Jamani naombeni mnisaidie hata kazi za ndani kwa hapa DSM

EveningStar

JF-Expert Member
Nov 14, 2018
262
162
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 29, nipo DSM, elimu yangu ni shahada ya kwanza ya sayansi ya chakula na teknolojia, muaminifu na mchapakazi.

Nimetafuta kazi kwa muda mrefu sana pasipo mafanikio, jamani mimi nina shida kubwa sana, kwanza sina sehemu ya kuishi, ninalala ukumbini kwa ndugu, chakula ni kwa shida pia.

Jamani naombeni kwa yeyote yule mwenye kazi yoyote halali ikiwemo kazi za ndani nipo tayari kuifanya bila kujali elimu yangu. Kwahiyo naombeni mnisaidie jamani, mimi kwasasa nataka kazi bila kujali malipo ya aina gani, kikumbwa nipate tu pakulala na chakula kwa maana nimechoka kulala ukumbini jamani maana tangu 2015, nilipomaliza chuo, sasa nimechoka jamani nisaidieni.

Mawasiliano yangu, 0758 106 501

Ahsanteni na MUNGU awabariki!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Broo yule jamaa niliekuconect nae uliishia wapi?? Hukunipa feedback

Vrou van samaria give me bit of water to drink
 
Ajira zenyewe ziko wapi sikuhizi? acha mawazo ya kuajiriwa, jiajiri anza ata na mradi wa karanga tu
 
Mkuu acha kuwaza maswala ya kuajiriwa, muda wote uliopoteza tangu 2015 hadi sasa ni mda mrefu sana, anza kujiajiri ata kwa kuuza karanga mkuu au maji. Mtaji hauzi elfu 10. Ungewaza kujiajiri tangu ulivyo maliza chuo ungekuta sasa hv unaajiri vijana wenzako. Ukitaka kufanikiwa kimaisha usiwaze kuajiriwa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Broo yule jamaa niliekuconect nae uliishia wapi?? Hukunipa feedback

Vrou van samaria give me bit of water to drink
Kwanza Samahani ndugu kwa kutokupa feedback, ulinisaidia sana kunipa taarifa.

Kuhusu yule jamaa, mimi nilimtumia CV yangu pamoja na vyeti kwenye email yake. Nikaendelea kumfuatilia akaniambia nisubiri kwanza.

Baada ya kupita muda mrefu bila majibu yoyote kutoka kwake, ikabidi nimtafute, kumtafuta akaniuliza kwa mshangao, kweni haukuitwa?, mimi nikamjibu sikuitwa na nani?, akaniambia ile CV yako na vyeti nilimtumia jamaa mwenya kazi na kuniambia atakutafuta basi ngoja nimuulize.

Sasa baada ya jibu hilo ndiyo kimya mpaka leo ndugu na mimi wala sikumtafuta tena, nahisi kama nitamsumbua tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa broo pole sana

Kauli hii rahisi sana kuongea kama wewe una kianzio, unakaa kwa wazazi, ulibahatika kupata kazi haraka, umeajiriwa, ulikuwa na kila kitu wakati unaanza kujiajiri hukutegemea kwa kila kitu hicho kidogo ulicho anza nacho kama mtaji.

Kuna mwingine akipata hata hiyo 5000 ndio anapata sabuni ya kufulia na chakula au matibabu zahanati za serikali.
 
Umezungumza kweli mkuu, vibarua vya viwandani vyenyewe ni shida kuvipata, ukipata leo kesho unakosa hata siyo vya uhakika yaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu acha kuwaza maswala ya kuajiriwa, muda wote uliopoteza tangu 2015 hadi sasa ni mda mrefu sana, anza kujiajiri ata kwa kuuza karanga mkuu au maji. Mtaji hauzi elfu 10. Ungewaza kujiajiri tangu ulivyo maliza chuo ungekuta sasa hv unaajiri vijana wenzako. Ukitaka kufanikiwa kimaisha usiwaze kuajiriwa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
ni kweli mkuu,wazo lako ni zuri,nakumbuka baada ya kumaliza chuo,nilianza kuuza chapati,na nilipata hili wazo sababu kipindi chote nilipokuwa nasoma niliona wanafunzi wanapata shida ya vitafunwa(niliishi off campus) na nilianza na mtaji wa elfu 20(elfu 10 nilinunulia chuma cha chapati,hotpot na 10 nyingine nilinunua mahitaji kwa ajili ya chapati i.e unga,mafuta,chumvi etc)
Kwa siku nilitengeneza chapati 40 na zaidi na kila chapati niliuza 300,na usiku nilipika kwa special odder..
 
Mkuu acha kuwaza maswala ya kuajiriwa, muda wote uliopoteza tangu 2015 hadi sasa ni mda mrefu sana, anza kujiajiri ata kwa kuuza karanga mkuu au maji. Mtaji hauzi elfu 10. Ungewaza kujiajiri tangu ulivyo maliza chuo ungekuta sasa hv unaajiri vijana wenzako. Ukitaka kufanikiwa kimaisha usiwaze kuajiriwa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
msaidie basi huo mtaji wa elfu kumi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nenda kwa Azam kwenye viwanda vyake vya vyakula na vinywaji unatapata kibarua.

Tena kwako ni rahisi sababu ya ulichosomea na dini yako.

Au kajaribu pale Ubungo Terminal kama unaenda Maziwa kuna kiwanda cha mabomba kaombe kazi ila unaanza na kazi ya shuruba kuchekecha mchanga unaowekwa kwenye mabomba.

Au nenda kwa MO kaombe kazi viwandani kwake.
 
Mkuu acha kuwaza maswala ya kuajiriwa, muda wote uliopoteza tangu 2015 hadi sasa ni mda mrefu sana, anza kujiajiri ata kwa kuuza karanga mkuu au maji. Mtaji hauzi elfu 10. Ungewaza kujiajiri tangu ulivyo maliza chuo ungekuta sasa hv unaajiri vijana wenzako. Ukitaka kufanikiwa kimaisha usiwaze kuajiriwa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ningependa iwe hivyo, ushauri ni mzuri ila tatizo ni hali niliyokua nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nenda kwa Azam kwenye viwanda vyake vya vyakula na vinywaji unatapata kibarua.

Tena kwako ni rahisi sababu ya ulichosomea na dini yako.

Au kajaribu pale Ubungo Terminal kama unaenda Maziwa kuna kiwanda cha mabomba kaombe kazi ila unaanza na kazi ya shuruba kuchekecha mchanga unaowekwa kwenye mabomba.

Au nenda kwa MO kaombe kazi viwandani kwake.
Mkuu wazo lako ni zuri, miongoni mwa hivo viwanda ulivovitaja nilisha kwenda hasa kwa azam, muhzar, kwa azama nilihangaika mara kadhaa sikufanikiwa wana watu wao wa kudumu, kwa murzah vibarua siyo vya ukakika leo unapata, kesho nakosa au unweza kosa week nzima au kwa week unabahatisha siku moja au mbili. Yaani ni changamoto kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom