Jamani mbona vitu vimepanda ghafla

Karibu mara zote uchumi unavyoenda, mzunguko wa fedha ukiongezeka bei huongezeka..

Mapacha hawa wawili kwa kawaida wana uhusiano huu.

Higher unemployment equals higher money supply, higher money supply equals infation.

Higher printing of money equals higher money supply, highwr money supply equals inflation.

The opposite is also true.

Hii ni kwa kufuata kanuni za kiuchumi za kawaida, kwamba, price point is where the curve of supply meets the curve of demand. If money supply increases, this naturally increases demand and the price point.

Na mpaka miezi michache iliyopita, moja ya point za kujivunia za serikali ya Magufuli ilikuwa kudhibiti mfumuko wa fedha. Mimi nilitaka kupinga umakini wa point ile, lakini sikuwa na data rasmi.

Sasa baada ya kuona uzi huu, naona Magufuli ameweza kufanya jambo la ajabu linalokiuka kanuni za kawaida za kiuchumi. Kama ulitaka kumpigia makofi, subiri kwanza, hili si jambo la kujivunia. Ni jambo baya.

Magufuli ameweza kupunguza mzunguko wa fedha, na hapo hapo, inavyoonekana, nafikiri kwa kutumia kodi, kuongeza mfumuko wa bei.

Ameweza kupunguza mzunguko wa fedha kwa kuingilia mzunguko wa kawaida wa fedha. Sababu moja ni kuondoa hela za serikali katika mabenki ya biashara kwa mkupuo kinyume na ushauri wa wataalam kama Lawrence Mafuru (Mafuru alimshauri Magufuli asiingilie mzunguko wa fedha kiholela, akaondolewa kazini, matokeo yake tunayaona).

Kwa hiyo hapo amepunguza mzunguko wa fedha. Kawaida mipango hii, ikifanywa kwa umakini, hupunguza mfumuko wa bei.

Lakini kwa sababu serikali ya Magufuli imekosa umakini, jitihada za kupunguza mzunguko wa fedha zinashindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kwa sababu serikali inaondoa effect ya mzunguko wa kodi kupunguza inflation, kwa sababu serikali ina utitiri wa kodi zinazorudisha bei juu na hata kuipandisha zaidi ya ilipokuwa awali.

Kwa hiyo mwananchi anapigwa mara mbili.

Kwanza mzunguko wa kodi umeanguka. Nafikiri kwa lugha ya kitaalamu wanasema "vyuma vimebana". Watu wamepigwa hapo.

Ukitaka kuangalia kile kinachoitwa "silver lining" from this dark cloud, kusema kwamba, mzunguko wa fedha kusinyaa kutatupa ahueni kwa kupunguza bei, unapigwa mara ya pili. Kodi kubwa zinafanya bei zisipungue, na mara nyingine bei kupanda.

Kama unaamini sana kanuni ya "invisible hand" kama alivyoisema Adam Smith, utasema kwamba kama watu hawana hela bei zitashuka zenyewe. Maana wauzaji, on a large scale, hawawezi kuuza vitu kwa watu wasio na hela. Tatizo wauzaji hawawezi kuuza below a certain profit price point, definitely not below a breaking even point, bei ya kurudisha gharama zao tu. Kwa lugha ya mtaani tunasema, muuzaji hawezi kufanya biashara kichaa ya kuuza kitu kwa bei ndogo kuliko gharama alizoingia kununua na mpaka kufikia kuuza.

Mzunguko mdogo wa fedha ukiendana na kodi kubwa kama nilivyoeleza hapo juu, utasababisha watu watake kufanya biashara kwa magendo.

Mwanauchumi Arthur Laffer aliandika kwamba, katika suala la kutoza kodi, kuna curve inayooanza kwa kupanda juu, halafu inafikia point au plateau juu, halafu inashuka chini. Hii curve ni ya uhusiano wa kiwango cha kodi inayokusanywa na serikali na ulipaji wa kodi.

Mwanzo kwenye kodi ndogo sana, watu karibu wote watalipa kodi. Watu wengi hawataki kushikwa kwa kutolipa kodi kama kodi ni ndogo sana. Lakini kutoza kodi ndogo sana hakuipi mapato makubwa serikali.

Kadiri serikali inavyoongeza viwango vya kodi, ndivyo watu wengi zaidi wanavyotafuta njia za kufanya biashara bila kulipa kodi. Mpaka point ya juu kabisa ambapo tunaona "point of diminishing returns" ambapo kila serikali inapozidisha kodi, ndivyo mapato yanavyozidi kupungua.

Arthur Laffer alionesha kwamba serikali inayopenda kuongeza kodi tu, inaweza kujipunguzia mapato yenyewe. Kwamba, serikali inaweza kukusanya kodi zaidi kwa kupunguza kodi chini ya "point of diminishing returns" na kuongeza kodi zaidi ya hii point hakusaidii kuongeza mapato yanayotokana na kodi.

Kwa kifupi, hata kama unataka kutetea serikali ya Magufuli kubana mfumuko wa bei, kwa kusema jambo hili linadhibiti mfumuko wa fedha, point hii inakuwa haina maana, kwa sababu kodi kubwa na nyingi zinazoletwa na serikali hii, zinafumua bei upya iwe juu.
Huyu Arthur Lucifer ameongea ukweli
 
Huyu Arthur Lucifer ameongea ukweli
Hii hapa sample curve, kwa wale ambao wanaweza kuelewa visuals zaidi kuliko maneno.

laffercurvegraph.png
 
Mbona ccm walituambia budget ya mwaka huu imekuja kumkomboa mnyonge.
Ila kinachonishangaza ni kuwa tangu 2005 kila budget nasikia imekuja kumkomboa mnyonge, namshangaa huyo mnyonge sijui ni kwanini hataki kukomboleka

Unyonge ni mtaji wa wanasiasa mkuu,hawana cha kuombea kura zaidi ya hilo
 
Wewe utakuwa mpiga dili.. Ukiwa unapiga kazi kwa bidii mambo yatakuwa murua tu..kwasasa mnajengewa msingi ili mje muishi vizuri..majizi na wauza unga ndio wanaolalamika awamu hii..
Wachimba Makaburi na watu wa Mochwari hamuwezi kulalamika huu ni wakati wenu
 
Duh! Kila mwaka serikali inapotangaza bajet zake mfumuko wa Bei unaibuka. Hivi mm nashangaa Sana Hawa wafanyabiasha kwani hawaoni Kuwa mishahara haijapanda.?
 
Hao kuku sio wa kienyeji tena, hao kuku wa geti kali.
Ili aitwe wa kienyeji lazima akazurule ajitafutie riziki yake mwenyewe, wewe jukumu lako kumpatia malazi tuu
Mfuko wa 50kgs chakula cha kuku umepanda toka 40,000/- hadi 45,000/-.Halafu kuku wangu wa kienyeji nimewazoesha kuwapa chakula hawajui kudanga !
 
Mimi mvutaji wa sigara nilikua nanunua paketi ya SM 2600 ika jana nimenunua 3400. Yaani imepanda shilingi 800. MATAGA
Kwa wewe naomba iuzwe hata elfu hamsini. Tunakupenda ndugu yetu na hatutaki utumie mabidhaa yanayodhuru afya yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom