Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Nilikuwa Kigoma siku si nyingi na kwa kweli nilishangaa sana kuona jinsi mkoa huo ulivyo nyuma sana kimaendeleo kulinganisha na mikoa mingine.
Kigoma ni mji ulio kando ya ziwa maarufu lenye kina kirefu kuliko maziwa yote duniani linaitwa ziwa Tanganyika.
Kigoma ni mkoa ulio maarufu sana kwa uvuvi wa samaki watamu kuliko samaki wengi niliowahi kula. Hasa dagaa wao ambao huwezi kuwakinai na hata ile migebuka nakwambia huwezi kuiacha mezani hata kama umeshiba.
Kigoma ni eneo maarufu kwa uzalishaji wa mawese na hivyo uzalisha mafuta ya mawese na utengeneza sabuni safi sana kutokana na zao hilo la mawese. (sijui kama TBS wameshawapa kiwango)
Kigoma inazalisha chumvi nyingi sana nadhani kuliko hata mikoa ya pwani inayozalisha chumvi.
Kigoma ni mkoa unaopakana na nchi za Congo na Burundi na kuwa na access nzuri ya ku supply needs za nchi hizo ambazo ni land locked.
Kigoma ni mkoa wenye rutuba na unaonekana kuzalisha mazao mengi sana kuliko maeneo mengi niliowahi kutembelea. Nimeona wakizalisha mboga mboga tena kubwa kubwa. Kwa mfano Nyanya, vitunguu n.k vya Kigoma ni vikubwa kubwa.
Kigoma wana opportunity za utalii kwa kuwa na misitu yenye wanyama ambao wanapatikana huko tu duniani kama wale sokwe weusi.
Kigoma ndio mkoa pekee ambako saa 1 usiku bado ni mchana kweupe kabisa na saa 1 asubuhi bado ni usiku wa giza tororo. L/O/L.
Kigoma jamani, Kigoma niseme nini zaidi?
Lakini nenda Kigoma ujionee jinsi walivyosahauliwa. Barabara choka kabisa.
Hakuna umeme wa uhakika kabisa!!!!!!!! wanaishi kwa umeme wa mgao kama vile kwamba hawako katika nchi hii. Maana kulipokuwa na shida ya umeme kwa ajili ya ukame katika nchi hii miaka michache iliyopita hata kuleta karaha za Richmonduli, nchi yote ilijua kuwa nchi iko kwenye janga. Magazeti na tv na radio zilitangaza asubuhi na jioni. Nakumbuka mpaka JK aliweka mkakati wa kuhakikisha tunapata umeme wa ghali kabisa toka kwa washirika wao. Lakini leo Kigoma umeme ni mgao kila siku na hakuna wala anayepiga kelele maana kule hakuna watanzania na kama wapo hata kama wataishi kwa shida ya kutokua na umeme hakuna noma, wacha wataabike tu.
Kigoma iko karibu kabisa na ziwa. Inaelekea kwamba kazi ya maji ya ziwa lile ni kuvua na kusafiria tuuuuuuuuuu.
Mji wa Kigoma kwa mfano hauna maji ya uhakika na salama. Kwa muda wa wiki mbili niliona maji yaki flow katika bomba siku mbili tu. Hii ni ajabu sana. Nilitembelea katika eneo fulani la mji huo nikakuta watu wakiwa wamechimba mashimo mengi marefu katika viwanja vyao katika harakati za kutafuta maji ya kutumia.
Nilibaki nikijiuliza maswali mengi sana kama kweli huo mji uko karibu na ziwa au la?. Hivi inakuwaje mtu ajaze mashimo marefu katika kiwanja chake katika harakati za kutafuta maji? kwanza niliona hata usalama wa watoto wao uko hatarini.
Kigoma mjini niliona barabara moja ya lami ambayo inaanzia ujiji na kuishia stesheni ya reli na niliambiwa na wenyeji kwamba kabla ya hapo ilikuwa inaanzia eneo linaitwa Mwanga hadi stesheni ila ni hivi karibuni imeongezwa kutokea pale Mwanga hadi ujiji. Na sasa kuna nyingine inajengwa kuelekea eneo waliniambia linaitwa Kibirizi imeshajengwa kama km 2 hivi. Na pia kutokea pale Mwanga kuna nyingine imeshajengwa kama km 5 hivi kwenda kwa wakina Zito panaitwa Mwandiga.
Lakini, ukifika pale Kigoma utaona ni kama mji una barabara moja ya lami tena ya kiwango cha chini kabisa. Hiyo inayoanzia Ujiji hadi Stesheni.
