Jamani huyu binti yangu ataniua kwa presha....

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Binti yangu ndio kwanza ametimiza miaka 7 mwaka huu, lakini amekuwa na mabadiliko makubwa sana kitabia. Ni mwaka huu ndio ameingia darasa la pili na amekuwa ni mdadisi na mbishi kupindukia.

Kuna wakati kama tunaangalia kipindi kwenye TV, naweza kutoa maoni yangu juu ya kipindi hicho, kama maelezo yangu hayatakuwa sahihi kulingana na uelewa wake, basi atabishana na mimi na mara nyingi anatoa reference za mwalimu wake (yaani jinsi walivyofundishwa) au kama aliwasikia wanafunzi wenzake wakilizungumzia jambo hilo, hata kama atakauwa amepotoshwa.

Nikiwa kama mzazi, najaribu kumuelewesha kulingana na umri wake lakini unaweza kuzuka ubishi mpaka nakereka. Mh! Watoto wa siku hizi wamekosa kweli adabu. Mfano, kulikuwa na tangazo la Kondom kwenye TV. Wakati tangazo likiendelea akaanza kusema, 'hizi kondom ndio zinazotumika kuzuia maambukizi ya Ukimwi'

Mimi kwa hekima nikamuuliza kwamba, ni nani amemfundisha, akanijibu kuwa ni mwalimu wao. Nikamwambia ni kweli lakini sio ukimwi tu bali pia hutumika kwa uzazi wa mpango………..
Basi alinikata kalma na kuniambia kuwa uzazi wa mpango wanatumia vidonge vya majira na sindano za kuzuia mimba……………… He! Nilishikwa na butwaa. Mke wangu alinitupia jicho kali kama ananionya, ikabidi nikae kimya……….. nikajua nimechemsha.

Haikuishi hapo, siku iliyofuata alinijia na vipeperushi viwili, kimoja kinachoelezea njia mbalimbali za uzazi wa mpango na kingine kilikuwa kikielezea juu ya maambukizi ya Ukimwi, pamoja na kinga zake, na alikuwa anataka kuthibitisha kile alichokuwa akikisema siku iliyopita.

Nilijaribu kumuelewesha kwamba, mambo hayo sio wakati wake kujifunza kulingana na umri wake, nilimshauri asubiri akiwa mkubwa atajifunza mambo hayo kwa undani. Lakini alizidi kusisitiza kwamba anataka kunithibitishia kwamba jana alikuwa sahihi. Ilibidi nikubali kuwa alikuwa sahihi ili kuepuka malumbano.

Amekuwa na tabia ya kunikosoa bila hata ya aibu na si mimi tu hata mama yake pia hutofautiana naye kwa mambo madogo madogo. Anaweza kutumwa aandae meza kwa ajili ya chakula, yeye anachofanya ni kuondoa vitu vilivyopo mezani tu na kukaa kimya akiulizwa kwa nini hajaandaa meza, anadai ameshaandaa na ndio maana iko safi na haina kitu. Mama yake akimuuliza kwa nini hajaweka sahani na maji na vitu vingine. Anamwambia hakuwa specific, ‘ulitakiwa uniambie nitenge chakula' atasema, akimkosoa mama yake.

Hebu nisaidieni nimfanyeje binti huyu…………………………?
 
mambo ya utandawazi hayo ... je ni shule ipi anasoma ni hizi za kigeni au za zamani??? je mazingira muishio uswahilini au??
 
Inawezekana ana kipaji cha kushika na kupembua mambo, huna cha kuhofia hapo zaidi ya kujivunia kuwa nae

Ahsante mkuu, lakini ningependa abadilike kidogo, yuko too much aggressive akim-critisize mtu huwa anatumia logic hata zisizo za kweli ili mradi ku-justify msimamo wake.....................yuko kama mwanasheria, kama kuna jambo ulilihukumu kwa kwa namna fulani halafu siku nyingine ukafanya tofauti, atauliza sababu............. halafu ana kumbukumbu kitu cha ajabu.....................
 
mambo ya utandawazi hayo ... je ni shule ipi anasoma ni hizi za kigeni au za zamani??? je mazingira muishio uswahilini au??

Anasoma hizi shule za akademia............... Siishi uswahilini ki-hivyo
 
Hata kama ni KIPAJI MAALUM naona sasa kinavuka mipaka!
Kama anajua mambo ya ndani ya Uzazi wa Mpango kwa kiasi hicho, hiyo inaleta tishio ndani!
Vipi akili zake za upstairs/academics zipoje?...isije kuwa ni expert wa kudaka mazungumzo yanayoongelewa zaidi na wenzie au walimu yanayohusu maeneo hayo nyeti!
Ubishi mno kwa mtoto si dalili njema, naamini mama yake hafurahishwi kabisa na viroja hivyo!
Endelea kumchunguza ili hatimaye ujue whether tabia hiyo ina positives kwa makuzi na future yake!
 
Anasoma hizi shule za akademia............... Siishi uswahilini ki-hivyo

kabla ya haya mabadiliko mlikuwa mna tabia ya kukaa nae na kuongea au kumweleza mambo ya maisha au maadili??
 
Mmm watoto ndio walivyo wanawaamini na kuwasikiliza sana walimu wao kuliko kawaida.Mimi wangu hata nikimfundisha hesabu kwa njia rahisi ninayoijua mimi ataikataa kisa tu ni mwalimu hakumfundisha hivyo.
 
tatizo liko kwetu wazazi hatuna muda wa kukaa na watoto hata kuongea nao (ukaribu) kiasi kwamba malezi tunasaidiwa na walimu na majirani ... sisi tunajifanya busy na kazi
 
mtambuzi,kwanza nikupongeze kwa kuwa na binti mwenye akili sana na udadisi. Mungu amewapendelea sana. sio tu kwamba ana utayari wa kuongea anachokijua na kukiamini, lakini pia sio mvivu wa kukuthibitishia kuwa ana uhakika na anachokiongea. ulishawahi kufikiria advantage uliyonayo,kuwa mtoto huyu akikutana na fataki aliyeko sekondari majibu atakayoyapata kwake? ooh,nimempenda sana mwanao huyu!
tatzizo lako liko hapo kwenye bold! kwa dunia hii ya utandawazi,usipomuwahi mwanao kwa kumpa information sahihi,wakamuwahi waongo watamchakachua! kama ameleta kipeperushi kinachoonesha kama sindano ndo za uzazi wa mpango,ungefungua mtandao mkaangalia matumizi ya condom katika kuzuia mimba na ukimwi pia. akikuona una information sahihi ataanza kukuamini na kuja kwako kwa ajili ya kuthibitisha. fanya kujifunza kwake kuwa fun na mjifunze pamoja. narudia,huwezi kumzuia kujua mambo kwa sababu ya umri wake. mpe mafundisho yote,akiongea ukimwi mpe za magonjwa mengine ya zinaa na hepatitis. hata wakati ana tatizo atakuja mjadiliane jinsi ya kulitatua

Haikuishi hapo, siku iliyofuata alinijia na vipeperushi viwili, kimoja kinachoelezea njia mbalimbali za uzazi wa mpango na kingine kilikuwa kikielezea juu ya maambukizi ya Ukimwi, pamoja na kinga zake, na alikuwa anataka kuthibitisha kile alichokuwa akikisema siku iliyopita.

Nilijaribu kumuelewesha kwamba, mambo hayo sio wakati wake kujifunza kulingana na umri wake, nilimshauri asubiri akiwa mkubwa atajifunza mambo hayo kwa undani. Lakini alizidi kusisitiza kwamba anataka kunithibitishia kwamba jana alikuwa sahihi. Ilibidi nikubali kuwa alikuwa sahihi ili kuepuka malumbano.
Hebu nisaidieni nimfanyeje binti huyu…………………………?
 
mtambuzi,kwanza nikupongeze kwa kuwa na binti mwenye akili sana na udadisi. Mungu amewapendelea sana. sio tu kwamba ana utayari wa kuongea anachokijua na kukiamini, lakini pia sio mvivu wa kukuthibitishia kuwa ana uhakika na anachokiongea. ulishawahi kufikiria advantage uliyonayo,kuwa mtoto huyu akikutana na fataki aliyeko sekondari majibu atakayoyapata kwake? ooh,nimempenda sana mwanao huyu!
tatzizo lako liko hapo kwenye bold! kwa dunia hii ya utandawazi,usipomuwahi mwanao kwa kumpa information sahihi,wakamuwahi waongo watamchakachua! kama ameleta kipeperushi kinachoonesha kama sindano ndo za uzazi wa mpango,ungefungua mtandao mkaangalia matumizi ya condom katika kuzuia mimba na ukimwi pia. akikuona una information sahihi ataanza kukuamini na kuja kwako kwa ajili ya kuthibitisha. fanya kujifunza kwake kuwa fun na mjifunze pamoja. narudia,huwezi kumzuia kujua mambo kwa sababu ya umri wake. mpe mafundisho yote,akiongea ukimwi mpe za magonjwa mengine ya zinaa na hepatitis. hata wakati ana tatizo atakuja mjadiliane jinsi ya kulitatua

tatizo hatupendi kuongea na watoto wetu wakuja kutaka ufahamu tunawaona wamekuwa wahuni sasa unataka awe gizani hadi lini???
 
Mwanao ana mapepo. Ni vyema mtoto akuzwe kwa namna ya kuhofu mamlaka na Mungu pia. Maandiko yanasema mlee mtoto njia impasayo naye hatoiacha hata atakapokuwa mtu mzima.
 
Omba tu asije kukushushua mbele za wageni.mana huyo mtoto anaonekana hachuji maneno wala hachagui kipi aongee na wenzake,kipi aongee na wazazi.
 
Ahsante mkuu, lakini ningependa abadilike kidogo, yuko too much aggressive akim-critisize mtu huwa anatumia logic hata zisizo za kweli ili mradi ku-justify msimamo wake.....................yuko kama mwanasheria, kama kuna jambo ulilihukumu kwa kwa namna fulani halafu siku nyingine ukafanya tofauti, atauliza sababu............. halafu ana kumbukumbu kitu cha ajabu.....................

Mkuu acha awe aggresive hivo hivo kwa maoni yangu ya dhati kabisa naona si mbaya, ni kitu kitachomsaidia sana kimasomo darasani. Kwa experience yangu watoto wa namna hiyo huperfom vizuri sana kielimu
 
Watoto wa namna hiyo wanazidi kuongezeka sana kwenye dunia ya sasa, na ni tatizo kwa wazazi...manake tungetegemea watoto wetu wawe na tabia kama zile tulizolelewa nazo na kuwa na mipaka kwa kile wanachozungumza na namna wanavyozungumza. Anahitaji kuwa na mipaka, manake atashindwa kuishi na watu wengine. Wewe kama mzazi waweza muelewa na mkubali kama alivyo lakini jamii yenye matarajio ya tofauti kwa mtoto itampa shida. Mfundishe kuwa na mipaka na kuheshimu/kukubali mawazo ya watu wengine bila ubishi na hasa wale walio wakubwa kwake. Atabadilika tu.
 
lol! umenifurahisha mpendwa. wanawake smart namna hii, akina nyamayao wa kesho huwa hata ku-date mfumo dume hawawezi.inaishia date ya kwanza,lol! amkazanie tu kusoma ili akutane na civilised mwenzie!
Wasiwasi wangu akiendelea hivyo halafu akaolewa na mfuasi wa mfumo dume sijui kama wataelewana. Sema naye taratibu ataelewa
 
Back
Top Bottom