STUNTER
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 13,077
- 17,208
Ebhana kuna uchunguzi wa kimya kimya nimeufanya na nimegundua mengi sana kuhusu hizi pesa za wahindi hasahasa kwenye masuala ya mikopo.
Inaweza isiwe ishu saana ila kuna mambo nimejiuliza ambayo nataka tushirikiane katika kupata majibu ya maswali hayo...
1.Hivi ni kwanini wale washiriki(wakopaji wa mikopo) huwa hawaruhisiwi kukaa kwenye viti pindi muhindi akiwasili kwenye ivo vikundi?
2. Tunafahamu kwamba wezi, majambazi na vibaka huwa hawachezi mbali na sehemu zenye mifereji ya hela, yaani mabenki yamelizwa sana lakini sijawahi kusikia muhindi anayetoa mikopo amevamiwa au wale mawakala wao wamevamiwa na kuporwa hela
3. Kuna nyakati wale washiriki kabla ya kuanza vikao vya marejesho ya mkopo, huwa wanaambiwa wasome maagano(maranyingi yanakuwa nyuma ya kitabu cha marejesho) Je, hiyo ina maana gani?
4.Kwanini wale mawakala na wafanyakazi wa muhindi hawaruhusiwi kuchukua mkopo?
5. Tukirudi kwenye masuala ya ulinzi, yaani kwenye ofisi za hawa wahindi hakuna hata security inayoeleweka, utakuta kuna vijizee vilivyojichokea eti ndo wanawaweka wawalindie mamilioni, wtf muda mwingine unakuta hawana hata silaha, sasa unajiuliza hawa wahindi wanajiamini nini hasa???
6. Alafu kitu kingine, sijawahi kusikia mtu amezipoteza hela za mkopo(kutoka kwa muhindi)
Yaani hata kwa kukabwa tu sijasikia, Unakuta mtu anazitumia hela kwa ukamilifu kabisa pasipo upotevu wowote..
7. Na kingine unakuta mtu akishazipata zile hela basi anaanza kujutia wakati wa kuanza mirejesho ya mikopo, na wengi unakuta maisha yao ndio yanazidi kudidimia kabisaa,
kisha unakuta wengine ndio wanajuta kabisa huku wakila viapo kwamba mkopo huu ukiisha basi hatochukua mwingine tena,
chaajabu unakuta mkopo ukiisha anasahau adha zote na kujikuta anauchukua mwingine tena mkubwa kuliko ule wa mwanzo...
8. Ukitaka kushangaa zaidi basi fika kwenye ofisi zao, kwanza nyingi ziko uchochoroni alafu hazina quality nzuri yani kiufupi hazifananii kama eti ndio nyumba watu wanakohifadhi pesa pamoja na kuchukua...
-
Yapo mambo mengi sana na wengine watayaweka ila nahitaji tujadiliane hayo kwanza,
KARIBUNI