni lita 5 na hawawezi kukuibia
   
 14. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  10,000.00 mshale ukapanda fasta =5litres

  DUH gari yako ina cc ngapi!!??
   
 15. grey

  grey Senior Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nimeshajua janja yao. natembea na kidumu tuu. wanajaza naenda kuweka mwenyewe. Ahsante kwa ujumbe
   
 16. MANI

  MANI Platinum Member

  #16
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,872
  Trophy Points: 280
  Vitz au Duet 660 !
   
 17. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Usisahau chupa ndogo ya KILIMANJARO water kwa ajili ya kumiminia
   
 18. grey

  grey Senior Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hehehe, kweli kabisa na wembe wa kuikatia ili ifae kama funnel...
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Jamaa kun siku niliwaudhi ile mbaya waliponojazia kidumu tu nikamimina kwenye tank kwa hicho kichupa......karibu wapasuke sura
   
 20. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Full tank kila uingiapo shell mkuu, usifanye mchezo na haya maisha ya kiTZ, labda kutembea na galoni nako inakuwa kaazii kweli kweli
   
Loading...