Jamani ni course gan itamfaa mtu alie pata D masomo yote isipo kuwa mathe amepata F

Aende kusoma kozi za biashara.
akasomee.
1. Uhasibu
2. Procuremen
3. Business administration
4. Acconting in public sectors

At least hata akikosa ajira kwa kozi hizo apo anaweza kujiongeza kujiajiri.

Chuo cha kusomea aende
TIA (uhasibu)
AIA
IFM
...nimtakie kila la kheri
Sasa atasoma vp uhasibu wakati hata crediti ya mass hana
 
Na hesabu za kule sio ngumu sana, business mathematics anatoboa mana ataenda kusoma statistics,matrix,rate and exchange,sequence and series na algebra kidog kwenye somo la hesabu na hawaingii deep sana,
kwenye somo la finance yapo maelezo kibao atamudu hesabu atakazokutana nazo ni za kawaida sana capital budgeting,working capital, risk and return hapo kamaliza, akija kwenye economics hapa ni hesab za kujulmish kutoa na kugawanya sio ngum., account pia sio ngumu.
Ila akienda huko kwenye sayansi na matokeo yake hayo lazma atapata tabu mno.

Anaenda hata kama hajafaulu hesabu, kulingana na muongozo wa TCU,
mkuu ulipita chuo gani?? nimependa economics uliyo isoma
 
Kwa sasa ile notion ya kusema usome ili upate ajira, sijui kozi gani ni nzuri ili uajiriwe, hiyo haipo kwa sasa, mana kila kona kwa sasa wanalia ajira, si daktari,mhandisi, sheria,kote kugumu.

Kwa sasa mtu anasoma anachokipenda mana ukimchagulia mtu inawezkana hicho unachomchagulia hakimudu, tunaangalia utayari wa yule msomaji kwanza halaf ndo mambo mengine hufuata.

Bt anyway mfano mm angekuwa kaka yake ningemshauri asome;

1. Business administration kwa sasa, kwanin? kwasababu ndio koz ambayo ukisoma hata ukiwa na mtaji wako unajua pakuanzia mana utakuwa unaijua biashara kiundani na pia huwa ina ajira sekta zote mana mtu huyu anakuwa multi purpose kwenye zile soft activities za kozi yyte ya business, namaanish anawez kufany kaz kama mhasibu, afisa manunuzi, marketing, na zngine nyingi.

2. Ningemshauri achukue professional courses mfano achukue procurement and logistics management akimaliza hapo akapige mitihani ya bodi ya PSPTB , hapo atakuwa na uwanda mkubwa wa kufanya kazi ndani na nje ya nchi, nn maana ya procurement kwa kifupi? ni kozi ambay imebase kwenye manunuzi, inamaana anafanya kazi kama procurement officer, store officer na hata badhi ya kazi za transportation officer, labda nikwambie kitu, hakuna kampuni ambayo hainunui kutunza na kusafirisha, zote znafanya hivyo kwahiy ukisoma kozi hii unakuwa na uwanda mkubwa.

3. Ningeshauri asome accounting hapa akimaliza akapige mitihan ya bodi apate CPA akitoka hapo kama hatoajiriwa anaweza kufungua accounting firm akawa anafanya hata kazi za auditing kwemye taasisi mbalimbali.

NB: asiwaze kuajiriwa, mana ajira mtaani ni ngumu kiukwel yeye afocuss kile anachofundishwa akielewe na asikariri nikimaanisha hata akiwekwa kwenye interview anakuwa marketable. Na pia hata asipopata ajira ile elimu yake aweze kuitumia kumfanya awe na maisha mazuri..

kila la kheri.
Asnt sana ntatendea kaz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom