Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,395
Binti yangu ndio kwanza ametimiza miaka 7 mwaka huu, lakini amekuwa na mabadiliko makubwa sana kitabia. Ni mwaka huu ndio ameingia darasa la pili na amekuwa ni mdadisi na mbishi kupindukia.
Kuna wakati kama tunaangalia kipindi kwenye TV, naweza kutoa maoni yangu juu ya kipindi hicho, kama maelezo yangu hayatakuwa sahihi kulingana na uelewa wake, basi atabishana na mimi na mara nyingi anatoa reference za mwalimu wake (yaani jinsi walivyofundishwa) au kama aliwasikia wanafunzi wenzake wakilizungumzia jambo hilo, hata kama atakauwa amepotoshwa.
Nikiwa kama mzazi, najaribu kumuelewesha kulingana na umri wake lakini unaweza kuzuka ubishi mpaka nakereka. Mh! Watoto wa siku hizi wamekosa kweli adabu. Mfano, kulikuwa na tangazo la Kondom kwenye TV. Wakati tangazo likiendelea akaanza kusema, 'hizi kondom ndio zinazotumika kuzuia maambukizi ya Ukimwi'
Mimi kwa hekima nikamuuliza kwamba, ni nani amemfundisha, akanijibu kuwa ni mwalimu wao. Nikamwambia ni kweli lakini sio ukimwi tu bali pia hutumika kwa uzazi wa mpango………..
Basi alinikata kalma na kuniambia kuwa uzazi wa mpango wanatumia vidonge vya majira na sindano za kuzuia mimba……………… He! Nilishikwa na butwaa. Mke wangu alinitupia jicho kali kama ananionya, ikabidi nikae kimya……….. nikajua nimechemsha.
Haikuishi hapo, siku iliyofuata alinijia na vipeperushi viwili, kimoja kinachoelezea njia mbalimbali za uzazi wa mpango na kingine kilikuwa kikielezea juu ya maambukizi ya Ukimwi, pamoja na kinga zake, na alikuwa anataka kuthibitisha kile alichokuwa akikisema siku iliyopita.
Nilijaribu kumuelewesha kwamba, mambo hayo sio wakati wake kujifunza kulingana na umri wake, nilimshauri asubiri akiwa mkubwa atajifunza mambo hayo kwa undani. Lakini alizidi kusisitiza kwamba anataka kunithibitishia kwamba jana alikuwa sahihi. Ilibidi nikubali kuwa alikuwa sahihi ili kuepuka malumbano.
Amekuwa na tabia ya kunikosoa bila hata ya aibu na si mimi tu hata mama yake pia hutofautiana naye kwa mambo madogo madogo. Anaweza kutumwa aandae meza kwa ajili ya chakula, yeye anachofanya ni kuondoa vitu vilivyopo mezani tu na kukaa kimya akiulizwa kwa nini hajaandaa meza, anadai ameshaandaa na ndio maana iko safi na haina kitu. Mama yake akimuuliza kwa nini hajaweka sahani na maji na vitu vingine. Anamwambia hakuwa specific, ‘ulitakiwa uniambie nitenge chakula' atasema, akimkosoa mama yake.
Hebu nisaidieni nimfanyeje binti huyu…………………………?