Jamani mbuge wa Ukonga mhe. Eugean Mwaiposa amepotea

maph

Senior Member
Oct 16, 2012
177
50
Ndugu zangu naomba msaada wenu Mbuge wetu wa ukonga Eugean MWaiposa tunamtafuta sana kila sehemu lakini haonekani wala hapatikani mahali popote kama kuna mtu kamuona basi tunaomba atoe taarifa .......

Jimbo letu lina shida na maji hasa PUGU STATION -tunatumia muda mwibgi sana kutafuta maji , jamani tunaomba msaada wenu kwa yeyote anayeweza kutusaidia , mbugewetu sijuhi kama anajua hili tatizo kwa sababu hatumuoni wala kumsikia popote pale na sijuhi kama serikali inalijua hili tatizo hili miaka 52 ya uhuru lakini bado maji ni shida hapa km 21 kutoka mjini tena Wizara inayohusika na maji.

Itakuwani aibu kubwa kama huyu mbuge atakuja tena kutuomba kura 2015 na CCM kama mkimsimamisha tena mjue mtalikosa hilo jimbo.Eti yuko bize na Vikoba wakati maji ndo muhimu kuliko wote.pia najuta sana kwa kumpigia kura yangu sikujua haya yote . Tunaomba msaada basi hata apite pite maeneo ya huku mi sura yake nimeisahau kabisa .
 
Wabunge wote wa Dar wanaosikika ni John Mnyika peke yake wengine tutawasikia 2015 hasa hao wa Ukongo, Temeke na Segerea ndiyo balaa zaidi
 
Yupo huku Mbezi Beach anasimamia Hekalu lake,wewe usifanye mambo yako ya Msingi endelea kumtafuta na kumsubiri kama haujui magamba kuwa ni Mizigo.
 
Atakapopita hapa kuelekea kwenye shule yake ya Tumaini English Medium, nitakupigia simu umfuate fasta, huwa anapita pita hapa kwenda kwenye mradi wake huo. Niwekee mawasiliano yako kwenye PM
 
Ok, utakuwa umefanya jambo la maana sana kumbe hata kwa mapoti huko Kitunda wanamtafuta sana .....mi nilijua ni pugu tu .Ndugu fanya hivyo husije ukasahau .
 
...jimbo la Ukanga ni kama shamba la bibi, na kama si shamba bibi, basi NI NGAZI YA BABU...!

...makongoro wa ccm aliwadanganya danganya' baada ya kupata alichokuwa anahitaji, "akawaacha kwenye mataa". Sasa naye huyu mwanaCCM mwingine aliwadanganya danganya, mkampigia kura (kula) "anaazaKULA, mnaanza kulalama"

"...endeleeni hivyo hivyo...!"
 
Huyu mama hatutaki hata kumuona hii barabara ya mombasa kuelekea moshi bar haifai akija 2015 tutamtimua...
 
Sisi huku mikoani tangu uchafuzi uishe hawajaonekana,wamebadili hadi anuani zao wanatumia masanduku ya barua ya Dar,nasi mkiwaona huko wambieni watutembelee angalau kipindi hiki cha kuuaga mwaka.
 
Huyu mama hatutaki hata kumuona hii barabara ya mombasa kuelekea moshi bar haifai akija 2015 tutamtimua...

...Jerry Slaa, alishaga sema kuwa fedha ya barabara hiyo ilishaga tengwa kitambo..., kumbe fedha iliyokuwepo ni ya nusu kilomita tu...! loh ! "wajinga ndiyo, waliwao..."
 
Huyu mama hatutaki hata kumuona hii barabara ya mombasa kuelekea moshi bar haifai akija 2015 tutamtimua...
tehe tehe teheeeeee,mtamtimua kwa mayai viza au nyanya za masalo au mnamnyima kura....
 
Mama Mwaiposa anamaliza kopindi cha kwanza na cha,mwisho cha ubunge wake...kila mtu wa ukonga hajui alishindaje uchaguzi ule
 
Back
Top Bottom