Usafiri wa kutegemewa kwenda bara ni Treni peke yake. Lakini tiketi ni mpaka ujuane na watu wa railway. Bila treni utahitaji usafiri wa kuzunguka sana maana utapitia Kahama na kati ya Kigoma mjini hadi Kasuru hadi Kibondo hadi Nyakanazi barabara ni mbovu sana na gharama yake ni kali sana ndugu zanguni. Kwa sababu hiyo wao wanajua watasafiri kwa treni tu. Hii kwao ni nafuu sana. Kuhusu muda na siku za kusafiri wao hawana uchaguzi.
Hakuna mji ulio mchafu kama mji wa Kigoma katika nchi hii. Ni mji uliojaa takataka kila kona na huwezi kuamini kwamba kuna mamlaka ya mji ( Halmashauri ya mji au manispaa ya mji) maana uchafu, uchafu, uchafu kila mahali. Na mbaya zaidi wanyama wa kufugwa kama mbuzi kondoo nguruwe wanazunguka kufaidi uchafu huo barabarani kila mahali. Ukiwa unatembea kwenye street zao unapishana nao kama kawaida. Na sijui kama street zao zinaweza kufahamika kwa majina maana nyingine ni mitaro tu na kumbe hiyo mitaro ni street.
Kigoma ni mji una magari mengi sana kwa sasa lakini kwa sasa barabara yao hiyo moja inaonekana kuwa finyu na uwezekano wa kupata ajali ni rahisi pia.
Nilifurahishwa na jinsi walivyo organise public transportation.
Kuna daladala zilizopangiliwa vizuri na zimeandikwa vizuri kila inakokwenda. Utadhani uko Dar vile. Ukitaka kusafiri kwa daladala pale Kiogma kwa kweli mambo ni poa kweli.
Lakini nilishangaa kwamba Kigoma hakuna Stand ya mabasi ya abiria. Maana wanapoita Stand ni aibu tupu hapafai kuitwa jina hili maana ni kwenye kakona fulani tu. Sijaelewa mpaka leo kwa nini wamepaita mahali pale stand ya mabasi.
Kigoma ni mahali pa ajabu. Nilikuwa nikiishi hotel lakini nilikelwa sana na kelele za mihadhala kati ya wakristo na waislamu ambazo nadhani zilikuwa zikitoka katika radio ya msikiti wa Mwanga usiku kucha. Nilibaki najiuliza hivi hawa wananchi wa Mwanga wanapataje usingizi katika karaha kama hizi? Je hii mihadhara inawezaje kuruhusiwa na serikali? Je kila dhehebu likifanya hivyo nini kitatokea?
kabla sijapata jibu nikakutana na ukumbi kama Jamii forum unaitwa URUSI YENYE NGUVU. Hapa nikagundua wapo wakeleketwa wa chama fulani na wameweka ubao. Kila siku kuna malalamiko ya wananchi kuhusu mustakabali wao na mstakabali wa nchi yao. Siku moja nikakuta wametoa ujumbe kwa Nape na siku nyingine nikakuta wametoa ujumbe kwa Takukuru na siku nyingine kwa serikali yao kuhusu shida ya maji na kila mara utakuta wameweka ujumbe huu na ule. Ajabu ni kwamba yote wanayoandika wanayaandika kwa kirefu na ni ujumbe rahisi kuelewa nini wanasema.
Nisichojua ni kama kweli walengwa wa ujumbe huo wanausoma au wanapofusha macho wasiuone. Naona wana Kigoma wameamua wajisemee wenyewe kwa serikali kupitia njia hii maana nadhani wamegundua kuwa na wabunge hakuwasaidii lolote. Walijaribu Chadema wakaishia kukutana na mbunge tapeli ambaye moyo wake wote ulijaa tamaa na si kuwatumikia wananchi maana hakukuwa na tofauti. Sasa wamejaribu sisiemu hapa ndio kabisaaaaaaaaa!!!! Mmoja aliniambia siku raisi wa nchi akienda wataenda kumpokea wakiwa na vibatari na vifaa vya kuchotea maji. Hakuna tofauti yoyote katika vyama kuleta maendeleo Kigoma mjini. Na sasa kama maendeleo mjini hakuna ebu nambie vijijini!
Nilifurahi nilipotembelea makumbusho ya Livingstone kule ujiji maana huko nakwambia niliona panajengwa jengo la kisasa sana la makumbusho ili kuondoa aibu ya kijijengo kilichokuwepo kabla.
Inahitaji siku nzima kuieleza Kigoma. Lakini jamani Kigoma ni kama mkoa yatima katika nchi hii. Utadhani hauko katika serikali hii ya Tanganyika.
Habari ndio hiyo.
View attachment 2581