Jamani " lizzy" utaniua kwa barua yako tamu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani " lizzy" utaniua kwa barua yako tamu.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Ta Kamugisha, Apr 14, 2012.

 1. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Mpendwa Ta Kamugisha,

  Dhumuni la barua hii ni kutaka kukupa jibu la ombi lako ulilonifikishia takiribani mwezi sasa.Ila kwanza naomba unijulie hali yako ili nipate amani na furaha moyoni kusikia u mzima wa afya.Binafsi si mgonjwa ila upweke unanitawala kwa kutoweza kukutia machoni kila uwapo mawazoni mwangu.

  Tangu siku ya kwanza unanisalimia pale tulipokutana mara ya kwanza nilijikuta navutiwa nawe kwa ustaarabu uliouonyesha.Siwezi kusema nilikupenda ghafla maana ntakua nakudanganya na ninajidanganya pia.Lakini kadiri siku zinavyokimbia ndivyo moyo wangu hua unaongezeka mapigo pale nisikiapo kutoka kwako.Naomba nikwambie ukweli kwamba uliponitamkia mara ya kwamba wanipenda nilishangaa sana maana sikutegemea maneno yale ndani ya kipindi kifupi tu ulichopata kunifahamu.Taratibu nilianza kukuelewa na kuamini kwamba inawezekana maana mapenzi hayapangiliwi.

  Baada ya kuchukua muda wangu kukusoma na kukufahamu nimeamua na ningependa kuwa wako mpenzi au hata mkeo huko mbeleni kama nia yako ni thabiti.Nakubali kwasababu nimegundua u mwanaume mzuri mwenye heshima kwa watu na pia mwenye kujiheshimu...mwenye mapenzi na mwenye kujali...mwenye sauti ya kuremba masikio yangu kama kinanda kinachopigwa kwa ujuzi na pia mwenye kujituma.Naahidi ntakua nawe bega kwa bega iwe kwa shida na raha...ntakupenda kwa moyo wangu wote bila kusahau kukuheshimu wewe na mawazo yako.

  Natumai barua hii itakuacha mwenye furaha hata kama ilikukuta na huzuni.Naomba utabasamu kwaajili yangu japo sikuoni furaha yako ni yangu pia.Nakupenda sana ewe mfalme wa moyo wangu na ninatumai nitabaki kua malkia na mtawala pekee wa moyo wako.

  Wako akupendae Lizzy!

  PS
  Asante sana kwa nauli ntajitahidi pindi nipatapo nafasi nije mjini kukuona.Natamani sana kuhisi joto lako na mikono yako ikinizunguka.Niyaone macho yako ukiniambia unanipenda pia kuninong‘oneza yaliyo moyoni mwako.ALAFU JIANDAE KULA CHAKULA KIZURI NTAKAPOKUJA...NDIZI UZIPENDAZO NTAKUJA NAZO MWENYEWE.
  Kwaheri kwa sasa!

  "Raha ya barua iwe tamu kama hii"
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Kama ni Lizzy mwingine kila lakheri mkuu ..

  Kama ni Lizzy aka Lizzy Luu aka mama mchungaji aka hunny bunny ......... nakuambia acha kujifagilia.
   
 3. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Wivu sasa, hautaki mwenzio nipendwe au?
   
 4. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Pendwa tu..
  Sina shida nawe kipendwa ..
   
 5. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Hapo nasukuru kama umelitambua, mtoto kazimi, kafa, kaoza kwa bepari la kihaya
   
 6. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Tupate burudani,tutarejea

  A Man Who Can't be Moved - The Script
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Hivi Miss Kaazi Kweli kweli siku hizi simuoni sana, sijui yuko wapi.
   
 8. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,071
  Likes Received: 421
  Trophy Points: 180
  Huyo binti ushamaliza kazi. hana ujanja kwako ta kamgisha. Hongera sana kwa kuibua kifaa.
   
 9. Michael Pima

  Michael Pima Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Haya maneno yamekaa kidumedume, Lizzy wa wapi huyo?
   
 10. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Sasa pale atakapokuja mwenyewe na kukana...!
  Lakini kama ni kweli basi wastahili hongera kwa kufanikiwa kumzidi kete baba mchungaji!
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahahahahahaha Ta Kamugisha bana. . .asante sana kwakunikumbusha hii kitu. Ngoja nimuombe mtu nauli alafu akishakubali tu namzingua nayo nione reaction. . . Lolzzz

  Nwy hongera kwakufanikiwa kutuma pesa ya stamp na bahasha, FINALLY, maana ndivyo vilivyokuwepo kati yako na barua.

  Akupendae daima,
  Lizzy.
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Heheheheh. . . acha afurahi kwa siku mbili tatu bana, kupendwa na kuachwa ni bora kuliko kutokupendwa kabisa.
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kheeee. . .Umesahau kua nimeolewa? Mwanamke kutulia Konnie!!!Lolzzz
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kazi gani tena hiyo alomaliza Dubu?

  @Amy. . .
  Hata sipingi mwaya. Niliandika na kuituma mwenyeweeee.
   
 15. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Wala hayajakaa kibeberubeberu! Yamekaa kikike hasa!
  Namuonea gele ajabu kuibua hata mie kwa mbaali nilikua nammezea mate !
  Kumbe wakubwa wanafaudu !
   
 16. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,681
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha ha, Mh, don't be happy, you might have worn sex, but this is temporary victory.
   
 17. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Dah wapi Bishanga ndani Unga Ltd??
  Afrodenzi hebu mtafute. Bishanga aje kubadili LOCATION haraka..
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Acha umbea wewe. . . Ntakuvisha sketi.
   
 19. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...kweli, faraja jipe mwenyewe.
   
 20. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Lol mwanaume umbea kusutwa inakaribia kuwa suna....
  Teh kwani unataka kumiliki wote?
  Lol mwachie basi Eliza wa Tegeta Bishanga wake
   
Loading...