Jamani! Hivi George Galloway ni mtu wa aina gani?

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
George Galloway anapatikana kwenye TV moja ya Iran inayoitwa Press TV. Anachambua siasa za kimataifa.Anaweka mada mfano Libya,au Somalia n.k. unaruhusiwa kupiga simu (reverse call) unatoa mchango wako naye anafafanua.Nauliza wanazuoni wa humu JF mnauonaje weledi wake?
 
Mrdash1

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,378
331
George Galloway anapatikana kwenye TV moja ya Iran inayoitwa Press TV. Anachambua siasa za kimataifa.Anaweka mada mfano Libya,au Somalia n.k. unaruhusiwa kupiga simu (reverse call) unatoa mchango wako naye anafafanua.Nauliza wanazuoni wa humu JF mnauonaje weledi wake?

Usiumize kichwa......
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
13,627
23,345
George Galloway ni mtu mpenda sifa anayejua jinsi ya kula hela za waarabu kwa kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Nakumbuka alipokuwa mbunge huko kwao UK alipata kumtetea Sadam wakati Blair alishaamua Sadam apewe kichapo. Baada ya kuonekana misimamo yake ni ya kigaidi wapiga kura wake walimtosa. Ila ni mpambananji asiyechoka huyu jamaa
 
trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
George Galloway ni mtu mpenda sifa anayejua jinsi ya kula hela za waarabu kwa kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Nakumbuka alipokuwa mbunge huko kwao UK alipata kumtetea Sadam wakati Blair alishaamua Sadam apewe kichapo. Baada ya kuonekana misimamo yake ni ya kigaidi wapiga kura wake walimto sa. Ila ni mpambananji asiyechoka huyu jamaa
Asante sana sikuwa najua alikuwa mbunge. Vp kuhusu imani yake? Ni muislamu na je wa imani kali?
 
tz1

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
2,124
523
Asante sana sikuwa najua alikuwa mbunge. Vp kuhusu imani yake? Ni muislamu na je wa imani kali?
Sithani kama ni mpenda sifa,mi naona ni msema kweli.Wakati wa vita ya sadam,tony blair alitumia gazeti la daily mail kuchapisha documents feki
wakidai zilikutwa nyumbani kwa sadam.Zikionyesha kwamba jamaa alikua kwenye pay roll ya sadam.jamaa akaonekana mbaya ndipo alipo shindwa seat kwenye ubunge.
Baada ya hapo akawapeleka dailymail mahakamani na akashinda kesi akalipwa hela nyingi sana kama sikosei ilikuwa zaidi ya pounds millioni moja
hela zote hizo alipeke iraq kusaidia watoto yatima.
Kuhusu dini yeye ni mkristo ila mke wake wa ndoa ya pili ni muislam.
Serikali ya uk inajaribu sana kumfunga mdomo.
 
Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,703
142
Nampenda sana Galloway, anawachachafya sana viongozi wa nchi za magharibu.
George Galloway ni mtu mpenda sifa anayejua jinsi ya kula hela za waarabu kwa kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Nakumbuka alipokuwa mbunge huko kwao UK alipata kumtetea Sadam wakati Blair alishaamua Sadam apewe kichapo. Baada ya kuonekana misimamo yake ni ya kigaidi wapiga kura wake walimtosa. Ila ni mpambananji asiyechoka huyu jamaa
 
  • Thanks
Reactions: tz1

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,703
142
Kwangu mimi ni mtu anayejua agenda chafu za viongozi wa nchi za magharibi.Kwa bahati nzuri kapata mouth piece ,Press TV, ambayo anaweza kuitumia to express his views. Anaujua ukweli tofauti na mavuvuzela ya vyombo vya habari vingi duniani kama BBC,CNN,Sky News,Aljazeera nk.
George Galloway anapatikana kwenye TV moja ya Iran inayoitwa Press TV. Anachambua siasa za kimataifa.Anaweka mada mfano Libya,au Somalia n.k. unaruhusiwa kupiga simu (reverse call) unatoa mchango wako naye anafafanua.Nauliza wanazuoni wa humu JF mnauonaje weledi wake?
 
trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
722
Asante sana tz1.. Ila wapiga simu wengi humpa Asalaam Aleykum! Naye anaitikia Aleykum Salaam.Wakimwambia Eid Mubarak anaitikia Thank you!
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,709
8,802
Asante sana tz1.. Ila wapiga simu wengi humpa Asalaam Aleykum! Naye anaitikia Aleykum Salaam.Wakimwambia Eid Mubarak anaitikia Thank you!

Ahaahhh mbona kawaida au na huyu ni Muislam?
attachment.php
 
tz1

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
2,124
523
Asante sana tz1.. Ila wapiga simu wengi humpa Asalaam Aleykum! Naye anaitikia Aleykum Salaam.Wakimwambia Eid Mubarak anaitikia Thank you!
Asalaam aleykum ni salaamu ya kawaida na siyo ya kidini.
 
IPECACUANHA

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
3,185
1,867
Asante sana sikuwa najua alikuwa mbunge. Vp kuhusu imani yake? Ni muislamu na je wa imani kali?
Mara ya mwisho nilimuona kwenye Bigbrother UK pamoja na Rodman. He won a parliamentary seat kwa kura za waislamu wapakistani kwasababu alipinga vita ya Irak. Alikua na tuhuma ya kupewa hongo ya mapipa ya mafuta na Sadam Husein
 
Ilongailunga

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
1,388
888
Galloway ni mbunge kupitia chama kidogo cha Respect, ni mpinzani mkubwa wa dola za kifalme za kiarabu(petro-monarchies)
 
RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,863
2,744
Wako wachambuzi wengi sana wenye kujua game la mabeberu wa magharibi lakini tatizo ni powerful machines propaganda za western CNN, SKY, BBC, AL Jazeera ... wakisaidiwa na tawala za kifalme kwenye nchi za kiarabu. Inashangaza na kusikitisha kuona Saud Arabia imekaa kimya huku Wapalestina wanauawa mamia kwa maelfu kama siyo malaki... UN sijui wanafanyakazi gani na wako kwa maslahi ya nani huku wanadamu wasiokuwa na hatia wanauawa kila kukicha ...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom