Jamani kuna nini kwani kinaendelea Tanzania kwa sasa?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,018
16,801
Ukiamka unasikia sijui Gwajima hujakaa sawa sijui Makonda na vyeti feki hujajipumzisha mara unasikia tena sijui Halima Mdee na Spika Ndugai ukiangaza angaza tena unasikia sijui mchanga wa dhahabu na mtu bado hujapumzika na unayatafakari hayo mara ghafla tena unasikia sijui akina roma wamefanywa nini.

In short Mimi Mtanzania mwenzenu nimechanganyikiwa na haya ya nadhani nahitaji counseling ya kutosha kwani naanza kwa mbali kuichukia Tanzania na huko tuendako kama hali hii haitaisha au kumalizwa nadhani itabidi tu nimkabidhi rasmi roho yangu Israeli aondoke nayo tu Mbinguni kwa Baba Mungu.

Ndugu zanguni na wana JF wenzangu Tanzania yetu imekumbwa na nini sasa? Mwenye hii hofu na wasiwasi ni Mimi peke yangu tu au?

Ewe Mwenyezi Mungu tusaidie!
 
Yesu anasema atakaye kupenda maisha na kuziona Siku njema basi auzuie ulimi wake usinene mabaya na midomo yake isiseme hila na aitafute amani. Pia tukumbuke auwaye kwa upanga atauwawa kwa upanga.
 
Ndugu, ni upepo mbaya tu unapita kipindi hiki. Hali itatulia muda si mrefu.
Kwani hizi drama zimesababisha Shughuli zako zisimame?
 
  • Thanks
Reactions: e2n
Je tatizo hulijui??? Miaka iliyopita ilikuwa kama ilivyo sasa??? Je nani alaumiwe sisi, yeye au wao??
 
Ukiamka unasikia sijui Gwajima hujakaa sawa sijui Makonda na vyeti feki hujajipumzisha mara unasikia tena sijui Halima Mdee na Spika Ndugai ukiangaza angaza tena unasikia sijui mchanga wa dhahabu na mtu bado hujapumzika na unayatafakari hayo mara ghafla tena unasikia sijui akina roma wamefanywa nini.

In short Mimi Mtanzania mwenzenu nimechanganyikiwa na haya ya nadhani nahitaji counseling ya kutosha kwani naanza kwa mbali kuichukia Tanzania na huko tuendako kama hali hii haitaisha au kumalizwa nadhani itabidi tu nimkabidhi rasmi roho yangu Israeli aondoke nayo tu Mbinguni kwa Baba Mungu.

Ndugu zanguni na wana JF wenzangu Tanzania yetu imekumbwa na nini sasa? Mwenye hii hofu na wasiwasi ni Mimi peke yangu tu au?

Ewe Mwenyezi Mungu tusaidie!
Taratibu utazowea hata Rwanda b4 1959 ilikuwa poa zilivyoanza vurugu watu waoga wakakimbia nchi lakini kizazi hiki hakina haja ya kukimbia nchi maana nchi ni mali yako unakimbilia wapi?
 
Njaa kali watu hawana hela , vyakula juu , ubunifu hakuna ndo tatizo ya yote hayo mkuu. Wanaoshiba ni wachache, watu wamejizira na kujichoka hali ambayo ni mbaya kwa jamii.

Kila mtu atafuta jinsi ya kuwa maarufu apate pesa. We subiri pesa ikiaanza kumwagika kila mtu akashiba kama utasikia na utafuatilia hayo ya mitandao.
 
Watanzania ach tulie tu kwa ujinga wetu. Miaka yote tunalia maji umeme mashamba wanauziwa akina fulani madini yanaibwa tembo na faru wameisha twiga wanaibwa mchana. Yoote haya na mengine tunayalilia kila siku lkn ukifika ule wakati mkipewa pilau baai akili yote inahamia kwenye beseni. Tunasahau yote tunasema tunapenda kusoma namba. Acha tu tuchanganyikiwe kwakweli
 
Bongo full disco weka muziki,we acha kelele piga muziki
Ben saambili kapotea
Madawa ya kulevya
Leta muziki Manji, gwajima,wema karipoti centro
Leta muziki Bashite wa kolomije kavamia klaaaaus na mibastola

We leta maneno acha muziki,
Nape kaunda tume kufanya uchunguzi uvamizi klaaaausss radio.

Tume ikaja na majibu mda mfupi sana.
Leta muziki
Nape kasahau pale waziri yuko chini ya nani?
Kapewa majibu kimbelembele kapeleka mbele.
Leta muziki
Nape katumbuliwa.
Acha muziki kaitisha press conferens.
Mara katishiwa bastola.

Mara anadai wanataka kumuuwa.
Muziki karudi mtama jimbo lake ubunge kutumikia wananchi
Piga muziki Nay "natishiwa kuuwawa"

Lete muziki Halima mdee muheshimiwa "We fala kaa kimya"♩
Leta muziki "Roma mkatoliki katekwa".
"Atapatikana before j2"by kolomije boy

Leta muziki "mi nakaa kimya"by msafi alumasi☎
Gwajima "ntamtumbua huyu alumasi iwe maji
Saturday kina Roma wametupwa beach ununio, wakatembea kupata baja, then wakaenda hm then O bay kuripoti.

Leta muziki acha maneno .
Press conferens j3.
Mara mwambyeke katokea kabla ya aliyeitisha press.
Leta muziki conference imeisha.
Roma hajasema lolote la maana zaidi ya kusema kapigwa sana, na nani hamjui.

Leta muziki, sijui kesho kunani walahi
Mnafanya kazi nyie watu kweli??
Episode 2 coming soon
 
we jamaa achana na tanzania pambana na maisha yako hawa jamaa ni wampito tu, miaka yao ikizidi sana ni kumi tu kama watatoboa watu wa hivi wala sio wakukupa stress badilika nao
 
Nchi iko salama tu hakuna shida ila Tanzania tunapenda maneno sana ya umbeya na udaku.

Nchi haina shida kabisa ila Dr Magufuli ana vita na wengi ktk system kimaslahi baada ya kubana njia zote za ufisadi.

Kwahiyo kuna mbinu nyingi zinatumika kudhoofisha utawala wake toka kwa mafisadi.
 
Hakuna nchi iliyo salama wewe! Achana na kudumaza akili yako huku ukifumba macho eti nchi iko salama!

Nchi iko salama tu hakuna shida ila Tanzania tunapenda maneno sana ya umbeya na udaku.

Nchi haina shida kabisa ila Dr Magufuli ana vita na wengi ktk system kimaslahi baada ya kubana njia zote za ufisadi.

Kwahiyo kuna mbinu nyingi zinatumika kudhoofisha utawala wake toka kwa mafisadi.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom