Jamani hivi ni vitu vya ajabu au mimi ndio sielewi?

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
12,777
2,000
Ebhana kuna uchunguzi wa kimya kimya nimeufanya na nimegundua mengi sana kuhusu hizi pesa za wahindi hasahasa kwenye masuala ya mikopo.
Inaweza isiwe ishu saana ila kuna mambo nimejiuliza ambayo nataka tushirikiane katika kupata majibu ya maswali hayo...

1.Hivi ni kwanini wale washiriki(wakopaji wa mikopo) huwa hawaruhisiwi kukaa kwenye viti pindi muhindi akiwasili kwenye ivo vikundi?

2. Tunafahamu kwamba wezi, majambazi na vibaka huwa hawachezi mbali na sehemu zenye mifereji ya hela, yaani mabenki yamelizwa sana lakini sijawahi kusikia muhindi anayetoa mikopo amevamiwa au wale mawakala wao wamevamiwa na kuporwa hela

3. Kuna nyakati wale washiriki kabla ya kuanza vikao vya marejesho ya mkopo, huwa wanaambiwa wasome maagano(maranyingi yanakuwa nyuma ya kitabu cha marejesho) Je, hiyo ina maana gani?

4.Kwanini wale mawakala na wafanyakazi wa muhindi hawaruhusiwi kuchukua mkopo?

5. Tukirudi kwenye masuala ya ulinzi, yaani kwenye ofisi za hawa wahindi hakuna hata security inayoeleweka, utakuta kuna vijizee vilivyojichokea eti ndo wanawaweka wawalindie mamilioni, wtf muda mwingine unakuta hawana hata silaha, sasa unajiuliza hawa wahindi wanajiamini nini hasa???

6. Alafu kitu kingine, sijawahi kusikia mtu amezipoteza hela za mkopo(kutoka kwa muhindi)
Yaani hata kwa kukabwa tu sijasikia, Unakuta mtu anazitumia hela kwa ukamilifu kabisa pasipo upotevu wowote..

7. Na kingine unakuta mtu akishazipata zile hela basi anaanza kujutia wakati wa kuanza mirejesho ya mikopo, na wengi unakuta maisha yao ndio yanazidi kudidimia kabisaa,
kisha unakuta wengine ndio wanajuta kabisa huku wakila viapo kwamba mkopo huu ukiisha basi hatochukua mwingine tena,
chaajabu unakuta mkopo ukiisha anasahau adha zote na kujikuta anauchukua mwingine tena mkubwa kuliko ule wa mwanzo...
8. Ukitaka kushangaa zaidi basi fika kwenye ofisi zao, kwanza nyingi ziko uchochoroni alafu hazina quality nzuri yani kiufupi hazifananii kama eti ndio nyumba watu wanakohifadhi pesa pamoja na kuchukua...
-
Yapo mambo mengi sana na wengine watayaweka ila nahitaji tujadiliane hayo kwanza,
KARIBUNI
STUNTER
 
Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,245
2,000
Nina jamaa yangu anafanya kwenye kampuni ya wahindi anadai wakipewa mshahara zile pesa zinanuka UDI..bado wanachukulia dirishani..kwahyo Mkuu usishangae hawa wala pilipili ndio zao
 
Queen of Sheba

JF-Expert Member
Feb 5, 2016
735
1,000
Ukitaka usiendelee kopa kwa wahindi, kila leo utakua wakurejesha tu na hapo huoni hata hyo hela umefanyia nini cha maana. wanachozifanyia hela zao wanakijua wenyewe.
 
STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
12,777
2,000
Nina jamaa yangu anafanya kwenye kampuni ya wahindi anadai wakipewa mshahara zile pesa zinanuka UDI..bado wanachukulia dirishani..kwahyo Mkuu usishangae hawa wala pilipili ndio zao
Wacha tumuite swahiba wetu Jambazi ili atuambie chochote
 
The Technologist

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
640
1,000
1. Sio kanuni kwamba ukiwa na hela lazima uvamiwe na majambazi! Nenda migodini ukaone vile watu wanavyokaa na hela mingi tena ndani ya kambi za maturubai!

Mara nyingi kuibiwa ni matokeo ya lifestyle ya mhusika.

7. Kama mtu amerejesha mkopo na kuchukua mwingine mkubwa zaidi ina maana kwa kiwango kikubwa alifanikisha mradi wake - tatizo li wapi?
 
STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
12,777
2,000
Ukitaka usiendelee kopa kwa wahindi, kila leo utakua wakurejesha tu na hapo huoni hata hyo hela umefanyia nini cha maana. wanachozifanyia hela zao wanakijua wenyewe.
Nawashuhudia baadhi ya jamaa na marafiki wakiendelea kukongoroka kutokana na mkopo wa muhindi na inakuwa kama hauwafaidishi.
Labda humu jf atajitokeza aliyenufaika.. Maybe
 
STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
12,777
2,000
1. Sio kanuni kwamba ukiwa na hela lazima uvamiwe na majambazi! Nenda migodini ukaone vile watu wanavyokaa na hela mingi tena ndani ya kambi za maturubai!

Mara nyingi kuibiwa ni matokeo ya lifestyle ya mhusika.

7. Kama mtu amerejesha mkopo na kuchukua mwingine mkubwa zaidi ina maana kwa kiwango kikubwa alifanikisha mradi wake - tatizo li wapi?
Tatizo vile wanavyosuasua mpaka wengine utakuta wananifuata niwakopeshe ili wakalipe mkopo(unaona mkanganyiko ulipo?) mpaka naamua kuwasaidia tu.
Ishu inakuja kama wanaweza kujitahidi kurejesha rejesho kila wik(japo kwa kusuasua)
kwanini baada ya mkopo kuisha wasiendelee utaratibu wa kujiwekea kima/kiwango sawa na kile walichokuwa wapeleke kwenye mkopo, na baada ya muda zile hela wakazitumia kwenye hayo malengo yao mengine?? Why why
 
Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,155
2,000
Waogope sana wahindi kwenye suala la pesa. Kuna siku nilifanya biashara moja na wahindi,tukaenda kuchukua pesa benki.

Jambo la kushangaza zile pesa nililetewa na mzee mmoja ambae alikua kavaa ovyo ovyo wakati hiyo benki ina wahudumu nadhifu.
 
The same thing kwenye mikopo yao, maranyingi unakuta kuna kijizee kilichokuwa rafu rafu ambaye ndo unakuta ni mlinzi ama manager...
 
sergio 5

JF-Expert Member
May 22, 2017
8,704
2,000
Wanavamiwa sana ila hawasemi tu
Conclusively ww point yako ni uchawa huna lolote
 
Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,995
2,000
Siku hizi huwa naziheshimu thread zako, Mara baada ya kuzifamyia kazi nikaona zina work hasa zile za jukwaa la mambo yetu ya 6*6. Natumiaga triek zako kukamata warembo nimekuwa fundi mnooo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom