Jamani maskini kigoma

Nilisema umeme ni issue na generator Kigoma zinachukua chati? sasa wafanya biashara mnaouza generators kwa nini msipeleke kule? market iko wazi wajameni

Generator.jpg

Generator-1.jpg
 
Sehemu hii panaitwa Mlole. Hapa pamejengwa vizuri na barabara zake ni safi ingawa ni tope kama kawaida. Hata nyumba unaona zimepangwa vizuri.

Kigoma Mlole.jpg

Na eneo hili ni Mwanga. Hapa ni karibu na mjini tu na tusema bado ni mjini tu.

Kigoma mwanga.jpg

Kigoma mwanga-1.jpg

Kigoma Mwanga-2.jpg
 
Mboga mboga na matunda kibao Kigoma. Hapa ni Kasulu vijijini ambako wajasiliamali hawa walikuwa wakinadi biashara zao:D

Mbogaboga.jpg



Mbogaboga-1.jpg

unaona nyanya hizo? si zinaweza kufaa kwa export au kuuzwa pale shoprite? lakini nani awasaidoe jamani?

Pamoja na utajiri wote huo angalia walivyokuwa na sura za kukata tamaa!
 
Mchukia Fisadi,

Sijui kama bado uko kigoma au umeshamaliza ziara yako. Kama bado uko kigoma tafadhali sana jaribu kutembelea na ujiji, kasulu na kibondo kama kasma itakuwa kikwazo twaweza kuwasiliana tuwezeshane angalau utujuze huko nako hali ikoje. Nategemea kutembelea Mkoa wa Lindi nitajaribu pia kupata mawili matatu ya huko na kuwajuza nako nadhani ni choka mbaya!!
 
Mchukia Fisadi,

Sijui kama bado uko kigoma au umeshamaliza ziara yako. Kama bado uko kigoma tafadhali sana jaribu kutembelea na ujiji, kasulu na kibondo kama kasma itakuwa kikwazo twaweza kuwasiliana tuwezeshane angalau utujuze huko nako hali ikoje. Nategemea kutembelea Mkoa wa Lindi nitajaribu pia kupata mawili matatu ya huko na kuwajuza nako nadhani ni choka mbaya!!

:D :D :);) Oh masikini nilishaondoka huko. Kwa sasa niko Tanzania. Kwa sababu ya shida ya umeme nisingeweza kukaa cafe na kutuma picha hizi maana gharama ingekuwa kubwa. :):eek:
 
Loooooooooo usiniambie ujiji, kule ni choka mbaya. Majumba nadhani aliyajenga sultani na mengine yanatisha. Lakini ajabu ni kwamba wao wameridhika kabisaaaaaa. Bao mtindo mmoja tangu asubuhi. Utawakuta wamekaa verandani tu.
Nilimtembelea rafiki mmoja na nilipoingia ndani nilikuta ukuta wa nyumba wa ndani umedondoka chini na wala hana taabu ya kuishi na kifusi cha udongo pale ndani. Ili mradi maisha yanakwenda.
 
Mchukia Fisadi asante sana kwa kutushirikisha ziara hii ya sehemu ya nchi yetu. Ni kweli haya ndiyo maendeleo tulioletewa na serikali yetu kwa miaka takribani 50 madarakani na ndio sababu bado wanataka wananchi wanenelee kuwa chagua!!
Je, hawa wanaoishi katika maisha magumu kiasi hiki waweza kufahamu neema ikoje sehemu nyingine au nchi nyingine? Nadhani mara nyingi inakuwa vigumu watu kuelewa haswa kwa kuwa wengi wamekuwa wakijifunza kwa picha.

Hapa tufanye je ili na walio kigoma na kwingineko waweze kuona neema zinazoonekana sehemu nyingine, ili wawe na uweza wa kuwahoji kina "Serugambo" na wenzie.

Nawakilisha!!
 
Hapo nyuma ya hiyo gari nyeupe katika eneo hili la Mwanga ndipo kuna ile URUSI YENYE NGUVU. Jukwaa la wana Kigoma kusemea shida na hoja zao kwa serikali. Kuna kila hoja kama mnavyofanya hapa jf;)

Urusi yenye nguvu.jpg

Angalia uchafu ulivyozagaa kila sehemu barabarani. Na hii ni hali ya kila siku.
 
:D :D :);) Oh masikini nilishaondoka huko. Kwa sasa niko Tanzania. Kwa sababu ya shida ya umeme nisingeweza kukaa cafe na kutuma picha hizi maana gharama ingekuwa kubwa. :):eek:

Asante sana kwa habari na picha. Hii kali sana, maana nilikuwa nikisikia Kigoma nilikuwa najua ni kama Arusha, Moshi,Morogoro etc! Hii habari isiishie hapa JF tu. Kuna haja ya kufichua mambo mengine yaliyojificha ambayo yana athiri Watanzania.
 
Hawa vijana nimekutana nao Kasulu walikuwa na nyuso za furaha kweli bila kujali wanaishije. Kwao maisha ndio haya. Angalia jinzi walivyo na neema ya maji ya kisima kilicho nyuma yao tu kikitililisha maji, lakini ni wachafu kweli kweli. mmmmmmmmmhhhhhhhhh hivi na hii inahitaji serikali ati????:(

Taifa la Kesho.jpg

Taifa la kesho-1.jpg

Na hawa niliwakuta pale Kigoma mjini wakicheza katika mchanga bila kujali uchafu uliozagaa kila mahali. Ni hatari kwa maisha yao lakini wacha wa enjoy kwani sisi baba na mama zao tumemua kuitelekeza nchi yao ya baadaye.



Taifa la kesho-3.jpg

Taifa la kesho-2.jpg

Na hawa wanatoka shule kwa furaha. Ni maeneo ya Kibondo huko:rolleyes:

Twatoka shule.jpg

Twatoka shule-1.jpg
 
Mchukia fisadi kwa kweli nilikuwahi kule mwanzoni bila kuwa na subira kumbe picha ulikuwa nazo...thanks very much matumizi mazuri ya camera na utunzi mzuri wa habari.

Ningekuwa na ujanja wa kuweza kuweka picha kama wewe nafikiri ingekuwa raha sana...mpaka sasa siwezi weka picha kama...kuna maeneo natembelea ningeweza kuweka picha hapa tukawa tunafahamisha sehemu mbali mbali za nchi yetu..

Thanks Mchukia fisadi.
 
Buswelu,
Asante.
Nilikwambia nina picha kwenye memory card ya 4Gb sijui kama ninaweza kuziweka zote hapa maana hata kuzitayarisha ili nizi upload kirahisi ina consume muda kwa kweli. Lakini naweka kila nitakachoweza. Nashukuru pia kwamba umejionea mwenye, na wana wa Kigoma walio jf hapa mimi kama nasema uongo wawe wa kwanza kukanusha. Nimejitahidi nisionekane pro politician lakini niweke realities. Na najua hapa hata wa sisiemu watanyamaza hawatasema sana mbali na kujidai wanamshambulia Zitto. Hapa msalaba si wa Zitto ni Government ya sisiemu.
 
Ningekuwa na ujanja wa kuweza kuweka picha kama wewe nafikiri ingekuwa raha sana...mpaka sasa siwezi weka picha kama...kuna maeneo natembelea ningeweza kuweka picha hapa tukawa tunafahamisha sehemu mbali mbali za nchi yetu..

Thanks Mchukia fisadi.
Ni rahisi tu. Kama ukiwanazo na unataka kuziweka, ni PM nitakufundisha jinsi ya kufanya. JF ni kisima cha kuelimishana ndugu yangu.
 
Kwa nishati kwa sababu hali ya misitu si mbaya nishati inapatikana bila taabu. Hakuna deforestration huko na hali ya mazingira si mbaya ingawa kwa sababu ya wakimbizi misitu iliathirika kidogo. Kutoka katika gari unaweza kuona miti imekatwa au imechomwa ovyo ovyo lakini si kwa hali ya kutisha. Angalia jinsi gunia la mkaa lilivyoshonwa tena huko Kibondo/Kasulu. Nadhani ukileta Dar mkaa kiasi hivi unatajirika. Maana si gunia moja hilo bali ni mawili katika moja. Wenyewe Dar mnaita Lumbesa;):D

Mkaa.jpg
 
Mchukia fisadi asante sana kwa picha ila atleast kuna maendeleo kidogo nilikuwa kigoma mwaka 2005 pale kwenye makumbusho ya livingstone hakukuwa na nyumba nzuri namna hii!kulikuwa na kijumba kibaya baya tu!nakumbuka kulikuwa na babu anaelezea historia ya hapo yaani kakariri maneno maana aliongea maneno yale yale nilivyokuwa huko 2004!endelea kutuwekea maphotos ina maana Gungu hukufika?mbona sijaona picha
 
Kipanga bahati mbaya mi si mzee maana nimemaliza darasa la saba 2009 kwenye ile shule ya medium school kwa hiyo mimi ni........?:D
...Teh!teh! tehhhhhhhh!!!! Haya bana nadhani huo mwaka hata hiyo shule uliyosoma itakuwa haijaanzishwa.....
 
Na hizi ni pamoja na nyumba za wakazi wa Kibondo. Usishangae hizi ni nyumba za kisasa kabisa. Tena hawa wana maisha bora hujawahi hatakuona. Nyumba zingine zina vyoo, zingine hazina kabisa sijui wanasubiri usiku wa giza ili wakamalize haja zao huko? Hii niliitathimini nikiwa ndani ya gari. Kila nyumba niliyoipita nilikuwa najaribu ku asses kama ina choo pia; maana hii ni ofisi ya lazima kuwapo katika kila nyumba kama ilivyo lazima nchi kuwa na ikulu.
Walio navyo, nakwambia vyoo vinafanana vibanda vya kuku unaweza kujiuliza je mtu akiingia humo anaingia vipi? Wima au kwa staili ya mnyooko?
:D.

Nyumba zetu.jpg

Nyumba zetu -1.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom