Jamani Imani za 'Vita ya Majimaji Bado ipo miongoni mwa watanzania!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Kuna watu watatu wameuwawa, usiku wa manane, kwa madai ya kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji (wamasai) wilayani Kiteto. Inasemekana marehemu walikuwa wakifanya tambiko la asili ili risasi zisiwadhuru watakapoanzisha 'vita' kugombea ardhi katika kijiji cha Sunya.

Hata hivyo wauaji waliwawahi kabla tambiko halijakamilika wakihofia kwamba huenda kweli wasingedhurika na risasi iwapo tambiko lingekamilika. Wakaamua kuwafyatulia risasi na kufanikiwa kuwauwa watu watatu miongoni mwa watambikaji. Makubwa hayooo wanajamii forum!

Tanzania kazi baaaado kwelikweli!
 
Back
Top Bottom