Jamani nina tatizo la kuogopa giza kupita kiasi (Nyctophobia), ushauri p'se! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani nina tatizo la kuogopa giza kupita kiasi (Nyctophobia), ushauri p'se!

Discussion in 'JF Doctor' started by Atabase Agaya, Feb 1, 2012.

 1. Atabase Agaya

  Atabase Agaya Senior Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wasalaamu kaka zangu na dada zangu wana JF.

  Mimi ni kijana mwanaume (36yrs) na nusu ya umri wangu nimeishi kijijini. Nabainisha hilo ili kuondoa shaka au dhana kuwa labda sikuzoea maisha ya kijijini. Nimezoea sana maisha ya kijijini na nakumbuka wakati ule hata umeme ulikuwa bado kusambazwa kijijini kwetu.

  Tatizo la kuogopa giza limeanza takribani miaka miwili iliyopita. Sijuhi chanzo hasa nini, lakini nakiri kuwa ni tatizo nililonalo na kadri muda unavyozidi kupita ndivyo uwoga unavyozidi!

  Nyumbani kwangu nimejiandaa kwa namna zote endapo umeme (National Grid) utakatika.

  Hali ya kuogopa giza kupita kiasi mara nyingi unitokea niwapo ktk chumba chochote ambacho umeme ukikatika ghafla usiku, nitashindwa kupata source yoyote ya mwanga. Mapigo ya moyo ubadirika na uwa najisikia kutaka kupasuka. Endapo nitakuwa nje ya nyumba au jengo na umeme ukakosekana, hilo siyo tatizo kwangu! Nikisafiri kwenda sehemu yoyote, lazima nibebe mishumaa kadhaa au taa ndogo ya ku-charge kwenye umeme (re-chargeable lamp).

  Mwenye kujua tatizo hili, naomba ushauri tafadhali.
   
 2. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole mkubwa.

  Hii kitu pia inanisumbua sana. Huwa nakosa hewa kabisa ikitokea niko kwenye chumba chenye giza usiku na hasa kama nitaamua kujilaza. Sijajua chanzo, lakini ni jambo ambalo linanipa tabu.
   
 3. Atabase Agaya

  Atabase Agaya Senior Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu, kumbe tuko wengi; Ebu tuwasilikize wataalamu maana JF ni mwisho wa maneno
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Mie nilikua zamani naogopa ila kwa sasa hapana
   
 5. Atabase Agaya

  Atabase Agaya Senior Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  King Kong III, ktk hali ya utoto, tatizo la Nyctophobia/Scotophobia ni kitu cha kawaida, lakini ktk umri huu tena ghafla,
  Inakanganya kidogo.
   
 6. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,659
  Likes Received: 5,252
  Trophy Points: 280
  Kuna vidonge vinaitwa "photosynthes" ndo'dawa na kinga tosha ya hilo tatizo. Angalizo vnamezwa usiku tu.
   
 7. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Jamani wataalam hebu tusaidieni.....im 26th na hii hali inanitesa mbaya! Huwa sizimi taa usiku na kama nipo sehem isiyo na umeme ndo balaa kabisa!? Jf doctors please!!
   
 8. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tatizo hilo linaitwa Nyctophobia na linatibika. Pole sana mkuu, tafuta professional advice. Na matatizo yetu ya mgao haya...
   
 9. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni maradhi ya akili yani akili zako zinanza kupungua ndo sababu.
   
 10. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  mmh! Na ww cku hizi ni docta???
   
 11. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Hee! Nilifikiri ni peke yangu kumbe tupo wengi,tunaomba madokta mtusaidie "HALI HII INATISHA"Mkuu pole sana.
   
 12. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,641
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  dah..pole mkuu,
  Jaribu kuangalia matukio ya nyuma...ni jambo gani liliwahi kutokea ukiwa gizani?
  inawezekana hofu na uoga unaoupata inatokea na tukio fulani/ kumbukumbu ya tukio la kutisha ulilowahi kupata.
   
 13. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Pole mkuu, jaribu kutafuta wataalamu.
   
Loading...