Jamani " lizzy" utaniua kwa barua yako tamu

Lizzy upo wapi siku hizi mama? Umenitenga na kunisusa! Tokea uje kunitembelea hutaki tena kunisalimia! Tafadhali popote ulipo nakutafuta, mpaka kwenye magazeti nimetangaza na sijapata jibu
 
Last edited by a moderator:
Lizzy upo wapi siku hizi mama? Umenitenga na kunisusa! Tokea uje kunitembelea hutaki tena kunisalimia! Tafadhali popote ulipo nakutafuta, mpaka kwenye magazeti nimetangaza na sijapata jibu
Hahahahaha. ..
Aisee kitambo sana.

Ta Kamugisha umenitafuta wapi ukanikosa bana?! Njoo UngaLTD utanikuta nimejaa zaidi ya maji baharini!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mpendwa Ta Kamugisha,

Dhumuni la barua hii ni kutaka kukupa jibu la ombi lako ulilonifikishia takiribani mwezi sasa.Ila kwanza naomba unijulie hali yako ili nipate amani na furaha moyoni kusikia u mzima wa afya.Binafsi si mgonjwa ila upweke unanitawala kwa kutoweza kukutia machoni kila uwapo mawazoni mwangu.

Tangu siku ya kwanza unanisalimia pale tulipokutana mara ya kwanza nilijikuta navutiwa nawe kwa ustaarabu uliouonyesha.Siwezi kusema nilikupenda ghafla maana ntakua nakudanganya na ninajidanganya pia.Lakini kadiri siku zinavyokimbia ndivyo moyo wangu hua unaongezeka mapigo pale nisikiapo kutoka kwako.Naomba nikwambie ukweli kwamba uliponitamkia mara ya kwamba wanipenda nilishangaa sana maana sikutegemea maneno yale ndani ya kipindi kifupi tu ulichopata kunifahamu.Taratibu nilianza kukuelewa na kuamini kwamba inawezekana maana mapenzi hayapangiliwi.

Baada ya kuchukua muda wangu kukusoma na kukufahamu nimeamua na ningependa kuwa wako mpenzi au hata mkeo huko mbeleni kama nia yako ni thabiti.Nakubali kwasababu nimegundua u mwanaume mzuri mwenye heshima kwa watu na pia mwenye kujiheshimu...mwenye mapenzi na mwenye kujali...mwenye sauti ya kuremba masikio yangu kama kinanda kinachopigwa kwa ujuzi na pia mwenye kujituma.Naahidi ntakua nawe bega kwa bega iwe kwa shida na raha...ntakupenda kwa moyo wangu wote bila kusahau kukuheshimu wewe na mawazo yako.

Natumai barua hii itakuacha mwenye furaha hata kama ilikukuta na huzuni.Naomba utabasamu kwaajili yangu japo sikuoni furaha yako ni yangu pia.Nakupenda sana ewe mfalme wa moyo wangu na ninatumai nitabaki kua malkia na mtawala pekee wa moyo wako.

Wako akupendae Lizzy!

PS
Asante sana kwa nauli ntajitahidi pindi nipatapo nafasi nije mjini kukuona.Natamani sana kuhisi joto lako na mikono yako ikinizunguka.Niyaone macho yako ukiniambia unanipenda pia kuninong‘oneza yaliyo moyoni mwako.ALAFU JIANDAE KULA CHAKULA KIZURI NTAKAPOKUJA...NDIZI UZIPENDAZO NTAKUJA NAZO MWENYEWE.
Kwaheri kwa sasa!

"Raha ya barua iwe tamu kama hii"

Daha hatari sana, kitu cha long time
 
Back
Top Bottom