Jamani hivi kwa nini baadhi ya wanyama hawamuogopi mwanamke??

Hi ya beberu kuchomoa uume wake akimuona mwanamke . Mmmh ni kali sana. Ina maana akuzubaa anaweza akamdu?
 
Kama wakristo tunao amini historia ya uumbaji wanyama wote walitangulia kuumbwa then akaja mwanadamu wa jinsia ya kiume yaani adamu. Na mungu alimkabidhi mamlaka na nguvu ya kuvitawala vyote viijazavyo dunia akiwa pekee yake yaani adamu pekee mkewe alikuwa bado kuumbwa so amekuja kuumbwa wanyama wote wakijua adam ndo boss wao waliyeambiwa wa mtii huyo mwengine wanamchukulia kama kale ka usemi eti mjakazi wa mfalme ni mfalme akiwa na wajakazi wenzie
 
Nimewahigi kusikia ila ni kuhusu Ngedere...maana huku nilipo

Ngedere ni wengi sana ila sijui connection iko wapi

Umeshamaliza chuo na bado unaishi msewe?? achiaga wenzako banah..

Any way pale UDSM huwa tunashuhudia madem pale CoET wanavyonyanyaswa na ngedere wakati wa kula...huwa wanadiriki hata kuwatishia ili wakimbie wawaachie msosi
 
kenya ni mfano hai japo siwezi kusemea kwa ujumla! kuna kipindi nyani walikuwa wakiwaonea sana wanawake kwa kuwapiga. lakini endapo mtu mwanaume akiwepo hata kama ni mtoto wa miaka mitano, nyani hao walikuwa wakikimbia!!

hiyo ni reference ndogo!

lakini pia, kwa sisi wakulima, kama mnavyojua, tunasumbuliwa sana na nyani, tumbili na ngedele, endapo mwanamke ataenda kulinda shamba lisishambuliwe na hawa viumbe, basi siku hiyo itakuwa ni shida tupu! atahangaishwa mpaka akome...! hii nahisi hata wao wanatambua kwamba yule ni mwanamke, japo sina uhakika na hili kwa sababu sijaanya research ya kutosha!! .... lakini endapo mtoto yeyote tu wa kiume wa miaka hata kumi akienda shamba kulinda, ana uwezo wa kufukuza hata nyani zaidi ya 40 peke yake bila bughudha!!

reference nyingine, kwa wale wenzangu na mimi tunaotokea vijijini hasa watoto wa wakulima, tutatambua hili! ng'ombe wa kulimia huwa wana dharau sana kwa wanawake!! yani ng'ombe wakati mwingine anaweza akasimama na hata kumtishia pembe yake!! ile amri ambayo hupewa ng'ombe kwa mfano, kusimama ili afunguliwe kamba... ni mara chache sana kutiliwa maanani na mwanamke, mara chache sana!
kiumbe kama mbwa, yuko radhi wakati mwingine hata AMNG'ATE mwanamke lakini si kuamrishwa kutoka nje (sometimes)!! binafsi mimi nimefuga sana hawa viumbe... mbwa mwindaji hapelekeshwi hivi hivi wana jf! labda mwana mama nae awe mwindaji na awe anamtumia huyo mbwa!! la sivyo, utegemee resistence kutoka kwa yule mbwa!!

Viumbe hawa wanaishi kwa kutambua sauti, hasa zenye amri!! mwanaume ana sauti ya kipekee!! uzito wa sauti yenyewe .. amri nzito kama mnavyojua!!

kwa upeo wangu... hizi ni factor chache ambazo ninazifahamu kwanini wanawake inafikia hatua wanadindiwa na hawa viumbe!
 
no research no right to say. kwa cc tulio kulia vijijini kuchunga ng'ombe na hata kukutana nyani hii ni habari ya kweli. hata mwanamke akikutana na nyani, nyani hawaondoki njiani mwanamke anaweza kulazimika kuahirisha safari au mpaka ampate mwanaume wa kumvusha. ukweli ndio huo.[/QUOTE]

Na kama mwanaume ni shoga a.k.a bwabwa, limesuka nywele, limevaa hereni, linajishembendua.......je nyani wanatambua ama ?
 
DUU UMENIKUMBUSHA KIJIJINI MASHAMBANI! MWANAMKE AKIKUTA JAMII YA NYANI SHAMBANI HATA KAMA ANGEPIGA MAWE HAWATOKI ZAIDI WANAZIDI KUMSOGELEA! Naamini wanaweza kututofautisha na wanatambua mwanamke ni dhaifu kabisa! Na huu ndo ukweli hata tuseme haki sawa mwanamke daima ni dhaifu - kimwonekano (maumbo), kivitendo n.k hii ndo sababu ya wanyama hawa kuwaona kuwa wadhaifu! Maana hata kama anafukuza hasogelei na hawi na ukakamavu! Mbona wanajeshi wa kike wanyama hawawafanyii hivyo? Wanyama wana tabia ya kutusoma hata miondoko! Jaribu ubadili miondoko, Sauti na ukakavu viwe sawa na mwanamke halafu sogelea jamii ya wanyama hawa: Nyani, Ngedere, Sokwe na beberu uone utofauti!
 
Back
Top Bottom