Jamani kila wimbo ni mapenzi !

Calist

Senior Member
Dec 17, 2010
130
0
Nimekaa kwenye Luninga kwa takribani saa nzima nikiangalia kipindi cha nyimbo bora 2010 kinachorushwa na Star TV, cha ajabu nyimbo zote ninazoziona zinazungumzia mapenzi tu mwanzo mwisho, ina maana wabongo hatuna uwezo wa kuimba nje ya mapenzi ?
 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
1,195
that's the only industry in which we thrive suspiciously fairly well! Kumbuka hata kwenye big brother!
 

Mtoto wa Kishua

JF-Expert Member
Oct 15, 2009
834
225
Ukiimba umasikini sio wote wana guswa na umasikini, ukimba ujamaa sio wote wana guswa na ujamaa, ukiimba ucha Mungu sio wote wana guswa na ucha Mungu, ukiimba maadaili sio wote wana giswa na maadili ,ukiimba kufunza nakujenga jamaii sio wote ana guswa na hayo, lakini ukiimba mapenzi karibu kila mtu ana guswa na mapenzi ndio mana siku zote mapenzi yatakubalika ,karibu kila mtu anakutana nayo! na nadhani ni watu wachache wasio guswa namapenzi labda unaweza kua ni wewe peke yako, sasa kwanini msanii ambaye anataka kuuza kazi yake akuhangaikiwe wewe peke yako kukuridhisha wakati ana hitaji kujikumu na maisha kwa kuuza kazi yake kwawengi wanao isikiliza? , maana ina wezekana labda wewe hata kazi hununui au ni mara moja moja , je ni kuulize mara ya mwisho umenunua kazi za wasanii yeyote iwe mapenzi au Ujamaa lini ilikua?
 

Calist

Senior Member
Dec 17, 2010
130
0
Mtoto wa Kishua umejitahidi kujitetea lakini unataka kuniambia wasanii kama Rose Mhando, Mr, Ebo, ebo,wakina camirion,na wengine wengi ambao hajikiti sana kwenye nyimbo za mapenzi hawatoki? Mi naona ni kukosa ubunifu tu, na hii ni kwa wanaojiita wanamziki wa bongo ambao mziki wao hadumu hata miezi miwili unapotea kabisa.
 

Baba Mtu

JF-Expert Member
Aug 28, 2008
871
225
Nimekaa kwenye Luninga kwa takribani saa nzima nikiangalia kipindi cha nyimbo bora 2010 kinachorushwa na Star TV, cha ajabu nyimbo zote ninazoziona zinazungumzia mapenzi tu mwanzo mwisho, ina maana wabongo hatuna uwezo wa kuimba nje ya mapenzi ?

Nyimbo unazozitaka wee zilishaimbwa na wanamuziki wa zamani, hawa wa bongo fleva hawana uwezo wa kutunga nyimbo hizo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom