Jamani nimetapeliwa na mjasiriamali ambaye ni member wa huku

Pole kwa kukwazika, na bado watu hawaelewi binafsi simsemi mtu ila nimepinga tabia ya wizi na kubeza au kudharau wengine. Tuko hapa kujikwamua na tunafikiri ktk umoja huu tunajengana na kuinuana. Sasa tukianza kushabikia wizi au kudharau watu wa chini sijui italeta picha gani. Mkuu tuko pamoja, tukikosa tunawekana sawa yanaisha.
Haya mkuu nisamehe, Tatizo nilivopost nikataja Kitomai watu wakanishambulia kuwa namtetea, aliyekuja kutoa clarification ni mwingine kabisaa mathematics , wewe ulitakiwa tu useme kuwa nimechanganya! BTW, pole sana, kwa hiyo aliyekutapeli ni nani mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Asante Mkuu kwa ufafanuzi, Kitomai adhurumu mtu laki3 ilikuwa hainiingii kichwani, ungeniambia kuanzia mill30 na kuendelea ingekuja kidogo akilini, nimeshachunguza mtu anayeuza bata humu ndani ni kitomari2, siyo Kitomai, sasa wote mnaoropoka mumtake radhi Kitomai, mnamchafuliana majina bure wakuu, wengine wanashabikia tu bila hata kufanya kautafiti hata kidogo wanapanua madomo tu, Kitomai hajawahi kuuza bata humu JF, Kitomari2 ndiyo anafanya biashara hiyo na mabango yake yapo mengi tu humu!

cc: Eberhard Mama Joe FairPlayer Mamndenyi gayo Kennedy neggirl



:nono:
 
Miezi mitatu tu tayari umekuja kumtangaza hapa je ingekwa miezi sita si ungefika hadi aljazeera?

Kweli kufanya biashara na masikini yataka moyo!


Haya mtaji hapa huyo mtu wako

Soma sheria za jf juu ya ufanyaji biashara ya hspa,


Swali: Je uliwahusha mods kabla ya kuanza hiyo biashara?

Kama ni kweli huyo Kitomari ana matatizo.Kwa nini asipokee simu au asijibu kama ana tatizo'? Na laki tatu ni nyingi kama huna ndugu lkn kwa nyinyi mabepari ni vijisenti
 
Kama ni kweli huyo Kitomari ana matatizo.Kwa nini asipokee simu au asijibu kama ana tatizo'? Na laki tatu ni nyingi kama huna ndugu lkn kwa nyinyi mabepari ni vijisenti

Jamaa kaja tena kuwashika kwa staili mpya, na tunavyo penda kushoboka
 
Kama ni kweli huyo Kitomari ana matatizo.Kwa nini asipokee simu au asijibu kama ana tatizo'? Na laki tatu ni nyingi kama huna ndugu lkn kwa nyinyi mabepari ni vijisenti

Jamaa aliyefanya uhuni ni kitomari2
Wizi ndani ya JF upo sana na mods washasisitiza jinsi ya kufanya bizness na mtu ndani ya JF,kuna jamaa anaitwa kitomari2 ni tapeli la kufa mtu ana ID kibao anaanzisha sredi kwa ID ya kitomari anajijibu kwa IDs nyingine zaidi ya 6 unaweza ukahisi jamaa ni muaminifu maana ID fake nyingine anajishukuru yeye kwa kujiuzia banta mzinga lol kuwa makini.


Ebu fungua hii sredi uone tapeli kitomari2 alivyo na ID lukuki sema mods wameziunganisha sredi kaanzisha yeye na anajijibu yeye!

~~~
www.jamiiforums.com/ujasiriamali/514230-bata-mzinga-wakubwa-kwa-wadogo.html
~~~~
 
Haya malalamiko hayana mashiko maana tungetegemea amtaje ili kuokoa wenzako.sasa hivi ni kama vapour
 
Ushauri wangu jf ni kiunganishi tu cha wajasiriamali.mimi siwezi kufanya biashara na mtu nisiyemjua kwa maana ya contacts.place of bness Legality na credibility yake kisa ni member hapa.fanyeni utafiti wa kutosha.resources are always scarce usiachie pesa kirahisi rahisi
 
sina nia ya kumtetea bwana kitomari2 ila nahisi atakuwa ameingiwa na tamaa ya kujipatia kipato bila kuwa na mzigo wa kutosheleza wateja wake. Binafsi nina experience nzuri naye ingawa hatujawahi kuonana. Nilimtumia pesa kwa m-pesa akanitumia vifaranga wengi kuliko thamani ya pesa niliyomtumia, nikamuona mwaminifu sana! akasema hivyo vilivyozidi nimtatutie pesa zake, nikaona poa sana. Tayari nimeishamlipa lakini bado ananidai pesa kidogo tu nimalizie hao waliozidi.

Sasa hizi habari za utapeli wake zimenikatisha tamaa sana kuendelea nae. Nahisi ananilia timing ndo anitapeli, nilimwambia najipanga then nimtumie hela anisafirishie mzigo mkubwa zaidi ya huu wa kwanza. Duh, imenikatisha tamaa sana aisee, nitamtafuta kwa simu nimwambie haya malalamiko maana mimi nikimpigia anapokea, hata nikituma sms ananijibu, nahisi bado narushiwa punje za mahindi niingie mkenge!!!!

Sasa mkuu usinge post,huyu angekamatwa kupitia kwako
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom