Jamani hii ni haki kumwacha mke mliyezaa naye watoto saba kwa kosa moja la matokeo ya DNA.

MERCYCITY

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
986
1,000
[h=1]Mwanamke adai DNA imevunja ndoa yake[/h]
ico_plus.png
Share
ico_bookmark.png
bookmark
ico_print.png
Print
ico_email.png
Email Rating
aliyeachika.jpg
Frederica Michael,mwanamke anayelalamikia kipimo cha DNA.
Na Florence Majani (email the author)

Posted Alhamisi,Decemba6 2012 saa 8:36 AM
Kwa ufupi
‘Nilimpenda mno mume wangu Mushi, Mungu anajua, lakini ameniacha kwa sababu ya majibu ya DNA ambayo nina hakika yalifanyiwa hujuma au yalikosewa katika mikono ya binadamu,” alisema mwanamke huyo kwa uchungu.

SHARE THIS STORY

0
inShare​

Related StoriesMWANAMKE mmoja mkazi Ilala, ameibuka na kukishutumu kipimo cha vinasaba (DNA) cha kutambua uhalali wa baba kwa mtoto, kwamba hakina ukweli kwani kimevunja ndoa yake.

Frederica Michael, aliyefika ofisi za gazeti hili jana, alikosoa kipimo hicho kuwa kina upungufu mkubwa, kwani hakikutoa majibu ya ukweli katika kesi ya uhalali wa mtoto wake mwaka 2005.
Alisema mwaka 2005, familia hiyo ilikwenda kupima kujua iwapo mtoto wao aliyezaliwa mwaka 2004, ni mtoto halali wa mume wake, Constatine Moshi.

“Nimejifungua Aprili 11, 2004 wakati huo mume wangu alikuwa safarini, aliporudi na kumkuta mtoto alibadilika na kusema siyo wake,” alisema Michael.

Alisema mume wake alikuwa akimtuhumu kuwa, ana uhusiano na bosi wake jambo ambalo mwanamke huyo alilikanusha vikali.

Wiki hii gazeti hili lilitoa takwimu za mwaka huu za matokeo ya vipimo vya DNA kutoka maabara ya Mkemia Mkuu, ambazo zinaonyesha asilimia 44 ya waliokwenda kupima uhalali wa baba siyo wazazi halisi wa watoto hao.

Mwanamke huyo alisema mume wake, alimkataa mtoto huyo akidai ana asili ya Kiarabu jambo ambalo Michael alilikataa na kudai kuwa, ukoo wao ni weupe na wana nywele laini hivyo yawezekana amerithi upande huo.
Alisema mgogoro huo ulikua na mwaka 2005, waliamua kupima DNA na Julai 20, mwaka huo huo majibu yalitoka yakionyesha mtoto huyo siyo halali wa Constatine.
Michael anakanusha vikali majibu hayo, akisema yana upungufu mkubwa kwani yeye ndiye anayeujua ukweli.

“Sikuwahi kuzini nje ya ndoa tangu nimefunga ndoa mwaka 1999 na mume wangu Mushi ambaye nimezaa naye watoto saba,” alisema.

Alisema kipimo hicho kinatekelezwa na wanadamu, hivyo wanaweza kufanya makosa ambayo yameigharimu ndoa yake.
‘Nilimpenda mno mume wangu Mushi, Mungu anajua, lakini ameniacha kwa sababu ya majibu ya DNA ambayo nina hakika yalifanyiwa hujuma au yalikosewa katika mikono ya binadamu,” alisema mwanamke huyo kwa uchungu.

Alisema ni vyema DNA kitumike kwa uangalifu kwani kinaweza kusababisha migogoro zaidi katika jamii.

Hata hivyo, Mkemia Mwandamizi wa Kitengo cha Masuala ya Jinai, Baiolojia na DNA, Gloria Machuve alisema kipimo hicho ni sahihi na kinatoa matokeo yenye ukweli kwa asilimia 99.
Machuve alisema maabara hiyo ilinunua mitambo bora zaidi na kisasa, ili kupata matokeo yenye uhakika hivyo matokeo yake yana uhakika na ukweli.
 
Anthonio

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
202
195
Kama anaamini kipimo kimekosea amshauri mumewe warudi tena.
ILA MKE ANAUMA!!!!!!!!!!!!!!!!
 
ureni

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,263
1,250
Mama huyo mtoto wa kiarabu na bosi wako je alikuwa mwarabu?Mama pole sana lakini ndio hivyo tena kama ulikua unamdanganya mmeo ndio matunda yake.
 
ureni

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,263
1,250
Kama anaamini kipimo kimekosea amshauri mumewe warudi tena.
ILA MKE ANAUMA!!!!!!!!!!!!!!!!

Mie sishauri hivyo manake kitu kitakachotokea hapa wakirudi kupima tena huyu mama atatumia nguvu yake yote aijuayo ya kulobi kubadilisha matokeo ili kuokoa ndoa yake kwa hiyo hamna haja ya kurudia kupima matokeo ndio hayo.Next time awe mwaminifu incase akipata second chance
 
filonos

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
647
225
HAHAAA....na bado..mlizoea sana kutupakazia..saivi mtasubiri sana..

haaaaa ..kwani nawewe ni kati yahao wa Hathiliwa na dhahama hiyo??mbona unaonyesha kama umepata Mkombozi wa KITANDA..haram???pole kitanda hakizai Haram kua mpole tu
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,497
2,000
je huyo mtoto aliy mweupeanachmbe chembe za mama? isije ikawa mtoto waliopewa hospitali sio wao wote wawili? na kama ana chembe chembe za mama, lakini za baba hakuna, naye anadai mikono ya binadamu nk, kwanini wasipeleke kwingine? halafu haya mazingira ya issue yenyewe, kwanini mume akutuhumu? je ulionesha dalili za kusaliti? na muda wa safari ilikuwa kipindi gani mwaka au miezi .
 
fluid

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
334
250
haaaaa ..kwani nawewe ni kati yahao wa Hathiliwa na dhahama hiyo??mbona unaonyesha kama umepata Mkombozi wa KITANDA..haram???pole kitanda hakizai Haram kua mpole tu

baba hayajanikuta lakini huwa inaniuma sana kuona mtu analea katoto kwa moyo mmoja akijua ni wake..yani kwanini umfanye mwenzio ***** kiasi hicho..
 
mtotowamjini

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
4,527
0
mwisho wa siku mwanamke ndio anajua ukweli na sio DNA machine...kama huyu mama anajua kua hajatembea na mwanaume mwingine basi huo ndio ukweli na sio DNA.. hizi mashine mimi siziamini sana hasa the fact zinaendeshwa na wabongo ndio kabisaaa
 
NATA

JF-Expert Member
May 10, 2007
4,510
1,195
Haya mambo ya DNA wangeyaacha huko huko Ulaya, huku kwetu yatatusmbua.
Sisi tunaishi kwa imani zetu e.g
Kitanda hakizai haram
Mtoto wa mwenzio ni wako
Kila mtoto anakuja na riziki yake

Mbona wanataka kutuvuruga na hii kitu.lol!
 
ZENITH

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
859
500
Mie sishauri hivyo manake kitu kitakachotokea hapa wakirudi kupima tena huyu mama atatumia nguvu yake yote aijuayo ya kulobi kubadilisha matokeo ili kuokoa ndoa yake kwa hiyo hamna haja ya kurudia kupima matokeo ndio hayo.Next time awe mwaminifu incase akipata second chance
Hence approved!teh teh teheekh!
 
mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
16,433
2,000
shenz type!!! hapa ndio tutajua kuwa mwanamke ni mtu mbaya sana....kazi kuwabambikizia wanume watoto ambao sio wao loh!! kweli siku hizi wanawake wanatoa papuchi kama karanga.
 
sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
2,000
Mie sishauri hivyo manake kitu kitakachotokea hapa wakirudi kupima tena huyu mama atatumia nguvu yake yote aijuayo ya kulobi kubadilisha matokeo ili kuokoa ndoa yake kwa hiyo hamna haja ya kurudia kupima matokeo ndio hayo.Next time awe mwaminifu incase akipata second chance

Hahahaaa chiiizii nimecheka sana
 
ZENITH

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
859
500
Haya mambo ya DNA wangeyaacha huko huko Ulaya, huku kwetu yatatusmbua.
Sisi tunaishi kwa imani zetu e.g
Kitanda hakizai haram
Mtoto wa mwenzio ni wako
Kila mtoto anakuja na riziki yake

Mbona wanataka kutuvuruga na hii kitu.lol!
Tukisema teknolojia zote zilizotokea ulaya tuwaachie wazungu wenyewe mbona tutakosa mengi?!
 
NATA

JF-Expert Member
May 10, 2007
4,510
1,195
Tukisema teknolojia zote zilizotokea ulaya tuwaachie wazungu wenyewe mbona tutakosa mengi?!

Hii wangeiacha tu huko huko ninachokiona mbele yangu wengi si watoto wa baba zetu mh!
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,107
2,000
mwisho wa siku mwanamke ndio anajua ukweli na sio DNA machine...kama huyu mama anajua kua hajatembea na mwanaume mwingine basi huo ndio ukweli na sio DNA.. hizi mashine mimi siziamini sana hasa the fact zinaendeshwa na wabongo ndio kabisaaa

sikubaliani na wewe kuna wanawake wanatembea na wanaume watatu hadi watano kwa siku na kesho yake hivyo hivyo,atajua mimba ni ya nani?na uzoefu unaonyesha kuna wanawake hawana idea baadhi ya mimba mwenyewe nani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom