Jamani kwanini mjadala uwe dar,dodoma na zanzibar, ndiyo tanzania nzima? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani kwanini mjadala uwe dar,dodoma na zanzibar, ndiyo tanzania nzima?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KWELIMT, Apr 9, 2011.

 1. K

  KWELIMT Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni nchi kubwa yenye ukubwa wa 945,000 sq km (365,000 sq miles na yenye idadi ya watu milioni 42,500,000 (IMF, 2008).Pia nchi hii ina mikoa zaidi ya 26(jumlisha mipya zaidi ya 3 iliyotangazwa)na wilaya 127 kwa takwimu ambayo haijajumuisha wilaya mpya na majimbo ya uchaguzi 239(NEC data,2010).
  Kutokana na maelezo ya hapo juu ni dhahiri kwamba huu mjadala wa muswada wa kuunda tume ya kuratibu hiyo katiba mpya kufanywa ktk mikoa DSM,DODOMA NA ZBR ni kuwanima wanchi wengi haki yao ya msingi kama ilivyoanishwa kwenye ibara ya 18 ya katiba ya 1977.
  Mi nadhani hizi kamati bunge zingepita kila mkoa na wilaya ili zipate maoni ya watu wengi.Huu uwakilishi wa mikoa hii una dhamira ya dhati ya kupata maoni ya walalahoi wa nchi ambao ikumbukwe zaidi 80% wanaishi vijijini,je watatikana KARIMJEE,au ukumbi wa Msekwa?
  Tatizo la viongozi wa Tanzania wako seroius na mambo yasiyo muhimu kuliko mambo muhimu kwa mustakabali wa taifa.
  kw watu walivyochoka vurugu zaidi itegemewe.   
 2. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  hata mimi siungi mkono miswaada kuendeshwa mikoa mi3 tu out of 26. Angalizo langu ni kuwa politicians ndo wamesababisha haya yote. mifano imeonekana wazi wazi, hakika imenisikitisha sana. Katiba ni ya wananchi wote wa Tanzania iweje leo ishupaliwe na viongozi wa vyama vya siasa? halafu iweje ifanyikie Dodom(CCM)+Dar(CDM&CCM)+Zenj(CUF&CCM)?
   
 3. D

  Danniair JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani ni akina nani hao waliomo ktk kamati hii? Je, vyama vya siasa vina wawakilishi wake ndani ya kamati? Nauliza kwa sababu wao ndio walioanzisha mjadala wa katiba mpya. Ktk uchaguzi mkuu viongozi, wagombea waliirudia kanda ya ziwa mara mbili ktk kampeni zao wakijua fika kuwa huko ndiko kulikokuwa na watu wengi. Sitaamini kuwa zoezi hili huko halitafika. Wito wangu: Kamati iende mkoa hadi mkoa, huku ikiwa na vituo mbali mbali vya kukusanyia maoni, pia siku hizo zitangazwe vizuri kama ilivyokuwa wakati wa daftari ya wapiga kura. Tena kama fujo zinajitokeza kwani siku hizi kuna intelejensia basi warudi nyuma na utaratibu wa picha uanze. Kwani inavyoonekana tayari masilahi ya vyama yameanza kujitokeza. Mwisho kabisa nawatakia heri kamati hii nikiwakumbusha kuwa wakivuruga basi wajue ifikapo zamu yao ya uongozi wa kisiasa wataumia kama ilivyokuwa kwa rais Chiruba. Gooddayyyyyyy.
   
 4. D

  Danniair JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa nimeelewa swali kufuatana na kanuni za bunge sheria ndivyo ilivyo kuwa hao wabunge hao waweka vikao vyao maeneo hayo kwa siku hizo 3. Ndipo warudi
  bungeni kusema sawa au la.
   
Loading...