Jamani kuna tatizo kubwa ofisi ya mkaguzi na mthibiti mkuu wa serikali (cag)

Maseto

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
864
Points
250

Maseto

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
864 250
Ndugu zangu wanajf.
Nimegundua kuwa kuna tatizo kubwa mno katika utendaji wa ofisi ya cag.mwaka jana hapa katika halmashauri ya wilaya ya musoma madiwani waliikataa rasmi taarifa ya cag kwa mahesabu ya halmashauri hii pamoja na cag kutoa hati safi.madiwani hao waliikataa taarifa hiyo baada ya kukagua baadhi ya miradi ambayo walibaini kuwa miradi mingi ilikuwa iko chini ya kiwango.walihoji kuwa kwa nini cag alitoa hati safi wakati miradi hiyo ilikuwa chini ya kiwango.
Si muda mrefu baada ya tukio la musoma cag alilaumiwa kwa kutoa taarifa isiyo sahihi kuhusiana na ubadhilifu wa katibu mkuu wa wizara ya nishati bwana jairo.
Mwaka huu mhe.zito alisikika akimtetea bwana mhando wa tanesco kwa hoja kwamba tanesco ilikuwa na hati safi kutoka kwa cag.lakini cag huyo huyo alipotakiwa kuikagua tena tanesco ameibua madudu kibao ikiwa ni pamoja na wizi wa zaidi ya bilioni 86 za kitanzania.
Ajabu ni kwamba zito huyo huyo anasema wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.zito ni mwenyekiti wa kamati ya mashirika ya umma.hivi yeye na cag huwa hawaoni madudu katika mashirika ya bandari,atc,tanapa,na kadhalika.
 

Forum statistics

Threads 1,392,959
Members 528,739
Posts 34,123,429
Top