Elections 2010 Jamani Lyatonga Mrema kapatwa na ugonjwa gani?

A L Mrema ni mwansiasa pekee aliethubutu kuitosa CCM wakati bado akiwa na waazifa wa waziri hakuna mwanasiasa aliejaribu kuacha utamu wa madaraka isipokuwa Lyatonga Mrema.

CHADEMA kupitia Zitto walililamika CUF kumsimamisha mgombea katika jimbo la Kigoma kaskazini lakini hawaoni dhambi kumsimaisha mgombea ubunge Vunjo mahali Mrema A L anapokubalika zaidi ya mgombea wao dhaifu na asiyekuwa na mvuto
 
siasa mchozo mchafu
Huyo huyo Lyatonga mlikuwa mnampenda akiwa waziri leo mnamponda hee acheni hizo kila mtu anatafuta kula
au hamfahamu siasa nayo ni aina ya ujasiria mali?
 
Heshima kwako Majasho,

Ni kweli CHADEMA wanakinyongo na Bwana Mrema tangu enzi akiwa NCCR mageuzi.Nakumbuka Mwenyekiti wa CHADEMA wakati huo Mzee E Mtei alikuwa akigombea ubunge mjini Arusha kwa tiketi ya CHADEMA alikuwepo pia Bwana Makongoro Nyerere alikuwa akigombea kwa tiketi ya NCCR Mageuzi.

Mzee Mtei alikuwaakifanya kampeni kwa muda mrefu mjini Arusha lakini Makongoro alikuwa akimsaidia kampeni za urais wa Bwana Mrema Tanzania nzima.Makongoro alifanya kampeni mjini Arusha kwa muda usiozidi siku tatu tu na akashinda.CHADEMA hawakumsimamisha mgombea urais walimuunga mkono Bwana Mrema.Bwana Mrema alipokuja Arusha aliwasimamisha Bwana Mtei na Makongoro Nyerere na kuwaachia mtihani wakazi wa Mji wa Arusha wamchague mgombea wanaemka.Mzee Mtei alisononeka sana kitendo cha Bwana Mrema kumsimamisha Makongoro Nyerere na yeye,alitaka asimamishwe pekee yake.Chuki za CHADEMA dhidi ya Bwana Mrema zikaanza hapo,kila analofanya Mrema ni baya,mbaya zaidi chuki hizo zimeendelezwa na mkwe wa Bwana Mtei ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA Bwana Freeman Mbowe na baadhi ya wanachama wa CHADEMA ambao wanataka kuufanya mtandao wa JF ni mali yao.Nimemsikia mwenyewe Mheshimiwa Zitto Kabwe akimsifia Muungwana mara kibao haikuwa nongwa,Mzee wa kujaza watu mapesa kamsifia Muungwana mara kibao hapakuwa na hoja zozote hapa jamvini za kuwatukana kina Zitto na Cheyo ??????.


Hey Kijana Mrema amekwisha habari alikuja na kwa kasi bila kuwa makini sasa habari zake zinapaswa kuwa historia kwenye siasa za Tanzania Chadema ni chama makini and kimekuwa kikijijenga taratibu mpaka leo kimefikia hali hii ya kuwanyima usingizi ccm hapo inabidi utoe heshima kubwa kwa CHADEMA, mfumu uliopo sasa hautoi ushindani sawa kwa vyama vya upinzani ndo maana uunaona ccm inatumia rasilimali za umma na viongozi wa umma kuhujumu upinzani lakini kama kungekuwa na katiba inayotoa uhuru na haki sawa ccm ingekuwa historia hivi sasa na uchaguzi wa mwaka huu bado ni kitendawili kikubwa na mbinu iliyobaki ni kutumia nguvu kubwa ya dola na pesa nyingi za kifisadi kujalibu kujipamba kwa mbwebwe zote lakini watanzania sio wote wanadanganywa kwa nguvu ya pesa. Tukirudi kwa issue ya mrema, anataka kupata huruma ya CCM baada ya papara zake zote kugonga mwamba hivyo akili ya mrema inamtuma kutafuta regitimcy ya CCM hivi sasa ili apate msaada kwani upinzani walikushwa msitukia siku nyingi, Sasa kama CCM wanajivunia kusifiwa na mwanasiasa aliyefilisika sera na nidhamu ya chama chake cha TLP basi CCM nao hawana tofauti na akili za mrema
 
siasa mchozo mchafu
Huyo huyo Lyatonga mlikuwa mnampenda akiwa waziri leo mnamponda hee acheni hizo kila mtu anatafuta kula
au hamfahamu siasa nayo ni aina ya ujasiria mali?


kumbe wenzetu wenye kujiita jina la silaha ya kuvua ziwani au baharini wanatafuta na wao kula
 
Huyu ktk viongozi wote wa siasa hapa nchini ndo **** wa mwisho sasa kama ccm wamefanya makubwa kwa nini asigombee vunjo kwa tiketi ya ccm, ckuwahi kumsikia akiongea point, hata pumba tu zimemshinda kuongea, anachoongea ni mvuke, anatafuta ktu cha kukumbukiwa maana naona amebakiza cku chache na kwa hiki kitendo amekosa sala zangu maana ni mnafiki
 
Back
Top Bottom