Jamani Housegirl wangu Huyu, Ananitafuta ubaya! (STRICTLY KWA WANAUME TU)

dah so tatizo ni wife kujua? Je kama ungehakikishiwa kuwa hatajua inakuwaje hapo!
 
Piga mpodo kaka acha kuremba hao mi ndo huwa natakaga sama hao wanaojileta ebo...
 
Sijafanya bado ila mambo yanavyokwenda nona umuhimu wa kuweka mikakati ya kutoanguka katika jaribu hili. Samahani wewe ni mwanaume au mwanamke?
Mkuu, nani alimleta huyu mfanyakazi? Wewe ay wife?
 
Ikimbie zinaa na muombe mungu akusamehe kwa kuwaza kutaka kuisaliti ndoa!
Ukithubutu kuisikia sauti hiyo ya ushawishi ya shetani inayokujia ndani yako na ukafanya uasi huo, basi ujue utakuwa umeweka gape kubwa sana kati yako na mkeo iwe amejua au hata kama hatajua
 
Inavyoonekana tayari ushamtamani na akiendelea kuwepo maeneo ya hapo ipo siku utammega badilika kifikra acha kumfikiria kimapenzi mfikirie kama mdogo wako wa kike halafu utaona mabadiliko.linda heshima ya nyumba kumbuka baba ndo nguzo ya familia itapotetereka wanaoitegemea ndio victims.
 
Sijafanya bado ila mambo yanavyokwenda nona umuhimu wa kuweka mikakati ya kutoanguka katika jaribu hili. Samahani wewe ni mwanaume au mwanamke?

Wanawake wako wengi sana mtaani huko kama unataka ''kupoza njaa''. Huyo housegirl mission yake kwako si tu kufanya ngono zembe na wewe la hasha. Maelezo yako yanaonyesha amepania kabisa kumpindua mama mwenye nyumba. Kumbuka kama aliweza kufika kidato cha nne kijijini tayari ana mwamko kuhusu maisha mazuri na pengine anaona kabisa hii ndio nafasi ya yeye kupata mwanaume wa kubadilisha maisha yake, bila kujali madhara yatayojitokeza kwenye ndoa yako!

She is going to destroy your marriage and family. Chukua hatua sasa, muachisheni kazi! Full stop!....Maamuzi magumu hayo kaka unatakiwa kufanya, kumuachisha mtu kazi bila kosa lolote....Kazi ni kwako!
 
Hii ni kwa wanaume tu pleeaseeeee! but mchango wako nimeuchukua ingawa umevunja masharti

Asante kwa kuuchukua Gugwe, mkuu hilo ni jina tu. By the way hakuna mwanaume yeyote mwenye busara anaweza kuku- support kama unamatamanio na h.girl wako.
 
Huyo binti amepimwa?. Siku wife hayuko na mkabaki peke yenu, akaja na khanga moja, si utazini naye. Solution mtimue mapema ama sivyo ndoa yako iko au itakuwa mashakani.
 
mkuu mbona ni jambo la kawaida tu,kama una chance mpelekee moto,hamna shida mkuu,inawezekana huyo house girl mnamnyima chance ya kutoka kwenda kupata service,muhudumie kiaina mkuu,msaidie mtoto wa watu
 
Mkuu huo mtego ni mkali sana yakupasa uushinde,haina haja ya kkukorofishana na mkeo,haina haja ya kumfukuza binti wa watu kwa ajili ya uzuri wake,simama wewe kama wewe na heshima yako ya baba mwenye nyumba na bosi nayo itasimama,kimsingi inavyoonekana n wewe umeshaanza kummezea mate.Acha mara moja,badili mwelekeo,jiweke naye mbali,utashinda!Penda kuwa na mkeo mda wote,atakuheshimu
 
Thanks mkuu nitajaribu

Eti utajaribu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
kwa leo mi mwanaume
 
mkuu mbona ni jambo la kawaida tu,kama una chance mpelekee moto,hamna shida mkuu,inawezekana huyo house girl mnamnyima chance ya kutoka kwenda kupata service,muhudumie kiaina mkuu,msaidie mtoto wa watu

Mkuu una ndoa
Jua jamaa ana familia ya watoto wanne
Likimfikia la kumfikia kwa mkewe kwa sababu ya tamaa ya kulala na house gal huoni familia ishasambaratika hapo
 
endelea kuheshimu ndoa yako kaka na familia yako
Jamani naomba ushauri kuhusu hili.

Mimi ni mume wa mke mmoja na watoto wanne. Hivi karibuni tumepata housegirl mpya kutoka Singida, amemaliza form four hakubahatika kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa sifa za shule za serikali. Ni mzuri wa kawaida, yaani hana muonekano ule wa mahousegirl-naamaanisha muonekano choka mbaya kweli anafaa hata kuwa mke wa mtu. Katika historia yangu sijawahi hata siku moja kutembea na housegirl na mpaka sasa nishaajiri hao h/girl si chini ya 6, huwa niko very serious na sitaki mazoea nao hata kidogo.

Huyu amekuja naona anataka kuniangusha katika msimamo wangu huu. siku ya kwanza kutambulishwa kwake alionekana kushituka sana ingawa na mimi kwa ndani nilimkubali kuwa mzuri. Maisha yakaendelea na siku zikafunguka. Sasa toka siku hiyo amekuwa anakosa sana sana tu confidence ninapokuwa nyumbani, mara atajikwaa, mara ataogopa kuja mbele yangu n.k mbaya zaidi ninapokuwa peke yangu lets say wengine wapo mbali ananichangamkia sana na kutabasamu muda wote kila nitakalooongee yeye anatabasamu hata kama si la kufurahisha, nikimtuma kitu ataniletea wakati napokea anainua kichwa kuniangalia kiuchokozi halafu anatabasamu, basi na mimi nikawa natabasamu. Ikitokea labda nimerudi nyumbani na nahitaji chakula mapema atanipikia vizuri sana wakati mwingine anongeza kitu ambacho hakikupangwa kwenye ratiba ya chakula cha siku hiyo, anaweza kunkaangia mayai au akachemsha chai ya maziwa akaweka na viuongo haraka haraka na kunipatia chakula.

Tatizo, wife keshamshitukia hizo nyendo zake, amekuwa kila mara ananiuliza kuhusu mtu huyu, anasema mbona fulani ukiwepo anakuwa hana confidence nikamwambia mi sijui embu muulize alipomuuliza akamjibu wife kuwa eti ananiogopa kwa sababu aliambiwa na mlinzi mi ni mkali sana achunge asinikorofishe. Lakini ukiangalia mapozi yake kwangu si ya mtu anayemuogopa. Si hizi ameongeza zaidi, kunisalimia/kuniamkia kwake imekuwa ngumu sana ni mara mojax2 sana. Mi kwa ujumla ni mtu nisiyejali vitu vidogo vidogo na nilichojaribu kufanya ni kuwa mbali nae, nimeongeza kuwa serious, na wakatui mwingine nakuwa mkali ninapoongea nae ili awe mbali nami au afute hicho anachofikiri au kukitafuta, Lakini nahisi ananitafuta ubayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

Nimfanyeje? au nifenye lakini nahisi kujidhalilisha kwa mah/girl!
 
Kaka dhambi ina tabia ya kuishi sirini mwite mbele ya mkeo kukiwa na mtu mzima mkanye live za uso ukiona ngumu mrudishe kwao ukimchana mkeo atakupenda zaidi na kukuheshimu
 
Kaka dhambi ina tabia ya kuishi sirini mwite mbele ya mkeo kukiwa na mtu mzima mkanye live za uso ukiona ngumu mrudishe kwao ukimchana mkeo atakupenda zaidi na kukuheshimu

Thanks mkuu nimeipenda hii
 
Back
Top Bottom