Jamani hii sukari!

Mtumishi Mkuu

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
259
92
Wakuu heshima yenu! Juzi jumamos nilishindwa kuamini masikio yangu pale shoprite mliman city. Huwa nina mazoea ya kununua baadhi ya bidhaa za nyumbani pale ikiwemo sukari. Cha kushangaza juzi nimeenda kama kawaida nikachukua pakiti 10 za sukari kila moja ikiwa ni 1 kg. Wakati ninaenda kulipia nikashangaa yule mhudumu ananiambia kuwa siruhusiwi kununua zaidi ya kilo 3 na hata waeweka matangazo. Nilishikwa butwaa ila ndio hivyo. Nadhani watanzania tunaelekea kubaya sasa.
 
Ina maana 1kg ni rahisi sana pale? Ikimaanisha kila Mtanzania afikae pale na aweze kumdu bei? Ama lengo lao ni nini baada ya majibishano humo ndani?
 
Hii nchi inafurahisha sana.....Mbona hawatafuti chanzo? Waalianza mafuta, sasa sukari, sijui kitafuata nini
 
Hii nchi inafurahisha sana.....Mbona hawatafuti chanzo? Waalianza mafuta, sasa sukari, sijui kitafuata nini

wenyewe wako bize kuomba ridhaa ya kuongoza nchi kuipeleka shimoni, suti za mwarabu zinatumaliza.
 
Ina maana 1kg ni rahisi sana pale? Ikimaanisha kila Mtanzania afikae pale na aweze kumdu bei? Ama lengo lao ni nini baada ya majibishano humo ndani?

Nikilinganisha na maduka ya mitaani huwa naona pale bei iko chini kidogo. Kwa mfano saiv sukari mtaani ni kati ya 2000 hadi 2500 wakati wao wanauza 1900!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom