Jamani hii story inaweza kutupa fundisho hasa wana ndoa - reference Mwanamke nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani hii story inaweza kutupa fundisho hasa wana ndoa - reference Mwanamke nyumba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by nyumba kubwa, Oct 24, 2011.

 1. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  mwenzio nacheka kwa uchungu, niliolewa mume wangu baada ya miaka sita ya ndoa yetu mume wangu akanitaarifu ya kwamba anataka kuoa mke wa pili, japo iliniuma sikushangaa sana kwani dini yetu inaruhusu kuoa wake hata wanne ikiwa tu utaomba ruhusa kwa mke wa kwanza naye akaridhia, basi kwakuwa mume wangu alisharidhia kuoa na kampata wa kumuoa sikuona kwanini nimkatalie nikamwambia amwambie tu huyu mkewe akija tuheshimiane na kila mtu ajuwe mipaka yake.  basi mume wangu yule akaanda harusi siku ikafika kweli akaoa, na siku ya harusi mke mwenzangu kweli alipendeza na kutunzwa zawadi tele, ndugu zake wa kitanga nakwambia wakajipamba taarabu zikapigwa lakini cha kushangaza taarabu zile kama zilikuwa zinanisema miye kwa mafumbo maana nyingi zilikuwa za kuhusu uke wenza, na mwanaume kwenda kwake nikaanza kuhisi kimchezo.  kwasababu ile harusi ya mume wangu nami na wakwe na ndugu wa mume wangu wote tulikuwa mstari wa mbele kuifanya ifane lakini wale ndugu wa mwanamke na yule aliyeolewa nikawa naona kama vile wameichukulia dili sana miye kuletewa mke mwenzangu yani kama vile sijui nini..  yule dada akagewa naye nyumba yake huko boko, maisha yakawa yanaendelea lakini kwa masimango akinisema vibaya kwa watu kwamba sifai wala simtimizii mume wangu ndio maana kaolewa yeye, kila nikipita kwa ndugu wa mume wangu napewa tu habari alizopeleka kuhusu mimi na kunisingizia vitu kibao, wakati miye nilikuwa namsalimia na kumjulia hali kila mara mume wangu akienda nikinunua chochote hata kanga namgea na yeye lakini yeye anilipiza kwa masimango na kunisema najipendekeza, wakati nilimruhusu mwenyewe mume wangu amuoe leo nasemwa kamfwata yeye sijui kutunza mume!!!!!!!!  wamekaa miaka miwili hivi yule dada hajashika mimba mpaka wakaanza kuzunguka kwa waganga, na madawa yote ya kienyeji yakamalizwa lakini wapi kumbe mwenzangu yule dada alikuwa anatumia dawa za majira ili asizae na mumewe hajui kumbe kawaida yake huwa anajiuza kwenye mahoteli makubwa na ndio huko alipokutania na mume wangu.  ikafika sasa mpaka nikaambiwa namloga ili asizae, akaanza kuniongelea vibaya mpaka kwa mume wangu, mume wangu na yeye kwa kupenda ya kuambiwa akanibadilikia kutwa akawa analala kwa mke mdogo kwangu kapasusa hela ya matumizi hanipi tena ananiambia nipewe na hao wanaume wangu yani vituko kibao na akaamua kuhamia kwa bimdogo.  ikabidi tena nitafute mtaji nianze kufanya biashara za hapa na pale namshukuru MOLA maisha yanaendelea, yule mume wangu ndio kaganda kwa mke mdogo hata kuja kusalimia wanae haji wala matumizi haleti.  yule mke mwenzangu yapo alikuwa na ndoa alikuwa anakutana na majamaa zake kwa siri, mwaka wa tatu MUNGU akamjalia akapata mimba, akaanza kwenda clinic na siku akatakiwa kupima ukimwi majibu yakaja amehathirika, akachanganyikiwa atafanyaje??? akawaeleza dada zake waliokuwa wanajuwa siri zake wakamwambia sasa kashaumbuka atafanya nini zaidi aje kuniona mimi aniambie nimpe ushauri.  akaja na dada zake watatu, nilishangaa nikajuwa anataka kuja kunifanyia vurugu, akanieleza kwa upole akitokwa na machozi kwa uchungu, nikaona kama mchezo wa kuigiza japo kanifanyia mengi mabaya na kunitia ubaya kwa watu nilimuonea huruma sana, ni ka mwambia sawa nitamsaidia na kumsaidia kwangu ni kwamba amueleze mumewe ukweli japo anaweza kupigwa na kuumizwa lakini atakuwa kashajuwa na yule baba akija huku miye nitamuelewesha kwamba asiwe na jazba.  mumewe aliporudi siku hiyo akamueleza mambo yote, kweli yule baba alipandwa na hasira sana sema akashindwa kumpiga kwasababu alikuwa mjamzito, kama tulivyojuwa mume wangu akaondoka na kuja kwangu kwasababu nilikuwa nimeshajuwa nikamruhusu tu kuingia ndani japo nami nina dukuduku langu.  baada ya kula na kuoga nikamuuliza vipi leo umekosea njia, ndio akaanza kuniomba msamaha akitokwa na machozi kisha akanihadithia yote, sikumjulisha kwamba nilikuwa najuwa, nilichomwambia ni kwanza omba wanao msamaha kisha asubuhi twende hospital tukapime maana wote tunaweza tukawa tumeambukizwa.  kesho yake tukaenda, tukapima kwakweli hatukuamini tulivyokuta wote wawili hatuna maabukizo, japo tulifurahi lakini hatukuamini, kwangu niliamini kwani mume wangu aliniacha na sikuwa na mtu mwengine tena ila yeye hakuamini kwani mkewe alikuwa nao halafu yeye hana hakuelewa kabisa, tukaambiwa tupime tena baada ya miezi mitatu, tukapima na kweli hatuna.  yule mke mwenzangu akajifungua mtoto ikawa bahati mbaya amefariki, ikabidi baada ya kupona mume wangu ampe talaka akarudi nyumbani na kunieleza jambo moja SITAKAA KUKUACHA TENA.  nimeandika leo ili kumshukuru MOLA wangu kwa kunirudishia familia yangu, na kuwapa moyo wanawake wote ndoa zao zenye matatizo kwamba MOLA ni mwema atamrekebisha mumeo kwa njia yake mwenyewe na kwa muda wake mwenyewe jipe moyo na endelea kuvumilia.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hongera zake!!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  unazitoa wapi hizi???????
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Katika ndoa wanawake tunavumilia mambo mengi saana Mungu mwenyewe anajua.... Inasikitisha kwa kweli, na katika hii hadithi, haya mambo yapo saana katika jamii ila tu ni mara chache wahusika mna bahatika eti msiwe mmeathirika. Wengi wanakua wameathirika kwa kweli, na mara nyingi familia nzima kuteketea. Huu ugonjwa wa Ukimwi huu... Umeleta mambo na ukilifikiria saana waweza changanikiwa, na wanandoa wengi ndo hasa wahanga.

  Ukiangalia katika hii hadithi kweli kabisa lazima ushangae wanawake tulivo viumbe wa ajabu. Umekaribishwa katika ndoa ya watu lakini utafanya vitimbi hapo weee ka vile nafasi yako mpya itamchanganya mumeo hivo hivo miaka yoote. Na ndo maana katika hali kama hizi mwanaume anapoamua kuongeza mke wa tatu wa pili huchanganikiwa saaana kuliko hata wa kwanza alipochanganikiwa kwa ujio wake.
   
 5. k

  kisukari JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,763
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  itanibidi nikaangalie hiyo blog ya mwanamke nyumba
   
 6. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Usifanye mchezo na loneliness; najua karibia blog zoote za Bongo. Hii blog niliyotoa hii habari inaitwa "Mwanamke nyumba"

   
 7. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Yes I also recommend; ina mambo mazuri sana hasa kwa wanawake. Basing on true life stories.

   
 8. m

  muhanga JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mmh ni story nzuri kwa kweli lakini haibadilishi ukweli kuwa 'si rahsi mtu kurudia matapishi' huyo mume once alishakuona hufai, amekurudia si kwa kuwa anakupenda ila ni kwa kuwa amekosa pa kishika baad ya mke mdogo kumkorofisha. Ingekuwa mie ningemkwepa kama ukoma! huo ni urafiki wa mashaka swala anacheza bluzi na simba.. guess what next??!!
   
 9. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  It is true; hapo wamerudiana sababu ya convenience tu; si kwa sababu ya penzi; nina imani hata huyu mwanamke hana feelings kwa mumewe kama walipokuwa zamani kabla ya hayo yalotokea; ila wameangalia faida nyingine za wao kuendelea kuwa pamoja ukizingatia they were not divorced.

   
 10. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  too sad
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  stori ya kusikitisha sana kwa kweli,lakini na nyie kinamama kwenye uzanga wenu huwa mnalisomba na kulileta nyumbani.
   
 12. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Duu habari hii ndefu lakini inamafundisho na majuto yake ....
  Kama wamepima na wote wameonekana ni wazima, na pia bi mdogo amepewa talaka, na kama wote bado wanapenda basi wasameheane na warudiane watunze familia.
  Kila la kheri yao
   
 13. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Too sad.lakini haya ndio maisha na mikasa wanayokumbana nayo wanawake wengi wa kitanzania.
   
 14. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #14
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Ai ndefu ila imenigusa sana
   
 15. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,675
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Bishanga unafikiri nimekuelewa basi? Unamaanisha kina baba huwa hawalibebi au?
   
 16. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dah imenigusa sana....kweli wanawake ni wavumilivu sana
   
 17. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sana, lakini itafika kipindi wanawake watachoka kuvumilia hayo mateso yote.
   
Loading...