Jamani mbona wahamihaji haramu ni wengi Sana Tz?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani mbona wahamihaji haramu ni wengi Sana Tz??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mayolela, Feb 4, 2010.

 1. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2010
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani,naomba wana JF tulijadili hili kwani kwangu imekuwa kero sana,yaani hata kazi za kuoika chai,karani,kufagia wapewe wahamihaji harum ,ambao wengi sana wanatokea Kenya.Naomba Idara ya Uhamihaji ifanye kazi ipasavyo,ndio hao sasa wanaongaika sana hili wapate hati ya kupigia kura kama raia ,jamani kweli tutafika- hata wazungu wengine wankuja kufanya kazi za ukarani tu hapa bongo,na permit zinatolewa kwa zaidi ya miaka miwili,nadhani sheria sio zaidi ya miaka miwili,utakuta mhamihaji kakaa hapa mpaka kanunua shamba sehemu.
  Tunaomba Idara husika itupie macho hili.Haswa kwenye hizi kampuni za kigeni hapa d,salaam.

  naomba tuoa hoja.(ili cctv isijeninasa,maana ndio haohao)>
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Feb 4, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,301
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Wizara ya mambo ya ndani na wizara ya kazi zimelala usingizi wa pono.
   
 3. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,645
  Likes Received: 418
  Trophy Points: 180
  Inabidi serikali iwe makini sana na watu kama hao!!
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,489
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Tusilaumu wizara ya mambo ya ndani peke yake. Ukimsikia rais wa Tanzania anasema hadharani kuwa Watanzania ni wezi na ndiyo sababu "wawekezaji" hawawaajiri, hii inawafunguliwa milango 'wawekezaji" kuleta kila Tom, Dick, and Harry na kuwapa kazi Tanzania kwa sababu wanajua hawataguswa. Chagueni serikali/viongozi makini.
   
 5. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,712
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kama wewe sio makini basi ujue serikali yako haitakuwa makini.
  umakini unatakiwa uwanzie kwako
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka kesi moja miaka michache ya nyuma nadhani kampuni ya Kioo ambayo ni Wahindi. Jamaa waliwaleta wahindi wenzao na kuwaingiza nchini kiharamu na wakapata ajira pale za nafasi za juu pamoja na kuwa walikuwa hawajui kiingereza wala kiswahili na wakawa wanawanyanyasa sana wazawa. Baadhi ya Wafanyakazi wazawa wakaenda kuwachomea Uhamiaji jamaa walienda pale na kupata bulungutu lao na wale wahindi wakaendelea kupeta pamoja na kuwa walikuwa nchini kiharamu.

  Wakongo, Wanyarwanda, Warundi, Waethiopia, Wasomali, Wahindi wa India, Bangladesh, Pakistan, Wachina na hata wazungu wanaoishi nchini kiharamu wanazidi kuongezeka kila siku na Wizara ya mambo ya ndani haiwachukulii hatua zozote kuhusu uvunjaji wao wa sheria za nchi.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Feb 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,523
  Trophy Points: 280
  Wahamiaji haramu wa Kitanzania mbona nao wengi tu kwenye nchi za watu...
   
 8. N

  Narumba Member

  #8
  Feb 4, 2010
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe Omega hapo juu kweli umenena nyie wenyewe mnaotoa comment hapa msikute mpo illegal kwenye nchi za watu. Hao illegal immigrant in Tanzania nao wanatafuta maisha kama nyie mnavyotafuta maisha huko majuu.Hebu acheni kuwasema kama vp rudini home muwafukuze.
   
 9. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,993
  Likes Received: 420
  Trophy Points: 180
  NCHI CORRUPT.... Aaah wacha niende zangu Leaders J'mosi kuzindua mradi wakupambana na Malaria... ZINDUKA...
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Watanzania wengi hawapendi purukushani katika nchi za watu. 99.9% ya Watanzania ninaowafahamu makaratasi yao yako bomba na wanaingia na kutoka bila wasiwasi wowote ule na wale ambao hawajapata makaratasi wanafuata njia halali ili kuhakikisha wanayapata makaratasi hao.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,489
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  So that makes it okay for Tanzania to turn a blind eye on this scourge?
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Feb 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,523
  Trophy Points: 280
  No, lakini watu wa Tea Party wakitaka hawa wahamiaji haramu watimuliwe nyinyi ma liberals mnaanza kulia lia ubaguzi
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Feb 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,523
  Trophy Points: 280
  Hmmmm....sijui wewe uko wapi mwenzangu....lakini huku tuliko sisi wengine ni viroja mtindo mmoja kuanzia watu kutokuwa na namba, kutumia majina na utaifa tofauti (eg. South African), etc.
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,486
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kujadili waTz waliopo nje wanaoishi bila kufuata sheria thats has nothing to do with topic in hand.
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,486
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  In actual sense matatizo mengi yaliyopo Tz yanasababishwa na state of anarchy. Kukosekana kwa dola imara yenye nia ya dhati ya kuindeleza nchi ndio msingi wa matatizo yote haya na yajayo.
   
 16. N

  Narumba Member

  #16
  Feb 4, 2010
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna lolote wala hawapati ukazi kihalali kuna watu wanajilipua kwa kujifanya wakimbizi ili wapate makaratasi. Wengine wanafunga ndoa za biashara na ni risk kweli kweli hadi wengine walikufa huko Detroit kwa kufunga ndoa za makaratasi na watu tofauti halafu wakapigwa risasi wote mtu na mchumba wake. Watu wanataabika majuu kuchonga namba au kutumia namba ya mtu. Waliopo marekani sasa hivi wanaomba tu obama awasaidie ili wapate hayo makaratasi.Kama huna makaratasi unasafa kweli kweli. Wapo wanaopata makaratasi kihalali bali ni wachache. Ila majority waliopo huko ni wale wanaoverstay baada ya hapo ni wanahaha kweli kweli kutafuta hayo makaratasi.
   
 17. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #17
  Feb 4, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unaonekana kuogopa mada ya waTZ wanaoishi nje illegally, Kwani shida iko wapi? Kama unataka kutendewa justice na wewe lazima utende justice.
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,489
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Achana na Tea Party. At least Marekani wana sheria zinazofanya kazi. Ukikamatwa unabangaiza illegally unapandishwa kizimbani then kwenye pipa, hadi kwenu. Lakini Tz, umesoma kile kisa cha Mwarabu wa Movenpick? Yupo illegally na wafanyikazi wazalendo wamelalamika lakini jamaa kapitisha mshiko polisi wanabaki wanawapigia simu wazalendo wafute malalamiko yao. That is Bongo and that is wrong.
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,489
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kama unataka kuanzisha mada ya Watanzania wanaoishi nje illegally, fanya hivyo. Hapa tunazungumzia wahamiaji haramu wanavyozidi kuongezeka Bongo. The two may be related lakini kuiingiza hapa ni kupotosha lengo.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Wewe kama unataka kubisha bisha, mimi nakwambia ninayoyajua siyo kila Mtanzania aliye majuu anataabika kupata makaratasi. Na wengi ninaowafahamu mimi wala hawakujilipua kama unavyodhania. Kama mtu madarasa yake yamepanda na una ajira ya maana basi inakuwa rahisi ukilinganisha na yule ambaye asiye na madarasa mengi.

  Ninaowafahamu mimi wengi wamefuata njia halali za kuomba makaratasi kama Watanzania bila kujilipua au kutangaza Utaifa wasiokuwa nao. Miaka hiyo ya nyuma ajira zilikuwa belele na hao Wabongo wengi fani walizosomea zilikuwa zinatakiwa sana na waajiri wengi.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...