Jamani ile ndege yetu na zile dola za kutoka Acacia vipi?

Maboya ni nyinyi msiokuwa na majukumu wa kiserikali. Kazi inafanywa kiuhakika, nyinyi mnageuka kuwa wasaliti, mnadhani hizi ni zama za ile smile ya JK.
Dawa ya deni ni kulipa, ingekuwa mnafanya kazi kiuhakika msingeitia Nchi hasara kubwa. Bomba mapenzi mshatutia hasara kwa kulipa cash kwa kutaka cha juu na imekamatwa na Dreamliner nayo itaota mbawa tena hiyo kazi ya uhakika ipo wapi?
 
Aliyesababisha ikamatwe yupo hospital Ulaya, kaenda kuwaonyesha wazungu malipo halisi ya usaliti kwa nchi aliyozaliwa.

Ni changamoto za muda na ndio maana ya majukumu mazito, nyinyi dawa yenu imeshapatikana,mkiuza siri za nchi kwa wanaotudai huko nje lazima cha moto mkione.
 
Kejeli kama hizi zinawakilisha akili ya kutotaka kuiona nchi uliyozaliwa ikisonga mbele, yaani mtu anafurahi kuona taifa lake linashindwa kupiga hatua!!.

Hizi ni purely akili za mtu mweusi. Na wanasiasa hutofautiana kwenye kushughulikia wasaliti, wengine huwapelekea shaba na kuwaondoa duniani, wengine wenye mioyo yenye uvumilivu huwavumilia tu.
So haya ndiyo majibu ya mtu mweupe pale anapokuwa hana jibu la hoja ngumu
 
Acha uchochezi

Mkuu umenichekesha sana awamu ya tano ukiuliza vitu vya msingi ni uchochezi sasa mbwembwe za nini live TBC Accasia wezi mara kampuni haijasjiriwa hii awamu waache mambo ya kudanganya wananchi mara acacia wamekubali kulipa Mambo ya ovyo tu Ndege ilisababisha Tundu Lissu kwa kusema ukweli Nachojua Uhongo audumu
 
Kukosoa ndio sifa kubwa ya mtanzania, wala hana aibu wala hajijui kwamba anafanana na lori lililonasa kwenye matope.

Sisi ni wavivu, na madhara ya huo uvivu wetu ndio hii tabia ya kudhani kwamba fulani ndio chanzo cha umaskini wetu.

Tabia mbovu sana ya kujifariji, huku suluhisho la tatizo letu likibakia kwetu sisi wenyewe. Poor Tanzanians.
Mbona hueleweki kama unajibu swali la mleta mada, au umekuja kuleta maumivu yako yalioko moyoni, naona umeandika huku unalia. Mwendawazimu wew
 
Usaliti ni kitu kibaya sana. Watu wanapambana ili Tanzania iweze kukuza utalii wake, iweze kufikika moja kwa moja kwa kutumia ndege zake yenyewe, mtu mmoja anaibuka na kutengeneza mazingira ya ndege hizo zisiweze kupatikana!!.

Unaposhirikiana moja kwa moja na watu wa nje ili kuikomoa nchi yako uliyozaliwa, maana yake wewe ni mtu hatari sana kwa afya ya uchumi wa nchi hiyo hiyo.

Suala la mtu kuwa mrundi au mnyarwanda sio muhimu sana, tunaangalia uzalendo na uchapakazi wake.

Wewe una ushahidi gani kama huyo unayemuita Baba yako ni Baba yako wa kweli kabisa?. Upo uwezekano Mama anafahamu kuwa mzee wako ni Mkongo au Mrundi.

We kama una mtoto basi asifuate akiri zako unavyofikilia Lissu maneno yake yalikua yanaweza kusababisha Ndege isije? Daaah Lissu alikua anatoa ushauri
 
Kukosoa ndio sifa kubwa ya mtanzania, wala hana aibu wala hajijui kwamba anafanana na lori lililonasa kwenye matope.

Sisi ni wavivu, na madhara ya huo uvivu wetu ndio hii tabia ya kudhani kwamba fulani ndio chanzo cha umaskini wetu.

Tabia mbovu sana ya kujifariji, huku suluhisho la tatizo letu likibakia kwetu sisi wenyewe. Poor Tanzanians.
Mkuu, usiwatukane watanzania eti kwa Kuwaita wakosoaji, wavivu, walalamishi na eti unawafananisha na Lori lililonasa kwenye matope....., jikite katika kujenga hoja yako wewe binafsi, bila kuongelea watanzania kwa ujumla wao. Watanzania ni watu makini wanaojielewa na no wachapakazi, huenda wewe ndiyo umepoteza dira....
 
Kelele wewe, ipo pesa ya kununua wapinzani tu. Unataka ndege una nauli? Mpiga dili ww.
 
Dege Bombardier lipo nje pale viunga vya Toronto na kwa sasa linapigwa winter ya Canada lingekuwa na namna ya kulalamika lingesema..

Za chini ya Kapeti, wale wadai wanainyemelea hivi sasa Dreamliner Boeing 787 (iliyo kiwandani) kupitia shauri jingine limefunguliwa USA..

Punde hii itawekwa hadharani..

Dawa ya deni ni kulipa tu.

Du! mbona wanatukaba hivi?
 
Mbona hueleweki kama unajibu swali la mleta mada, au umekuja kuleta maumivu yako yalioko moyoni, naona umeandika huku unalia. Mwendawazimu wew
Wendawazimu ni kushirikiana na wageni kwa nia ya kuiangamiza nchi yako.

Wendawazimu ni kuisaliti nchi yako kwa kuhujumu juhudi za nchi katika kuimarika kwenye sekta ya anga.

Mleta mada anaongea sarcastically, nyuma ya maneno yake kuna aina fulani ya kejeli.
 
Aliyesababisha ikamatwe yupo hospital Ulaya, kaenda kuwaonyesha wazungu malipo halisi ya usaliti kwa nchi aliyozaliwa.

Ni changamoto za muda na ndio maana ya majukumu mazito, nyinyi dawa yenu imeshapatikana,mkiuza siri za nchi kwa wanaotudai huko nje lazima cha moto mkione.
Ukisemwa ukweli unaitwa msaliti
Ukipiga picha Mali zilizojengwa Kwa kodi ya wananchi ambazo hazijakidhi viwango mnawaita wasaliti .....hapo kweli kazi ipo

Ova
 
We kama una mtoto basi asifuate akiri zako unavyofikilia Lissu maneno yake yalikua yanaweza kusababisha Ndege isije? Daaah Lissu alikua anatoa ushauri
Sio kila kinachofanyika maishani kinaandikwa magazetini. Ndio maana ya nchi kuwa na intelligence iliyo kazini masaa 24.
 
Mkuu, usiwatukane watanzania eti kwa Kuwaita wakosoaji, wavivu, walalamishi na eti unawafananisha na Lori lililonasa kwenye matope....., jikite katika kujenga hoja yako wewe binafsi, bila kuongelea watanzania kwa ujumla wao. Watanzania ni watu makini wanaojielewa na no wachapakazi, huenda wewe ndiyo umepoteza dira....
Nimeongelea muktadha wa hii mada sio kitu kingine, jifunze kuyatazama masuala katika mtazamo mpana zaidi.

Ni aibu sana kwa mtu kuwa na fikra za kutaka kuona uongozi wa nchi yake unakwama katika juhudi za kubadili hali ya maisha.

Hao majirani zetu wakenya wametuacha mbali kwa sababu ya sisi kwa miaka mingi kukosa ule mtazamo wa Tanzania kwanza linapokuja suala la kuipaisha nchi yetu.

Imeibuka roho ya usaliti, na ni mbaya sana kwa sababu inaondoa ule umoja wetu ambao ndio silaha ya nchi kuweza kufikisha miaka 56 ya uhuru.
 
Ukisemwa ukweli unaitwa msaliti
Ukipiga picha Mali zilizojengwa Kwa kodi ya wananchi ambazo hazijakidhi viwango mnawaita wasaliti .....hapo kweli kazi ipo

Ova
Mkuu usaliti una maana pana zaidi ya hoja zako. Kuwatisha watu kwamba tutashtakiwa MIGA ni usaliti pia, kujenga uoga miongoni mwa watu ni usaliti mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom