Jamani Kamshahara kangu!!!!!!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,700
Jamani naombeni japo mnipe ka elimu kidogo kuhusiana na bajeti ili niweze kusavaivu katika sikukuu hizi zijazo za mwezi wa Desemba. Kamshahara kenyewe ni TGS.D na kabla ya tarehe 20 Desemba kuna mambo yafuatayo natakiwa nikamilishe.
1. Kuna kadi sita za harusi.............kiwango kwa kuwa nipo single kila moja elfu 20.
2. Kuna kadi ya mchango wa birthday ya mtoto wa mwenye nyumba mwisho tarehe 10 Desemba.
3. Kuna fomu ya mchango wa ujenzi wa ofisi ya CCM............hii nimepewa na bosi wangu, inabidi nichangie ili kuongeza imani mbele ya bosi, nisije nikakosa safari za kiofisi.
4. Kadi mbili za send-off.
Hapo ili kukamilisha hayo mambo yote hapo kamshahara kote kameisha.............wenye uzoefu huwa mnasavaivu vipi katika hali kama hii??
 
Watumishi wote serikalini wezi,wanaishi kwa rushwa,visafari vya uongo na kweli,tender hewa,allowance za kazi hewa za masaa 1 inaandikwa 4
 
Msaidie bosi wako kuchangia SISIEMU, lakini hiyo michango ya mingine ni bullshit!
 
dah! kaka kumbe wewe una mshahara? nipige jeki walau na buku tano tu! nime uwawa vibaya!
 
Kaka kimbia haraka hiyo kazi ya kizushi wakati bado kijana na nguvu zako
 
Achana na kuchangia harusi, yaani kwa mwezi arusi nane na zote mchango si chini ya 20elfu??

Mchangie mwenye nyumba wako elfu kumi ya besdei na zawadi ya mtoto na kuhusu ofisi ya ccm sina wazo.
 
Duh! Mchango wa birthday upotezee. Nenda kwa bosi wako kwa lengo la kuomba ushauri kama ulivyokuja hapa, mwambie kama vipi akukopeshe.
Kama hiyo haifai tafuta ugonjwa ulazwe hospital. Watu watakuwa wanakuletea hela za pole. Make sure hautok hosp hadi harusi, birthday na huo mchango wa sisim ushapita.
 
Watumishi wote serikalini wezi,wanaishi kwa rushwa,visafari vya uongo na kweli,tender hewa,allowance za kazi hewa za masaa 1 inaandikwa 4
Hii yote inasababishwa na vimishahara vidogo vinavyotolewa na serikali.
 
Msaidie bosi wako kuchangia SISIEMU, lakini hiyo michango ya mingine ni bullshit!
Hili siwezi kulikwepa maana bosi mwenyewe kalishikia bango ile mbaya sijui kaahidiwa ukurugenzi!
 
dah! kaka kumbe wewe una mshahara? nipige jeki walau na buku tano tu! nime uwawa vibaya!
Siyo mshahara kaka ni kamshahara maana hakatulii hata siku moja.
Weka kiasi cha Mshahara ilituchakachue!
Du!!!
Achana na kuchangia harusi, yaani kwa mwezi arusi nane na zote mchango si chini ya 20elfu??
Hili ni tatizo kwa kweli kaka, lakini nina wasiwasi na mimi nikifikia wakati wa kuoa nitahitaji michango yao, jamii yetu ndio imekuwa hivyo.....lakini kwa hii lazima niwatose.
Mchangie mwenye nyumba wako elfu kumi ya besdei na zawadi ya mtoto na kuhusu ofisi ya ccm sina wazo.
Nitafanya hivi!!!!
Duh! Mchango wa birthday upotezee. Nenda kwa bosi wako kwa lengo la kuomba ushauri kama ulivyokuja hapa, mwambie kama vipi akukopeshe.
Kama hiyo haifai tafuta ugonjwa ulazwe hospital. Watu watakuwa wanakuletea hela za pole. Make sure hautok hosp hadi harusi, birthday na huo mchango wa sisim ushapita.
Huu ushauri mzuri sana........lakini namna ya kuigiza ugonjwa ndio ishu.
 
Duh! Mchango wa birthday upotezee. Nenda kwa bosi wako kwa lengo la kuomba ushauri kama ulivyokuja hapa, mwambie kama vipi akukopeshe.
Kama hiyo haifai tafuta ugonjwa ulazwe hospital. Watu watakuwa wanakuletea hela za pole. Make sure hautok hosp hadi harusi, birthday na huo mchango wa sisim ushapita.

teh teh,we humtakii mema mwenzio,akilazwa hospitali yenyewe m,nyamala ama amana au temeke si atafia huko.
 
Duh! Mchango wa birthday upotezee. Nenda kwa bosi wako kwa lengo la kuomba ushauri kama ulivyokuja hapa, mwambie kama vipi akukopeshe.
Kama hiyo haifai tafuta ugonjwa ulazwe hospital. Watu watakuwa wanakuletea hela za pole. Make sure hautok hosp hadi harusi, birthday na huo mchango wa sisim ushapita.

Hii kali, akalazwe wapi? kama hospitalza serikali zimejaa watu wanalala mzungu wa nne, labda wodi ya TB na cholera ndo kuna nafasi.
Na akienda hospital binafsi, malazi peke yake kwa cku si chini ya elfu15....!!
 
duh! Mchango wa birthday upotezee. Nenda kwa bosi wako kwa lengo la kuomba ushauri kama ulivyokuja hapa, mwambie kama vipi akukopeshe.
Kama hiyo haifai tafuta ugonjwa ulazwe hospital. Watu watakuwa wanakuletea hela za pole. Make sure hautok hosp hadi harusi, birthday na huo mchango wa sisim ushapita.

u have made ma dei. Thx
 
Hii kali, akalazwe wapi? kama hospitalza serikali zimejaa watu wanalala mzungu wa nne, labda wodi ya TB na cholera ndo kuna nafasi.
Na akienda hospital binafsi, malazi peke yake kwa cku si chini ya elfu15....!!

wafanyakazi wengine huwa wanagaramiwa huduma za afya.
 
wafanya kazi wengi wa serikali wanaishi kwamagumashi.......sijaona jambo la msingi uliloeleza ili nikusaidie namna ya kubajeti....

piga chini wote ....michango....michango......we vipi?

nilidhani unasomesha.....una ujenzi,......kumbe michango ya harusi...shauri yako na upendo wa mshumaa
 
Tengeneza safari za kughushi kama mfanyavyo serikalini
lazimisha upate imprest uchakachue
Jiingize katika deal za kitapeli upate faranga
 
Kwani kwa sasa TGS D ni Tsh ngapi, TGS E ni Tsh ngapi, TGS F ni Tsh ngapi na TGS G ni Tsh ngapi?
 
duuh pole mkuu na hii michango ya harusi kama hujaoa bado kuipiga chini ni very risky...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom