Jamani mke huyu!

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Rafiki yangu amebahatika kumpata mwenza wake wa maisha na ni mwaka wa tatu sasa tangu wapo kwenye ndoa.Tangu waoane na mwanamke huyu,furaha ya rafiki yangu imekuwa kubwa lakini yenye kuchanganyika na wasiwasi mkubwa.

Ni kawaida kusikia wanaume tunasema lazima mwanamke awe soft na mwenye mikono laini.Lakini kwa mwanamke huyu hali ni tofauti.Rafiki yangu akileta magunia ya mkaa mwanamke anabeba bila hata msaada wa mtu yeyote.Kuna nyumba wanajenga,nje kidogo ya jiji,wakati wa kwenda kununua mbao,matofali na simenti mwanamke alibeba mwenyewe.Mbaya zaidi mwanamke huyu akiamka saa kumi na moja kamili yeye ni tizi kwenda mbele.Ameaandaa kijimu cha kishikaji upenuni mwa nyumba na anapiga tizi mpaka rafiki yangu huyu anaogopa.
Katika mambo fulani jamaa anasema mkewe hachoki,ule usoft wa mikono na mwili mzima ndo basi tena haupo.Lakini cha kufurahisha zaidi mtaani hapo hakuna anayethubutu kuleta fujo,maana anagawa dose kama hana akili nzuri.Rafiki yangu ametokea kuwa na adabu ya kupitiliza.Amani imekuwa haba kwa rafiki yangu.
 
Huyo ni mwanamke shupavu na ndo anafaa.
mwambie rafiki yako asimwache.
Mwanamke kama huyo ukimwacha hom unakuwa hauna hofu juu ya usalama wa nyumba na mali.
Hata mkivamiwa una uhakika wa kushinda pambano.
 
Huyu ndio mwanamke sasa,tatizo la wanaume Wakibongo tumezoea wanawake walegevu legevu wasioweza kufanya kazi yoyote ngumu, i wish angekuwa mai waifu, mshikaji ana sababu ya kuwa na hofu bali amshukuru Mungu kwa kumpa mke shupavu.
 
mmh!! kufanya mazoezi ni sawa kabisa, hata kama anacheza magujuruu mi naona poa tu.
Lakini kubeba magunia ya mkaa na masement adharani naona ni unanihiii flani hivi.
Anajaribu ku-prove nini na kwa nani?
 
salaam muafaka kwa noname................... noname please njoo ukoment hapa......... manake nikuambia mwanamke kazi unasema siyo mapenzi............... haya huyu mwenzanu kaatoa kimasomaso .................. anafaa sana............ ngoja nikamfundishe na wangu mazoezi.................
 
mwambie aache ushamba! na akijizubaisha watampata wanaoweza kuitumia hiyo fursa.................

Jamani ndio maana wanaitwa wenza! kwa nini hatuelewi hili?

Nitatoa mfano; ni mtu nayevutiwa na mazoezi lkn kuna wakati nilijiachia sana na mwenzangu kumbe hakuwa anafurahia hiyo hali alianzisha mkakati wa mazoezi ya kukata tumbo nami nikamfuata! tunafanya mazoezi lkn ukweli yeye ndo anafanya zaidi yangu na hata misuli yeye inamtoka vizuri tumboni kunizidi hii ni challenge nzuri!
 
Kwa kweli sijaona shida bado, sasa amani imekuwa haba kwa nini? Anaogopa kupigwa? Hayo matofali anashusha mwenyewe kwenye lori au anafanya kusogeza tu yaliyopo chini kwa hatua chache? Magunia ya mkaa yanabebwa kichwani au mzegamzega au anaburuzia ndani tu? Mbona huyo kaka muoga hivyo? Na huyo mkewe angekuwa anaita wafanyakazi waje wasogeze hayo magunia ya mkaa angekuja na hadithi kuwa mkewe legelege, hata kusogeza gunia hatua mbili hawezi!
 
huyo mwanamke noma angalia sije akakutia kabali ktk mambo fulani ukilemaa au mkulya huyo
conquest
 
Brazo mwanamke wa shoka huyo.
Safi sana sasa hapo jamaa akitafuta nyumba ndogo atakiona cha mtema kuni.
 
