Jamani,,kipi bora...mafuta ya taa au umeme?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani,,kipi bora...mafuta ya taa au umeme??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchaga wa ukwel, Jul 20, 2011.

 1. M

  Mchaga wa ukwel Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku 2 zimeisha tangu nikiwaza umuhimu wa umeme na mafuta ya taa kwa walio wengi. Najua atakaepinga kuwa mafuta ya taa ni zaid atakuwa mwenda wazimu,au amezaliwa gorofani na kukulia forodhani. Kwa mwanakijiji yeyote anaejua historia yake na hali yake kiuchumi,mafuta ya taa ni msaada mkubwa kwake as long as hana uwezo wa kujipatia umeme.na afteral watanzania weng ni maskini. Sasa najiuliza iweje wabunge wapitishe mafuta kupanda bei na wakat umeme unaotumika na asilia ndogo ya watanzania vijijini bajeti yake ikataliwe? Kwanin wasingekataa na ile ya mafuta? Ni kweli wanatuwakilisha walala hoi? Kipato cha kabwela ni dola ngapi? Wabunge wanatumia akili kweli au matope? Tuwaeleweje? Au wanafuata mkumbo,mtu fulan akikataa basi nawenyewe wanafuata? Kwanin mawazo ya wapinzani yanaonekana si lolote ilihali wana ccm hata wakitoa mawazo mgando wanasikilizwa? Ni mara ngapi wapinzani wanatetea wanyonge sauti zao zinazimwa na NDIO ZA CCM? Naombeni mchango wenu wakereketwa!!
   
 2. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  aisee mangi umeongea la maana kweli, hili nalo limo kwenye hi bajeti ya Wizara Nishati na Madini, ni kweli wabunge wetu wote wapinzani na wa CCM wote wanazungumza kuhusu umeme tu wakati wengi wao wanawakilisha watu wasio tumia umeme.
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  si kweli kwamba kupinga mafuta ya taa ni zaidi ya umeme kwa umuhimu ni kwenda na wazimu, mafuta ya taa yanatumiwa moja kwa moja (direct) na watanzania zaidi ya asilimia 80 wakati wanaopata umeme ni 20%, na unatumiwa na wananchi wote indirect!!! ingawa siungi mkono watetewe wachache dhidi ya wengi, nafahamu mafuta ya taa yanatumika na wengi kupata mwanga (taa-chemli, vibatari, karabai n.k) kidogo kuendesha majokofu, umeme ni zaidi ya taa!!! viwanda vyaendeshwa kwa umeme, mifumo yote ya mawasiliano, umeme,taasisi za fedha, umeme, mifumo rahisishi ya kielectronic umeme, nimetaja machache, kwa hiyo msingi wa hoja ukiwa mafuta ya taa ni muhimu zaidi ya umeme sikuungi mkono, ukimaanisha upendeleo wa moja kwa moja wa wananchi wachache dhidi ya wengi kwenye nishati yao pekee iwapatiayo mwanga nitakuunga mkono, hata ukiratibu maandamano ya kupinga nitakuwa mstari wa mbele.
   
Loading...