Jamani kwa miundombinu mibovu bila mipango mbadala tutafika?

danco

New Member
Oct 16, 2011
2
0
Wana JF, Hivi kweli tunapofikiria suala la maendeleo ya nchi yetu itawezekana kwa aina ya viongozi tulionao? nimekuwa nikifuatilia baadhi ya nchi zilizopiga hatua kimaendelea duniani zimekuwa na vipaumbele vya kutekeleza na hasa upande wa miundo mbinu. Ni pale tu miundo mbinu inapokuwa vizuri ndipo shughuli za kimaendeleo zinaweza kufanikiwa. Hapa kwetu Tanzania, barabara haziko ktk hali nzuri ya kusapoti maendeleo, reli ndiyo usiseme, ndege ndiyo sasa tumebakiza 1, maji ndiyo asilimia chini ya 20 ya Watanzania wenye maji safi na salama, Umeme ndiyo usiseme, nk.

Hivi ndugu zangu, kwa ubovu wa vitu hivyo nilivyovitaja hapo juu, sitegemei kama tutapata maendeleo, kwani hata sekta binafsi zimedumaa kwasababu mtu aliyejiajiri anashindwa kufanikiwa kutokana na vikwazo hivyo hapo juu. Mimi naamini kabisa, ya kwamba bila ya kufanya mabadiliko ya KATIBA (ili kupunguza nafasi ya Rais hasa kuteua watendaji mbalimbali ambao kwa kiasi kikubwa huo uteuzi unaangalia USHIKAJI na mengineyo na si uwezo wa mtu husika, kuondoa nafasi nyingi zisizo na manufaa kwa Taifa kama Ukuu wa Wilaya na Mkoa ambazo ni gharama kubwa sana kuziendesha hizo ofisi wkt kuna wakurugenzi).

Pili ni kuwa makini ktk kuchagua viongozi wa nchi; kwani kiongozi wa nchi ambaye hajui kwanini Watanzania ni maskini, kwanini tuna tatizo la umeme, kwanini miundombinu ni mibovu, kwanini bajeti ya nchi sehemu kubwa ni matumizi ya kawaida na si kwa ajili yamaendeleo; Kiongozi ambaye anatumia gharama kubwa kwa safari nyingi sana ambazo kati ya hizo nyingi hazina maslahi kwa Taifa isipokuwa yeye mwenyewe, Kiongozi ambaye anafurahia safari badala ya kushughulikia matatizo ya nchi yake.

Mimi naamini kabisa kwamba wakati umefika wa kuchagua kiongozi mwenye Plan B, C, n.k kwa ajili ya ufumbuzi wa wananchi na si asiye na uelewa wowote katika masuala ya ujenzi na vipaumbele vya Wananchi. Naamini imefika kipindi tunahitaji kiongozi mwenye vision na nchi, mwenye kujua baada ya miaka 2,3,6 au 10 nchi itakuwa imefanya 1,2,3,4 n.k kwa ajili ya uchumi wa nchi. Na si viongozi wenye kusubiri mazingira yawafikishe huko automatically na si kutumia mazingira yaliyopo kumfikisha anapotaka nchi ifike.

Nimalizie kwa kusema, hakika aina ya viongozi tulionao kwenye ngazi za juu HAWANA VISION, HIVYO TUSITEGEMEE MIUJIZA YA KIMAENDELEO, KWANI HAWAJUI NI KWANINI TANZANIA NI MASKINI PAMOJA NA KWAMBA INA RASILIMALI NYINGI SANA KAMA WATU, MADINI, MAZIWA, MITO, ARDHI, MBUGA ZA WANYAMA, N.K.; MUNGU AKUPE NINI TENA HAPO?

Nawakilisha Wadau.
 
Back
Top Bottom