Niseme kwa kifupi jamaa ametushushia hadhi wanaume; tuombee tu hajamtamkia shemeji yetu huo upuuzi wake!
 
Rafiki yangu amebahatika kumpata mwenza wake wa maisha na ni mwaka wa tatu sasa tangu wapo kwenye ndoa...

...mpaka hapo inatosha kwamba ndiye mke aliyemchagua yeye. Kampenda mwenyewe, usimchanganye rafikiyo na 'power-Mabula' wake bana.
 
kwa kweli sijaona shida bado, sasa amani imekuwa haba kwa nini? Anaogopa kupigwa? Hayo matofali anashusha mwenyewe kwenye lori au anafanya kusogeza tu yaliyopo chini kwa hatua chache? Magunia ya mkaa yanabebwa kichwani au mzegamzega au anaburuzia ndani tu? Mbona huyo kaka muoga hivyo? Na huyo mkewe angekuwa anaita wafanyakazi waje wasogeze hayo magunia ya mkaa angekuja na hadithi kuwa mkewe legelege, hata kusogeza gunia hatua mbili hawezi!

anabeba mpaka kituoni.hakuna cha kusogeza.mifuko ya simenti kama mitatu kwa wakati mmoja.
 
duh, huyo ni kama yule Zena wa SANI. Anaweza akalianzisha wakati wowote
 
Rafiki yangu amebahatika kumpata mwenza wake wa maisha na ni mwaka wa tatu sasa tangu wapo kwenye ndoa.Tangu waoane na mwanamke huyu,furaha ya rafiki yangu imekuwa kubwa lakini yenye kuchanganyika na wasiwasi mkubwa.

Ni kawaida kusikia wanaume tunasema lazima mwanamke awe soft na mwenye mikono laini.Lakini kwa mwanamke huyu hali ni tofauti.Rafiki yangu akileta magunia ya mkaa mwanamke anabeba bila hata msaada wa mtu yeyote.Kuna nyumba wanajenga,nje kidogo ya jiji,wakati wa kwenda kununua mbao,matofali na simenti mwanamke alibeba mwenyewe.Mbaya zaidi mwanamke huyu akiamka saa kumi na moja kamili yeye ni tizi kwenda mbele.Ameaandaa kijimu cha kishikaji upenuni mwa nyumba na anapiga tizi mpaka rafiki yangu huyu anaogopa.
Katika mambo fulani jamaa anasema mkewe hachoki,ule usoft wa mikono na mwili mzima ndo basi tena haupo.Lakini cha kufurahisha zaidi mtaani hapo hakuna anayethubutu kuleta fujo,maana anagawa dose kama hana akili nzuri.Rafiki yangu ametokea kuwa na adabu ya kupitiliza.Amani imekuwa haba kwa rafiki yangu.

mwambie awe makini huyo ni mwajuma ndala ndefu
 
sasa kama baba lege lege yeye afanye nini? utakuta huyo mshkaji wako kazidi ulegevu.
 
...mpaka hapo inatosha kwamba ndiye mke aliyemchagua yeye. Kampenda mwenyewe, usimchanganye rafikiyo na 'power-Mabula' wake bana.

dah umenikumbusha mbali mzee,Power Mabula nakumbuka alitokea Kyela kama sikosei,maana utotoni nlishawahi kumuona akifanya mavitu vyake vya kukaza kamba kwa meno gari haliondoki!
 
anabeba mpaka kituoni.hakuna cha kusogeza.mifuko ya simenti kama mitatu kwa wakati mmoja.

Mkuu, mada yako ili kuwa nzuri sana ila umeiaribu kwa kuzidisha uwongo ni vigumu sana kubeba mifuko mitatu ya cement,umenifanya nihisi hata story yenyewe ni ya kutengeneza tu haina ukweli wowote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom