Jamani,Huku si kuchochea vurugu:DC atuhumiwa kushusha bendera!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani,Huku si kuchochea vurugu:DC atuhumiwa kushusha bendera!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sijui nini, Oct 9, 2010.

 1. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  VYAMA vya CUF na CHADEMA, wilayani Pangani, mkoa wa Tanga, vimemlalamikia Mkuu wa Wilaya hiyo, Zipora Pangani, kwa kitendo chake cha kushusha bendera ya vyama vyao bila sababu za msingi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima, jana kwa njia ya simu, walisema walishangazwa na kitendo hicho kwani hakikuwatendea haki hasa wakati huu wa kampeni.
  Katibu wa Wilaya CUF, Kitwana Sefu, alisema DC Zipora, alifanya hivyo kwa lengo maalumu ili kumuonyesha mgombea mwenza wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Gharib Bilal, alipopita juzi katika eneo la Bweni kuwa hakuna upinzani.
  Alisema pamoja na kujaribu kuwachokoza wana CUF, bado wanaamini hawatakubali kuchokozeka ila wataonyesha kuwa upinzani katika wilaya hiyo upo na utafanya vema.
  Naye Mkuu wa Wilaya huyo, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alikiri kuwaagiza bendera hiyo ishushwe kutokana na kitendo cha kupandisha mabango.
  Mbali ya CUF, DC Pangani alisema bendera ya CHADEMA ilionekana iko katika maeneo ya ofisi za serikali, ambapo haparuhusiwi kuwepo bendera kisheria.
  Naye mgombea wa CHADEMA, Mzee, alisema kweli alikutana na mkuu wa wilaya na wamekubaliana kila mmoja, achukue jukumu la kuepusha vyanzo vyote vya uvunjifu wa amani ili zoezi hili la uchaguzi liweze kufanikiwa.
   
 2. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Au ndo kuwatafutia JWTZ sababu ya kuonekana wapinzania wana fujo wakati wa uchaguzi???
   
 3. W

  We know next JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nina hamu sana ya kuja kuona jinsi historia itakavyo wahukumu watu!
   
Loading...