Jamani nimetapeliwa na mjasiriamali ambaye ni member wa huku

Ndio huyo wa arusha...amefanya so clearly ameweza.Mimi nisharipoti polisi kwani anaturudisha nyuma wahasiriamali wadogo kwa staili hii
 
Lakini Kwasheria Za Jf Ilikuwa Lazima Taaarifa Ya Biashara Ipitie Kwa Models, Hii Biashara Haita Wahusisha Jf, Rejea Taarifa Iliopo Kwenye Jukwaa La Biashara. Sema Kiubinadamu So Vizuri Na Nimshukuru Sana Ndaha Kwa Kumtaja Mwizi Huyu, Sikuwahi Kuamini Kama Sakata Lenu Litafika Hatua Hii
 
Asante ndaha, ni huyo huyo kanitapeli na mimi mkuu! Inauma sana maana bro anawaulizia naonekana kama mm siyo. Hyu jamaa kanifanya nimekuwa mbali na kaka yangu maana naona aibu

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Bado siamini kilichotokea. Huyu jamaa nilishawahi kufanya naye biashara kama mwaka umepita. Kama miezi mitatu imepita alikuja kaka yangu akaona ile mifugo niliyoagiza kwa huyu jamaa akatamani naye aifuge hivyo akaniomba nimwagizie halafu nimtumie maana yeye anaishi Lindi

Nikaongea na huyu mjasiriamali akanihakikishia mzigo anao ndipo tukakubaliana nimtumie pesa kama laki 3 hivi ili autume. Baada ya kutuma hela jamaa akaanza sababu mara amekosa basi na hatimaye anauguza hadi leo nikimpigia simu hapokei wala hajibu SMS zangu.

Namtahadharisha kuwa dhuluma siyo nzuri kwenye maisha na atambue kuwa yatakuja kumtokea pabaya maana ameweza kunifanyia hivi mimi ambaye sitaweza kumfanya kitu ila atakuja kumfanyia mtu ambaye anapenda revenge. Mimi naamini zaidi kwenye KARMA

Asanteni

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Mchane na jina hapa... hao matapeli ndo wakuwaumbua humu
 
Mtwa mimi nimemleta hapa baada ya kumtext na kumweleza nitakuja huku ili kusaidia na wengine. Hakunijibu alionyesha amedhamiria kudhulumu. Naomba tumjadili maana yeye ndiyo alikuwa kivutio cha wajasiriamali wadogo kutokana na kuwa na michango mingi hapa. Mambo anayotaka kuanza yatamfanya akose uhalali kabisa.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Na wewe mjinga kweli kutapeliwa kisha unaficha ficha jina. Safi kabisa ulivyofanyiwa. Hakuna tambarare bongo
 
Asante FairPlayer!

Jina limeshatajwa mara mbili sema husomi uzi vizuri! Nadhani siyo vyema kufurahia mwenzako akipatwa na matatizo.

Tapeli wangu ni Kitomari2 wa Tengeru

Karibuni mchangie

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Miezi mitatu tu tayari umekuja kumtangaza hapa je ingekwa miezi sita si ungefika hadi aljazeera?

Kweli kufanya biashara na masikini yataka moyo!


Haya mtaji hapa huyo mtu wako

Soma sheria za jf juu ya ufanyaji biashara ya hspa,


Swali: Je uliwahusha mods kabla ya kuanza hiyo biashara?
 
Miezi mitatu tu tayari umekuja kumtangaza hapa je ingekwa miezi sita si ungefika hadi aljazeera?

Kweli kufanya biashara na masikini yataka moyo!


Haya mtaji hapa huyo mtu wako

Sasa we ulitaka akae kimya wakati mtu amekata mawasiliano, kusema ukweli jasho la mtu haliliwi bure, huyu Kitomari lazima apate adhabu
 
Asante FairPlayer!

Jina limeshatajwa mara mbili sema husomi uzi vizuri! Nadhani siyo vyema kufurahia mwenzako akipatwa na matatizo.

Tapeli wangu ni Kitomari2 wa Tengeru

Karibuni mchangie

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Ungeweka wazi toka mapema. Polee
 
Wewe Yericko una dharau sana ila hazitakufikisha mbali. Ww tajiri imekusaidia nini?Lengo langu la kumleta hapa nikusaidia na wengine ili yasije yakawapata yaliyonikumba. Ndiyo tunavyosaidiana.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Yani hili swala ingetakiwa likemewe kwa hali ya juu kabisa na ikibidi iwekwe sticky ya matapeli wa JF kama sio kupigwa ban kabisa!!
Ofcourse ikisha thibitishwa kuwa kweli wametapeli!
Wasituharibia forum hapa!
 
tuwe makini usifikir kwa vile mtu yuko jf bas ni malaika, hii ni jamii wapo mpaka majambazi humu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom