Elections 2010 Jamani nagombea ubunge Babati Mjini kwa tiketi ya CHADEMA 2015

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,973
9,567
WanaCHADEMA HAKUNA KULALA, VIJANA TUJITOKEZE KUCHUKUA MAJIMBO AMBAYO YANAONGOZWA NA VIHIYO WA CCM. MIE NGUVU ZANGU NIMEZIELEKEZA BABATI MJINI MWAKA 2015. WASOMI TUSIPENDE KUNG'ANG'ANIA MJINI, TUJITOKEZE KWA WINGI KULETA CHANGAMOTO YA MAENDELEO, NA MJUE VIJANA NI TAIFA LA LEO.
KWA KUANZIA, TUWAHAMASISHE VIJANA AMBAO NI ASILIMIA 80 YA WATANZANIA KUJIANDIKISHA NA KUSHIRIKI KUPIGA KURA.
 
Nakushauri uwe FIT..... maana unaweza kuchakachuliwa na hali ikiwa TETE utajikuta umelazwa baada ya kuangushwa kwenye uchaguzi..
 
Mwanzo wa ngoma unaanza; nimependa maandalizi ya mapema; promiss if you dedicate you will get the constituency. nice
 
nakuunga mkono....mimi najipanga kugombea udiwani 2015....2020 nitakuwa mbunge rasmi.....kwa tiketi ya chadema ofcoz......jimbo nitakabidhiwa na mheshimiwa Lema
 
Nakushauri uwe FIT..... maana unaweza kuchakachuliwa na hali ikiwa TETE utajikuta umelazwa baada ya kuangushwa kwenye uchaguzi..

Sitaweza kuanguka kwa maana sina chakupoteza, la msingi nikuweka maslahi ya nchi mbele, watu waelewe sera.
Kiongozi wa kuanguka na kulazwa huwa ni yule anayefikiria maslahi yake kuwa atakuwa peponi, hivyo CHADEMA nina imani hawako hivyo, ndiyo maana Majimbo yanayoongozwa na CHADEMA yapo juu Kimaendeleo.
 
nakuunga mkono....mimi najipanga kugombea udiwani 2015....2020 nitakuwa mbunge rasmi.....kwa tiketi ya chadema ofcoz......jimbo nitakabidhiwa na mheshimiwa Lema

Mpiganaji Lema ndiyo sisi tumemchagua upo na mimi sawa kabisa, mie nililalia masanduku ya kura mpaka asubuhi, nilinakili mpaka namba ya seal iliyotumika kufunga masanduku.
 
Mkuu hata mimi nakuunga mkono kwa hilo cha msingi ni kuanza maandalizi sasa hivi usisubiri 2015 ndio uanze kujiandaaa, na mimi ngoja nitafute jimbo tena haswa ile mikoa ambayo upinzani hawajapata hata mgombea mmoja
 
Mpiganaji Lema ndiyo sisi tumemchagua upo na mimi sawa kabisa, mie nililalia masanduku ya kura mpaka asubuhi, nilinakili mpaka namba ya seal iliyotumika kufunga masanduku.

pamoja mkuu......tutahakikisha sasa tumeshirikiana na vijana (kuanzia madiwani) mpaka kwa muheshimiwa mbunge ili wachakachuaji wakose cha kusema....najua wanasubiri mapungufu......hilo limekula kwao
 
Naenda kuanzisha miradi ya maendeleo katika kata yangu Getar na Haydom. Ninaandaa mipango ya miaka mitano ijayo. Maeneo muhimu ni mazingira, kuanzisha mafunzo ya ujasiriamali, makazi bora vijijini, Kilimo na ufugaji wa kisasa.

Jambo lingine ni uanzishaji wa elimu ya uraia katika vijiji mbalimbali katika kata hizo mbili.

Wakitaka mimi kugombea nitakuwa tayari, ila malengo yangu nikuwahamasisha watu kujileta maendeleo wanayoyataka.
 
pamoja mkuu......tutahakikisha sasa tumeshirikiana na vijana (kuanzia madiwani) mpaka kwa muheshimiwa mbunge ili wachakachuaji wakose cha kusema....najua wanasubiri mapungufu......hilo limekula kwao

Kweli kabisa dada Preta, kwakuwa tumeshalikamata Halmashauri ya jiji la Arusha, na ninajua bila shaka kwa kampeni tunazoziendesha Meya atakuwa Estomi Mallah, vijana wa CHADEMA wapo makini sana, kwa sasa wanajiandaa kuchukua kata zilizo mikononi mwa ccm, kwa kuleta maendeleo kwa vitendo katika kata zao.
 
Naenda kuanzisha miradi ya maendeleo katika kata yangu Getar na Haydom. Ninaandaa mipango ya miaka mitano ijayo. Maeneo muhimu ni mazingira, kuanzisha mafunzo ya ujasiriamali, makazi bora vijijini, Kilimo na ufugaji wa kisasa.

Jambo lingine ni uanzishaji wa elimu ya uraia katika vijiji mbalimbali katika kata hizo mbili.

Wakitaka mimi kugombea nitakuwa tayari, ila malengo yangu nikuwahamasisha watu kujileta maendeleo wanayoyataka.

Haydom kuna wapiganaji wa CHADEMA, ila kuna kata jirani pale inaitwa kata ya UFANA, pale wamejaa vihiyo wa ccm, naomba ukawasaidie wale jamaa. Nakuunga mkono ndg yangu.
 
Kila laheri wadau! Hope mtafanikiwa na uzoefu mlio upata mwaka huu mta utumia vizuri,
Mnweza kumtafuta Mdee awape siri ya mafanikio Kawe kwani inaonekana alisha anza siku nyingi kuwasaidia watu wa kawe!
 
Mwenyekiti wa Nec 2015 atakua jaji Riziwani. Amepata uzoefu wa kutosha kwenye kuchakachua kura.
 
KWA KUANZIA, TUWAHAMASISHE VIJANA AMBAO NI ASILIMIA 80 YA WATANZANIA KUJIANDIKISHA NA KUSHIRIKI KUPIGA KURA.

Mwaka huu kuna watu zaidi ya MILIONI NNE (4,000,000) HAWAKUYAONA majina yao kwenye vituo mtu wangu. Ndo taabu ya kuleta mizaha wakati wa zoezi nyeti kama hili.

Kuna haja pia ya kuibinafisha NEC kwa WAKOLONI tu
 
yaani nimesikitika sana nilivyosikia Babati imechukuliwa na ccm...
but good things take time...
yaani hongera sasa kwa kutaka kuchukua babati...
tuzidi kuomba na utafanikiwa....
tutarudi home(TZ) kukusaport.....
especially sisi wazaliwa wa hapo Babati inabidi tuungane na tujitokeze tumsaport huyu mwenzetu.....
 
nakuunga mkono....mimi najipanga kugombea udiwani 2015....2020 nitakuwa mbunge rasmi.....kwa tiketi ya chadema ofcoz......jimbo nitakabidhiwa na mheshimiwa Lema

YOU GO GIRL................
safi sana naamini chadema itachukua nchi
tukiwa na watu mashuja kama nyie
POWER TO U ALL
 
Mwenyekiti wa Nec 2015 atakua jaji Riziwani. Amepata uzoefu wa kutosha kwenye kuchakachua kura.

Aiseh! Umejuaje? yaani una akili wewe! wameanza na kumpa uadvoketi (sidhani kama anastahili) sasa muda si mrefu baba yake atamtangaza Jaji halafu baada ya miaka miwili anastaafu then anakuwa appointed Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi. Uzoefu anao, kuanzia alipokuwa makamu mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi yanga akachakachua uchaguzi wetu na kutudanganya kuwa katumwa na JK kutuambia lazima tumchague Llyod Nchunga hawakati hakuwa chaguo letu. Huyo dogo hovyo sana!
 
Jamani mimi 2015 jimbo langu la Mbulu ndiyo nitaliongoza kwa kuwa moja ya majimbo ya uwekezaji hapa nchi jamani mshikamano ni muhimu sana,Naunga mkono 100%
 
Back
Top Bottom