Jamani nimetapeliwa na mjasiriamali ambaye ni member wa huku

gayo

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
238
93
Bado siamini kilichotokea. Huyu jamaa nilishawahi kufanya naye biashara kama mwaka umepita. Kama miezi mitatu imepita alikuja kaka yangu akaona ile mifugo niliyoagiza kwa huyu jamaa akatamani naye aifuge hivyo akaniomba nimwagizie halafu nimtumie maana yeye anaishi Lindi

Nikaongea na huyu mjasiriamali akanihakikishia mzigo anao ndipo tukakubaliana nimtumie pesa kama laki 3 hivi ili autume. Baada ya kutuma hela jamaa akaanza sababu mara amekosa basi na hatimaye anauguza hadi leo nikimpigia simu hapokei wala hajibu SMS zangu.

Namtahadharisha kuwa dhuluma siyo nzuri kwenye maisha na atambue kuwa yatakuja kumtokea pabaya maana ameweza kunifanyia hivi mimi ambaye sitaweza kumfanya kitu ila atakuja kumfanyia mtu ambaye anapenda revenge. Mimi naamini zaidi kwenye KARMA

Asanteni

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mtaje...halafu unamtapelije mwenzio sh laki 3...mbona hela ndg hiyo kwann ujishushie hadhi...mm mtu akinitapeli huwa simfatiliii ndo kwanza Mungu huwa anaongeza kapu langu
 
Mtaje...halafu unamtapelije mwenzio sh laki 3...mbona hela ndg hiyo kwann ujishushie hadhi...mm mtu akinitapeli huwa simfatiliii ndo kwanza Mungu huwa anaongeza kapu langu

Laki 3 kwako ndogo ila kwa wengine ni kubwa sana!
 
Mods ... tunaomba mufanyie kazi tuhuma dhidi ya member wa forum hii, jf isije kuwa na sifa mbaya haswa katika jukwaa hili muhimu la ujasiriamali, pia ninashauri mleta mada achunguzwe pia ili asijekuwa anamchafua member wa jf pasipo ukweli

We need fair and justice in this saga

Moderators your task is to deliver a Verdict
 
siku zote huwa nasema nyuma ya fake id za users wa jf kuna siri kubwa sana.ukiachia id za mabingwa ktk nyanja mbalimbali, wahalifu nao hawako nyuma.kuna id za vibaka,matapeli,majambazi,mafisadi nk.tuchukue tahadhari.
 
Huyo atakua kitomari2..hata mimi kanitapeli lak 5 ya bata mzinga..kila siku usafiri hakuna nikamtuma mpaka mdogo wangu aarusha achukue hao bata mzinga kamkwepa na mpaka sasa hapokei simu.Nimesharipoti polisi na RB ninayo
 
Taja jina mkuu. Nimekereka sana, mtu mwenye tamaa za kipuuzi mi huwa ananikera. Jina tafadhali.
 
Huyo atakua kitomari2... hata mimi kanitapeli lak 5 ya bata mzinga..kila siku usafiri hakuna nikamtuma mpaka mdogo wangu aarusha achukue hao bata mzinga kamkwepa na mpaka sasa hapokei simu.Nimesharipoti polisi na RB ninayo

...pole sana mkuu!
 
Huyo atakua kitomari2..hata mimi kanitapeli lak 5 ya bata mzinga..kila siku usafiri hakuna nikamtuma mpaka mdogo wangu aarusha achukue hao bata mzinga kamkwepa na mpaka sasa hapokei simu.Nimesharipoti polisi na RB ninayo

Kitomari wa Tengeru Arusha au Mwingine!!
Huyu Kitomari wa Arusha sidhani kama anaweza kufanya vitu kama hivo.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom