Jamani mbona rais wangu hakuongelea suala la Dowans? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani mbona rais wangu hakuongelea suala la Dowans?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngwendu, Jan 1, 2011.

 1. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jana nimeisikiliza kwa umakini hutuba ya rais wa JMT nikiwa na matarajio makubwa ya vitu viwili ambavyo vinagusa hisia za waTanzania wengi kwa sasa, nayo ni
  1. Katiba mpya
  2. Dowans
  Suala la katiba amenifurahisha. Pia siku zote huwa sina wasiwasi na kikwete kwa vitu vinavyogusa jamii kuvitolea maamuzi ambayo wengi huwa wanakubaliana nayo, mfano lilipoibuka suala la ununuaji wa mitambo chakavu ya dowans. Lakini pia ninachokiona ni kuwa hana cha kupoteza kwenye urais wake hasa kwa suala hili la katiba kwa kipindi hiki cha mwisho kwake.
  Suala la dowans hakuliongelea kabisa japokuwa ameongelea crisis ya umeme.
  kwani hii kwangu ni mara ya kwanza kwa rais JK kutoongelea suala linalogusa nyoyo za wengi katika sehemu husika na muda husika.
  Wakuu kama kuna mtu anahabari za ndani atujuze, ni kitu gani kilichojiri.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  shareholder
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  king hujaelewa swali langu, mbona liko wazi?
  Jamani mtu yeyote mwenye datail ya kilichojiri kwa hili la dowans kwani wengi tulikuwa tumekaa mkao wakusikia tamko la mkuu. plz.
   
 4. Licence to Kill

  Licence to Kill Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ulikuwa huna kazi ya kufanya au ulikuwa umepigika kiasi hata ngawila za kwenda kwenye social enjoeyment ikakupiga chenga, hivi ni nani mwenye akili timamu akae kwenye runinga kutegemea kwamba mkwere atakuja na jambo jipya au la maana? kama unaishi Dar karibu hapa Club san siro tugawane umaskini maana inaonekana huyu Mkwere amewabana vilivyo.
   
 5. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hajaliongela maana anaona aibu, haya na soni kulipa mabilioni kwa uzembe wa serikali yake na mashirika yake...
   
 6. Nyodo1

  Nyodo1 Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwandishi wa speech alisahau kuiweka, na JK wall hakuipitia kabda ya kusoma. Hakuwa muda ndiyo karudi kutoka safari. Huyu jamaa ni mtupu sana
   
Loading...