Jamani naomba msaada, nimeandaa bwawa nataka nifuge samaki nisaidieni mbegu nzuri ya kufuga

Sagejo

Member
Aug 12, 2014
8
45
Jamani naomba msaada, nimeandaa bwawa nataka nifuge samaki.

Nisaidieni mbegu nzuri ya kufuga.
 
KIMARA BRIDGE

Senior Member
Jul 31, 2015
135
250
Chuo cha uvuvi au taasisi yoyote ya serikali simshauri. Aende kwa wazalishaji binafsi akachukue. Akipata mbegu ya dume tupu (YY) itafaa zaidi
HDMI ebu dadavua kigodo, namake wengine tunawaogopa watu binafsi kwa sababu wanadanganya sana.
 
HDMI

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
592
1,000
HDMI ebu dadavua kigodo, namake wengine tunawaogopa watu binafsi kwa sababu wanadanganya sana.
Kuna wazalishaji binafsi ambao wako vizuri. Mimi natumia sana vifaranga kutoka Bigfish (Kigamboni) au ukiweza Ruvu Fish Farm (Mlandizi)

Tatizo la serikali ni kwenye huduma baada ya kukuuzia. Kama unavojua ni wasanii sana. Ukiwaita site wakushauri hata kwa malipo kidogo wana jeuri sana. Wao wakishakupa control number ukalipia vifaranga jua ndio mmemalizana
 
KIMARA BRIDGE

Senior Member
Jul 31, 2015
135
250
asante mkuu, nimekuelewa. inaonekana hawa watumishi wanamastress yao ya kazini na wanafanya as usual hawataki kujiongeza.
 
Sagejo

Member
Aug 12, 2014
8
45
Chuo cha uvuvi au taasisi yoyote ya serikali simshauri. Aende kwa wazalishaji binafsi akachukue. Akipata mbegu ya dume tupu (YY) itafaa zaidi
Ahsante sana kwa ushauri wako nashukuru ndugu yangu
 
KIMARA BRIDGE

Senior Member
Jul 31, 2015
135
250
Nipo mbeya ndugu yangu, labda kama unafahamu sehemu yoyote huku naomba nielekeze
mimi niko Dar, kwa mikoani sina ideas yeyote labda ufunge safari au wasiliana na Bigfish au Ruvu fish farm kama HDMI alivyoshauri, ili uone kama wanaweza kukusafirishia huko ulipo.
 
Kitto Sr

Member
Jan 14, 2016
28
75
Nipo mbeya ndugu yangu, labda kama unafahamu sehemu yoyote huku naomba nielekeze
Kama uko mbeya mjini.. Nenda Iyunga kalobe, kuna jamaa anafuga sana samaki na ana hivo vifaranga vya kutosha
Atakushauri vizuri.kwenye Google map ukiangalia hiyo kalobe utaona location inaonekana
 
Sagejo

Member
Aug 12, 2014
8
45
Kama uko mbeya mjini.. Nenda Iyunga kalobe, kuna jamaa anafuga sana samaki na ana hivo vifaranga vya kutosha
Atakushauri vizuri.kwenye Google map ukiangalia hiyo kalobe utaona location inaonekana
daaaah ahsante sana ndugu yangu nitaenda, mimi nipo hapa iyunga
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom