Jamani naomba msaada ,kipi utapenda ndoa/harusi yako iwe navyo kati ya hivi?

LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,389
672
Huwa nashindwa jua ni kipi hasa mtu atajiona anafurahia ndoa yake kati ya hivi na kujiona kaoa au kaolewa

  1. upate baraka za watumishi wa mungu islam na ukristo (sijui kwa wapagani)
  2. upate cheti cha ndoa
  3. uwingi wa watu katika sherehe za harusi yako
  4. michango mikubwa katika harusi yako
  5. kutumia hammer kuanzia wapambe hadi mashabiki
  6. kuzurura na magari mji mzima wakati wa sherehe yako
  7. ndoa ya maharusi na wadhamini na mfungishaji tu, iwe kanisani, msikitini au bomani
  8. watu wale hadi wamwage chakula na vinywaj waoge kabisa
  9. kasherehe kadogo nyumbani na ndugu zako juu ya harusi yako
  10. kuishi kwa amani na upendo katika ndoa yako hata kama hamja funga ndoa kidini au kimilana kiserikali lakin mnapendana kiroho na kimwili kwa dhati wewe na mkeo au mumeo
 
  1. Upate Baraka za Mungu Kupitia watumishi wake
  2. kuishi kwa amani na upendo katika ndoa yako hata kama hamja funga ndoa kidini au kimilana kiserikali lakin mnapendana kiroho na kimwili kwa dhati wewe na mkeo au mumeo
 
Namba 10 ndo inayohitajika. Vyeti, baraka, nk ni vitu visivyo na msingi wowote. Mbona 1-9 enzi hizo havikuwepo na bado ndoa zilidumu na kunoga?
 
Mimi nadhani 1, 2, 9 na 10 zinahusika zaidi kwa pamoja ama moja moja.

Namba 5 inahusika kama wataka kutengeneza documentary na jina mitaa flani.

Namba 8 si mbaya kama uwezo waruhusu na vipaumbele vyako vya msingi umevitimiza. Kumbuka hii ni once in life time (kama worldcup south africa 2010 teh teh)

3 na 4 zaweza kuwa ni litmus test ni nafasi gani ulonayo katika jamii na wanajamii wanakuchukuliaje
 
Back
Top Bottom