Jamani Maisha ni Magumu sana Ulaya, Watu Wanateseka - Mwana FA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani Maisha ni Magumu sana Ulaya, Watu Wanateseka - Mwana FA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Jul 18, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Jul 18, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msanii maarufu wa Bongo Flava Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ambaye alienda nchini Uingereza kusoma amerudi Tanzania na kusema maisha ya ulaya ni magumu sana na watu wanateseka sana. Mwana FA hawashauri watu waache kazi zao Bongo kukimbilia ulaya.

  [​IMG]

  Siku chache baada ya kudondoka kutoka pande za Uingereza anakopiga kitabu, mkali wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA amesema na ShowBiz amejionea kwa macho yake baadhi ya watu wanaoishi huko wakitaabika bila kuwa na ishu ya kufanya.

  Msanii huyo alisema kwamba, baadhi ya vijana wengi bado wana ndoto za kwenda Ulaya wakidhani kwamba maisha ni rahisi kitu ambacho siyo cha kweli kwakuwa huko pia wapo watu wengi wasiokuwa na ajira wanasota mitaani.

  “Ulaya maisha magumu washkaji, mtu kama una dili yako ya kupata miambili miambili Bongo bora utulie uendelee kuongeza kipato na kuijenga nchi yako badala ya kukimbilia Ulaya.

  Ninachoongea watu wanaweza wasiniamini lakini anayeweza aende akajionee mwenyewe,” alisema FA ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake mpya, ‘Nazeeka sasa’ iliyowashirikisha Prof. Jay na Sugu.

  Akiizungumzia picha ya Rais Kikwete iliyopo katika baadhi ya tisheti zake (kama anavyoonekana pichani), Hamisi alisema kwamba, hivi sasa ameamua kuachana na ujinga wa kuvaa nguo zenye picha za mastaa wa Ulaya wakati yeye ni Mbongo. “Yaani mimi namfagilia sana JK kuliko Rais yeyote duniani kwa kuwa ni mzalendo wa kweli. Kwangu mimi Kikwete wa kwanza halafu anafuata Obama,” alisema FA.

  Aidha, mchizi aliiambia safu kuwa, mwishoni mwa mwezi huu atarudi Uingereza kwa ajili ya kumalizia masomo yake ambapo anatarajia kukusanya mafaili yake na kurudi Bongo Desemba mwaka huu akiwa na Masters yake.

  ........utaona na kusoma unachokipenda..........
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG]
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  asituzuge life majuu zuuri bana.......mbona watu tunaona mapicha wa majuu wanakula happy si kitoto.....nyani ngabu kila siku anakutana na Monica gym huoni anafaidi akirudi bongo atakutana na shoriz wenye vitambi wakinywa safari beer bar....
   
 4. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Nadhani Mwana FA hakuongea yote kuhusu maisha ya ulaya sababu ya limitation ya muda wa kipindi. Ngoja nijaribu kujazia.


  1. Ukweli ni kuwa hakuna sehemu amabo maisha ni rahisi. Kila sehemu tanzania,kenya, darisalama,katelelo, london , coventry , nk masiha ni magumu hasa.
  2. Nchi zetu za kiafrika siasa ndio ajira inayolipa zaidi.upenyo wa kuibuka, kujipatia riziki kihali ni mdogo sana. Vijana wa ulaya wana uwezo wa kijipatia vijisenti kwa kwa ajira za box toka akiwa na umri wa miaka kama 17 hivi.
  3. Ukiwa na vigezo vya kusihi huko ulaya maisha vita ya maisha ulaya inaweza iswe ngumu kama vita ya maisha bongo.
  4. Maisha ulaya sio magummu kivile ndio maana sio lazima uwe na Master au degree kupata ajira. kwa elimu ya Veta , ufundi, udereva unaweza kushi maisha ya kawaida kihalali.Nchi zatu za kiafrika sababu ya ufiyu wa ajira unabidi tusome sana.kwa wastani mtu unaanza kujitegema na kupta ajira ukiw labda una miaka 23.
  5. Mwisho ingawa maisha ni magumu kila sehemu wenzetu wametuzidi kuweka mifumo bora ya mambo kama elimu, afya, sheria,mindombinu. maamuzi ya mambo mengi yanafanyw akwa kufuata ushauri wa kitaalamu na sio ushauri wa kisiasa kama tanzania.
  Na mimi show biz time yangu kupitia jamii forum imeisha. Maisha ni vita usikate wala kukatishwa tamaa
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ukiona maisha magumu zaidi rudi huku bongo,mapori ya babu zako yapo
   
 6. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Maisha ni magumu popote pale katika hii dunia, iwe Ulaya, USA au Africa. Muhimu ni kujishughulisha popote pale ulipo na usichague kazi. Mie nadhani huyo Mwana FA alijenga maghorofa mengi kabla hajafika ulaya, alijua ulaya ni pepo ndogo, kumbe nako inabidi ufanye kazi kwa nguvu ndipo upate fedha.
  Ila si haba hata kama maisha magumu ughaibuni ila wenzetu kwa miundo mbinu nawafagilia sana. Vile vile mtu kupata kazi huko ni juhudi zako sio mambo ya undugu kama bongo.
   
 7. B

  Babuji Senior Member

  #7
  Jul 18, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mhhhh
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Babuji mbona unaguna? vipi kisu kimegusa mfupa?
   
 9. Violet

  Violet Member

  #9
  Jul 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ulichokisema Mwana FA, watu wengi wanadhani maisha ni marahisi ulaya, usa nk. Tz hata ukiwa huna kazi, utaishi tuu, familia ipo, kwingine ukizubaa tuu ukakosa nyumba, inamaana huna adress, bila adress msaada kupata ni ngumu sana. Hata ma homeless wa TZ , huwezi linganisha na wa huko wanaolala nje kwenye -20
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Mwana FA anamagilia JK akirudi amvae amsaidie ajira jamani hilo shuti la mbali hamjui tu.....mtaona akirudi....
   
 11. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani YO YO amenichekesha mpaka nimelia,eti mabinti wa kibongo wanavitambi vya safari,teh teh teh teh teh teh!!!!!!!
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kumuambia mtanzania arudi bongo tu simply bila kujua situation ya mtu siyo busara.

  Kuna watanzania ambao hawafanyi chochote ughaibuni na hata wakirudi Tanzania hawata lifanyia taifa chochote. They are losers Ulaya and they will be losers hata Bongo. Sorry for the harsh words. Lakini sioni maana ya kun'gang'ania mtu ambae hafanyi chochote Ulaya arudi Tanzania mkitegemea atafanya chochote.

  Kuna wale ambao kuwa ughaibuni kuna faidi kwa familia zao na wanaweza kuwa faida kwa familia pia. Imagine mtu kama Hashim Thabeet ambae familia yake Tanzania walikua masikini na Mungu kamjalia na sasa ana tegemea kutengeneza pesa nzuri NBA. Why should he come back? Asi ifikirie familia yake? He is expected to make $3 million per year. Who makes that much in Tanzania at such a young age tena bila ufisad?. He, his family & Tanzania can benafit from him akiwa ughaibuni.

  Kuna watanzania wana fanya mambo makubwa tu kwa Tanzania kuliko watanzania waliopo nyumbani. Je mna fahamu mtu kama Mwanakijiji hayupo Tanzania? Can you tell me ni watanzania wangapi waliopo nyumbani who are doing what he is doing? Je Tanzania hainufaiki na Mtanzania kama Mwanakijiji anayeishi ughaibuni?

  Tanzania ni nchi maskini na ni kweli it needs it's people in order to move forward. Lakini pia kuna nchi kama India na China ambazo zipo mbele yetu sisi na ina raia wengi tu nje ya nchi. What we need is people who help Tanzania wherever they are. For all those who can stay in Tanzania & help for within I think that's what's best for the country but I also believe that if we all played our part Tanzania itaendelea tu. Kuna wabongo kibao tu nyumbani but they are not doing anything for Tanzania or Tanzanians. Mimi personally I prefer being back home because that's where I believe I can best serve my country. My place is in Tanzania. But I also believe we have many brothers and sisters around the world who can best serve as wherever they are.

  Mimi naona kikubwa ni kua na taifa la wachapakazi. Kwa sababu moja ya tofauti kubwa kati ya nchi zilizo endelea na ambazo hazija endelea ni working hours za work force zao. Mimi naona kama wewe ni Mtanzania unaeishi nje na you are doing something of use bora wewe kuliko anayeishi nyumbani na hafanyi chochote cha maana. Na pia kama wewe ni mbongo unayeishi nje & you can bring nothing to the nation hata ukirudi there is no lose hata ukibaki nje.

  Mkitaka kuona umuhimu wa kuwa na Watanzania wazalendo ndani na nje ya nchi look no farther than JF itself!

  Kila mmoja kwa nafasi zetu na kwa vipaji vyetu tuki litumikia taifa we will some day get there. As the late JFK put it, "Ask not what your country can do for your but what you can do for your country."
   
 13. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Maisha sehemu yoyote yanaweza kuwa magumu au rahisi. Jambo la msingi ni jitihada yako katika kuyakabili maisha hayo.
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  MwanaFA anajikomba kwa JK eti anamfagilia JK kuliko Obama is this true? Huku tunajiita kujikomba ili akirudi apate ka ajira kakubebwa yeye anafikiri JK hamfagilii Obama!Thubutu.
   
 15. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyu jama ni mwanamuziki na sio mwanamapinduzi wa mawazo, nani alimwambia kuwa kuna sehemu maisha ni marahisi, no way!! maisha ni magumu popote pale, hata Bongo maisha ni magumu. Halafu Violet namshangaa sana lini ukawa huna kazi halafu ukaendelea kula vizuri Bongo na nani amekudanganya kwa hilo, au nyie ndo wale wale hata kama una DIV0 mjomba atakupa kazi, ebu achane hizo. Bongo miundombinu sifuri, kupazta kazi hata kama una masters ishu???? sasa sijui mwanaFA na masters yake atafanya kazi wapi, kaka usidanganyike eti kwa sababu unamfagilia Kikwete basi mlango uko wazi kwa ajira, hell no, kaka lazima ustruggle vya kutosha lasivo utabaki kuimba mashairi tu.


  Rom
   
 16. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Inategemea uko majuu ya wapi. Sehemu zingine hawakuruhusu ukose mahali pa kukaa, chakula, elimu na matibabu utapatiwa tu kama ikidhihirika kwamba umekosa kabisa kazi.
   
 17. Amosam

  Amosam Senior Member

  #17
  Jul 18, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako wewe mbishi hata jina lako unalipinga!Huyo jamaa Mwana FA ni msanii na ni ajira tosha kwake,kwenda zake kuongeza masomo ni njia ya kuboresha hiyo ajira yake ya muziki,sasa we unang'ang'ania eti anajikomba kwa JK,wewe unataka ajikombe kwanani?Acha hizo umekua sasa ndugu.
   
 18. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ulaya huwezi kuijua kwa kukaa miezi mitatu-minne.
  inategemea umeenda kwa category ipi? mfano mtu kamaliza medicine muhimbili akienda UK atakuwa milionea.tumewaona wahindi.
  labda yeye alitegemea atapata pesa zakujilipia ada kwa kukaa miezi mitatu.huwezi kutoa tadhimini ya ulaya kwa miezi mitatu
   
 19. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  I agree, it takes sometime kujua maisha halisi ya mahali hasa ulaya na sio miezi miwili mitatu then unarudi bongo kisha unarudi tena unakaa miezi miwili mitatu,kuna vitu unaweza kufaham kwa muda mfupi kama huo lakini sio kiasi cha ku draw conclusion, japokuwa kuna watu wanasota kweli lakini kuna watu pia wanaingiza kiasi cha kutosha tu ni jitihada za mtu mwenyewe pale mahali alipo haijalishi ni bongo ama ulaya.
   
 20. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  I hope hauja nichanganya mimi na Mwana FA mwanamuziki. We share the same name but we are different people.

  Ni kweli huwezi kujua ulaya kwa kukaa miezi michache. Wala mimi sijaongelea based on kukaa miezi michache. Unless you have confused me na Mwana FA mwanamuziki I don't know why you quoted me and used speech directed to me
  .
   
Loading...