Jamani nini mpango wa ccm na wakuu wa wilaya kuhusu katiba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani nini mpango wa ccm na wakuu wa wilaya kuhusu katiba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'ong'onsela, Feb 9, 2012.

 1. N

  Ng'ong'onsela New Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hili nalo linatutisha ,kuna ajenda gani ya siri kuhusu wakuu wa wilaya? au ndio matokeo ya kikao cha dharura kati ya Rais na wabunge wa ccm....
   
 2. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  wanaogopa kivuli chao wenyewe. Wanajua kuwa mkurugenzi hawawezi kumshurutisha kwa sababu hawezi kufukuzwa kazi kiholela asipofanya wanayoyataka. Kuna wengine kama kawaida yao wanaunga mkono hoja bila hata kutafakari nini anachokipigania
   
 3. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,779
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Wakuu wa wilaya ni sawa na mabarozi wa nyumba kumi wa CCM hivyo wasipohusishwa kwenye jambo hili ujue CCM imekwisha na ni mwanzo mzuri wa kupata katiba itakayoiondoa CCM madarakani! CCM wameshtukia hilo ila wamechelewa kwani CHADEMA walijifanya wajinga wakamkubali Kikwete na hivyo kusababisha hoja zao zote zikaingia kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba! Serikali ikawafumba macho wabunge wa CCM kwa kusema mapendekezo hayo ni ya serikali............ Ukifuatilia hotuba ya kambi ya upinzani bungeni ambayo kwa siku ya jana iligeuka kuwa kambi inayoongoza bunge, utaona jinsi CHADEMA walivyowafanyia kitu mbaya jamaa wa CCM!
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Kuliwahi kuwa na mkoa wa ziada usio kuwa na ardhi yaani TPDF, hivi bado upo? wakuu wengi wa wilaya ni wanajeshi wastaafu ambao ni CCM damu damu!!!

  Hii inaonesha namna gani CCM ni wezi wa kura na kushinda chaguzi kwa hila!
   
 5. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hakuna tofauti yeyote wakuu.
  Wakuu wa wilaya siyo pekee wataopewa uwezo wa kuitisha mkutano. Kuna viongozi wengine wa kata, tarafa, vijiji n.k ambao wanaweza kuombwa na tume kuitisha mkutano. Thats about it!
  Wakurugenzi wataingiaje kwenye mambo ya siasa?..
  Na je, Zanzibar nani atakuwa na uwezo wa kuitisha hiyo mikutano?.... Sheha? au mkurugenzi wa mipango?
  Katiba ni suala la muungano, na local government si suala la muungano kwani Z'bar wana mfumo tofauti kidogo.
  Hapo suala ni uwezo wa kuitisha mkutano tu, na tume inaweza kuwaskip kama ikitaka na kutumia wale wa ngazi ya chini.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Aisee ni hatua kubwa sana, huyu mama Anna kilango ni mamluki tu hana jipya
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  yani huyu mama ananikera, sijui anaishije na yule babu malecela asiyeweza hata kuongea
   
 8. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  kilango ananchefua sana eti "simameni....eeehe .....simameni tunaunga mkono hoja", akiwalazimisha vilaza wenzie wasimame ili kuunga mkono hoja kabla hata speaker hajaruhusu. milaza nayo ikasimama, kama katuni yaan
   
 9. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Jamani hata kama wakiongea kwa jazba vipi bado Wapinzani wameng'ara kwenye mswada huu.

  Huyu mama nimemtazama jana kwenye runinga yaani anaongea mpaka mate yanamtoka kutetea ma-DC wawemo kwenye mchakato wa kuunda Katiba mpya! Kwa kweri aliniboa stiff!Pambaf Kabisa. Huu ndiyo upuuzi wa mibunge ya CCM! Wanawatetea ma-DC ili waweze kudhibiti wale watakaoshiriki kwenye mchakato wa uundaji wa Katiba mpya.

  Hata hivyo sidhani kama itawasaidia sana. Nafikiri wanajifurahisha tu.
   
 10. s

  sawabho JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Wote ni makada wa chama fulani cha siasa.
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ingekua ni chadema ndo chama tawala ccm wangeng'ang'ania hao ma Dc?
   
 12. T

  Tata JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Wakuu wa wilaya/Mikoa ni makada damu wa CCM, wanaoteuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM, wanamwakilisha Rais/mwenyekiti wa CCM kwenye mkoa/wilaya na ndiyo wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama kwenye mikoa/wilaya. Kwenye hizi kamati utakuta makamanda wa polisi wa mkoa/wilaya; maafisa usalama wa taifa mkoa/wilaya; makamanda wa jeshi, na vikosi vingine vya ulinzi na usalama. Hivyo kwa ufupi wakuu wa mikoa/wilaya ni makada wa CCM waliokabidhiwa rungu la dola kwenye mikoa na wilaya na lengo ni kuhakikisha maslahi ya CCM yanasimamiwa kwa kutumia nguvu ya dola kwenye mikoa/wilaya zao.
   
 13. B

  Bagumako Yoweli Member

  #13
  Feb 10, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kujua hilo uliza Fabian Massawe alifanya nini Bukoba kwenye uchaguzi uliopita mpaka akateuliwa kuwa RC.
   
Loading...