Jamani Naomba Msaada Nikivua Nguo (t Shirt) Inapiga Shoti.

Hii mi naona ipelekwe kule jukwaa la joke.

hii sio utani.
Katika elimu ya Fizikia kuna elimu umeme inayoitwa "Static Electricity".
Mfano tukiwa shule ya msingi tulikua na mtindo wa kusugua kalamu kikwani kwenye nywele halafu tunaigusisha kwenye vipande vidogo vidogo vya makarakasi, ulikua unaona vikaratasi vinavutwa mithili ya sumaku inavyovuta chembe chembe za chuma. Miili yetu na vitu vyote visivyopitisha umeme na vinavyopitisha vina asili ya chaji chanya na chaji hasi. Unaposugua kwa muda kifaa chochote katika mwili au sehemu nyingine yenye chaji, moja kwa moja unazifanya chaji zijipange kuelekea mwelekeo mmoja vile vile chaji hasi na chaji chanya hutengana na kutengeneza pande mbili.

Hivyo kwa kutumia elimu kama hiyo, msuguano uliopo kati ya vinyweleo vya mwili na hiyo T-shirt yako hutengeneza kitu kama hicho, tukio ambalo wewe utaliona kama mwanga(cheche) au utasikia kama sauti. Sauti au mwanga unaotoka ni matokeo ya mbadilisho wa nishati umeme kwenda nishati mwanga au sauti.

"Energy can neither be created nor destroyed but it can be transformed from one form to another".
 
jaribu yafuatayo:

Weka balbu moja ya wat 20 ikiwak atu ujue unao umeme..utumie huo kuchajia simu na kupigia pasi..utapunguza bili za mwisho wa mwezi..duh..ila isijekua unakaribia kufanana na yule dogo mwenye macho ya X-ray..
 
Jamani Si Utani Ninatatizo Kila Nikivua Tshirt Inatokea Cheche Kama Vile Kupiga Shoti Je Hii Ni Nini?

Hapana jamani msimcheke mtoa mada,hii phenomenon ni real,inaitwa static electricity,inatokana na kusugua baadhi ya vitu,mfano ukisugua rula ya mbao kisha ukaigusisha pini inainyaka kama sumaku,hata kwenye material ya baadhi ya mablanketi ukiyavuta ujifunike yanakupiga kau meme. Mavella,usishangae ni jambo la kawaida na si mijuiza,ni electrons zinakuwa zimeji expose.
 
Daaah! hii kali inawezekana unatembea na mionzi hatari ya nyuklia...fanya hima usije ukalipuka muda wowote.
Usihofu angalia material ya t-shirt labda yana chembechembe za umeme, ni t shirt tu au hata suruali na nguo nyingine?
 
Back
Top Bottom