Jamani hilo neno "mchakato" lisitumike ktk ofisi za serikari

ligendayika

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,183
198
kama unafuatilia maswala yoyotye katika ofisi za serikari ukipambana na neno hilo ujue hapo usumbufu na ucheleweshaji unaanza na linapelekea mianya ya kukosa uadilifu kwa watendaji wa serikari na mwishowe ni Rushwa. naomba tujadili wana JF mnaonaje.
 
siku hiz neno mchakato limekuwa la kujitetea kila kitu ukioji,unaambiwa tuko kwenye mchakato tena ilo neno muheshimiwa pinda na jk upenda sana kulitumia,linatumika kujitetea pale kiongoz anapishindwa kuwajibika
 
Kama utendaji wetu umegeuka kuwa wa maneno zaidi kuliko vitendo, hauwezi kuacha kulitumia neno hilo
 
Nikweli hili neno wakati mwingine hadi linaudhi! Nakumbuka kuna wakati nilikuwa nafuatilia barua yangu ya kikazi katika ofisi fulani ya serikali kila nikienda naambiwa barua yangu ipo katika" mchakato". Ile barua ilikuja kutoka baada ya miezi mitatu!
 
kuna haya maneno mawili ambayo watendaji wazembe katika idara zote wanayatumia mara kwa mara kuhalalisha uzembe wao,na ingekuwa amri yangu basi yangefutwa kwenye kamusi ya kiswahili na ni hilo la mchakato na changamoto.siyo kitu cha ajabu siku hizi ukifuatilia issue yoyote jibu utajibiwa kuwa hiyo ni changamoto na tuko kwenye mchakato wa kufuatilia na hata urudi mara kumi jibu ni hilo hilo.haya maneno mpaka miaka ya 1990s hayakuwepo kwenye kamusi ya kiswahili nahisi ujio wake una madhara makubwa kwa taifa letu!!!!
 
Mchakato maana yake ni "process' sasa lisipotumika neno hilo serikalini kitu gani kitaweza kutekelezeka bila ya mchakato.
Cha msingi na cha maana ni kuwa hiyo michakato iwe na time frame ambapo tunaweza kuuliza kulikoni iwapo muda umepita kabla ya utekelezaji
 
Mchakato maana yake ni "process' sasa lisipotumika neno hilo serikalini kitu gani kitaweza kutekelezeka bila ya mchakato.
Cha msingi na cha maana ni kuwa hiyo michakato iwe na time frame ambapo tunaweza kuuliza kulikoni iwapo muda umepita kabla ya utekelezaji

Tatizo linatokea hapo kwenye hilo neno procces procces haina mwisho mkuu anaweza kuwa hata miaka kumi
 
Back
Top Bottom