Elections 2010 jamani huu si uchakachuaji wa sauri ya wapiga kura?

Mtu Mmoja

JF-Expert Member
Mar 18, 2010
593
64
hili suala la wabunge wa viti maalum binafsi linanichanganya. CCM chadema na cuf wanafurahia kupata wabunge hawa japo wanajua fika wamechaguliwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo (kuwa na uke).

wabunhe hawa sio siri wameichakachua sauti ya wananchi (demokrasia) ndani ya vyama hivi kwa kiwango kikubwa sana. hapa nitatoa mfano wa uchakachuaji kama ulivyo kwa chadema.

katika uchaguzi uliomalizika hivi punde, chadema ilipata wabunge 22 (wanaume 21 na mwanauke 1) wa kuchaguliwa majimboni, viti maalum ikapata 23 na nasikia wataongezewa viwili hivyo watakuwa na 25 (wote wanauke)!

!. hapa tunachakachua demokrasia au tunaimarisha?
2. hivi umaalum wa hawa wenzetu unatokana na nini?
3. kubagua watu kwa misisngi ya jinsia na kuwapa vyeo si kinyume cha katiba?
4. hawa wabunge wanamwakilisha nani officially huko dodoma kama kila jimbo lina mbunge wake?
 
ndugu, suala hili liliwahi kushikiwa bango na mpiganaji sofia simba kuwa lilipobuniwa lilikusudiwa kuwa la muda tu ili kupromote hali ya wanawake kujiamini na kukubalika na kuchaguliwa ktk jamii.............. ishu inakuja pale watu kama maua daftari ambaye ni mmoja wa wakongwe wa siasa naye hataki kwenda jimboni kugombea anasubiri viti maalum.......... au mkongwe kama anna abdalaha alitangaza kungatuka siasa, naye unamwona ndani ya viti maalum!........... hapo ndipo viti maalum vinapopoteza maana iliyokusudiwa..........

hilo la ubaguzi kuwa kinyume cha katiba, nadhani kimsingi uko sawa, ila kumbuka tena kuwa ndani ya hiyo hiyo katiba ndimo vilumoanzishwa hivyo viti maalum............. sasa affirmative action ikotokea kuwa imesimikwa nadani ya katiba na ikapingana na katiba yenyewe, hapo sijui ligi itakuwaje........... labda wataalamu wa katiba waje watusaidie mawazo...............
 
Hii ni hoja ya msingi kabisa.
Na hata wabunge hao wa viti maalumu huwa mara nyingi sio wakali ni kama mbwa asiye na meno kwani origin yake ni kubebwa so hawezi kuthubutu kuwa against na hoja za waliomteua.
 
haya sasa ndo mambo ya kupigia kelele nchi hii. tena ni ubaguzi mbaya saa unaotumia TUPU zetu kama kigezo! hata enzi za ukaburu hawakudiriki kutumia UKE kama sifa ya kwa kiongozi!
 
Eneo la kufanyika kazi demokrasia hapo. ni muhimu kuangalia upya hizi nafasi na vigezo kama ikibidi
 
Back
Top Bottom