Jamani Haya Ya Sunflag Mmeyapata

Kiwori

New Member
Sep 27, 2007
2
20
Juzi nasikia wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha SUNFLAG mjini Arusha wamefukuzwa kazi.
Kama kuna mwenye taarifa naomba ani update?
 

Mr EWA

JF-Expert Member
Mar 15, 2007
332
225
Nami nimesikia kutoka BBC asubuhi kuwa wafanyakazi kama 300 wamefukuzwa kazi kutokana na mgomo wa kudai mshahara uliotangazwa na serikali.

Hapa pia wa kulaumiwa ni Chiligati kutosimaia kauli zake na kusababisha kile alichotangaza mwanzoni sio kile alichotangaza hivi karibuni.

Huyu pia sijui atasema kadanganywa na kamati aliyoiunda ya kumpelekea mapendekezo ambayo naye aliyatangaza na sasa anatangaza kitu kingine.

Nafikiri ktk wakati huu tulio nao hatuhitaji viongozi kama hawa na fikiri pengine ni uzee ndio unawafanya wapoteze kumbukumbu haraka juu ya kauli wanazotoa na hatimaye wnanajikuta kubadilisha kauli kila mara.

Je hili si kosa la yeye kuwajibika?
 

Democrasia

Member
Feb 1, 2008
79
95
Mzee Mwanakijiji huwezi kuamini kwamba haya yote amesababisha mkuu wa mkoa wa Arusha. ambaye amekaa madarakani kama mkuu wa mkoa kwa zaidi ya miaka 35
Mimi nadhani umefikia wakati JK aanze kufanya mabadiliko.
Watanzania tutaendelea kunyanyaswa mpaka lini
 

Mr EWA

JF-Expert Member
Mar 15, 2007
332
225
Na hawa askari wetu kutumia nguvu na kupelekea kuumiza wafanyakazi kadhaa ni kwamba hakuna mafunzo yanayofundisha chuoni kwa askari wetu ambayo ni yamuafaka kushughulikia issue kama hizi.
 

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,254
2,000
Inaelekea wakati tunaamua kuufuata huu mfumo wa uchumi wa kibepari haya hatukuyategemea au labda hatukujiandaa sawasawa kuyakabili.

Siyo Sunflag peke yake, viwanda vingi Dar wafanyakazi wako kwenye migomo wakidai kima cha chini 150,000/= kama ilivyotangazwa na serikali. Bosi mhindi wa kiwanda kimoja cha vifaa vya plastic alisema wao wataendelea kulipa 80,000/= na hiyo 150,000 inafikiwa na wale wanaofanya overtime!

Siajona action kutoka vyama vya wafanyakazi hapa; utawaona kimbelembele wanapotetea watumishi wa serikali ambao kwanza hata utendaji wa kazi ni wa mashaka, lakini kwa walalahoi wenzetu wanaozalisha viwandani kwa wahindi wameachwa kupambana wenyewe.

Wafanyakazi wa Tanzania unganeneni kukomesha huu unyonyaji!
 

Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,607
1,500
When you have poor rule of law haya ndio madhara yake. Nilishauliza mwanzo kabisa, in what ways will Kikwete enforce the new mishara?

There is no rule of laws in that country. What we do have is celebrity JK
 

Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
2,000
NIlishatoa kauli nyingi before, narudia tena,
Mishahara mipya ni UNREALISTIC!
JK alikuwa anajitafutia umaarufu kupandisha mishahara hovyo. Sasa matokeo yake ni inflation, viwanda vinafunga na wanaondoka. Mwenye masikio asikie hoteli na viwanda zipatazo 10 (na si ndogo za uchochoroni) zinafungasha na kuondoka destination: Malawi and Rwanda.
Huwezi kuleta ukommunisti wakati kuna soko huria. Kushabikia mishahara mikubwa wakati uchumi wenyewe wa nchi ni duni ni kukosa ujuzi wa kiuchumi. Mjiulize GDP ya nchi ni kiasi gani? HIyo mishahara mipya iko in line na pato la taifa. How can you pay more than you earn?
Ridiculous. Hii ni economics za miaka ya 60 na sisi watanzania tumebaki kushabikia tu!
Will a proper economist stand up come and clean the mess up!? We need leaders who can tell people the truth and the reality!
Sasa hao wafanyakazi si afadhali wangeendelea kupata 80,000 kuliko kufukuzwa kazi. Alafu mnaolalamika mnalalamika nini? This is capitalism! Look at European countries, they are waking up to the reality that planned economy is unsustainable, and now they have to fight the difficult fight. France, Germany are now waking up and smelling the coffe, sasa Tanzania nchi maskini tunataka kuishi kama wajerumani? Let us first build those viwanda na kujiimarisha then tutaongea.
I rest my case.
 

Democrasia

Member
Feb 1, 2008
79
95
Jamani naona hamjaelewa ni nini kinaendelea,
Hapa ni kwamba Mkuu wa mkoa ndio aliyeamuru wafukuzwe kazi
 

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
253
0
Susuviri umeongea in a proffesional way,asante. Lakini kumbuka raia wengi wa nchi hawana shule na ndiyo vibarua wa makampuni hayo,sasa unapotangaza kima cha chini ni laki moja na nusu na raia hawa wakasikia serikali yao imesema kupitia Mjinga moja Chiligati,unafikiria nini kitakachofuata? lazima wadai kwa nguvu zote. Wakulaumiwa hapa ni watendaji wetu wanojitafutia umaarufu pasipo kufiria kwa undani na kuja na kitu ambacho kitaleta uwiano wa mapato ya kampuni na mishahara ya wafanyakazi,siyo mtu anakurupuka tu na mawazo toka kwenye tume aliyoinda ikiwashirikisha shemeji. Usanii wa JK umezidi
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,678
2,000
Miaaka 10 ya maumivu TZ katika serikali ya JK. Still 8 years to go. Matumaini yote yamenishia. Now wonder wazamiaji wa meli wamerudi tena!!!!
 

Bobby

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
1,957
2,000
Hii ndio problem ya kutokuwa na serikali makini. Ukishakuwa huna rais usitarajie kuwa na serikali makini hata siku moja. Huyu mzee Chiligati toka aanze kutangaza mishara mipya ameshabadili si chini ya mara 2 figures za hiyo mishahara. As a result kuna wafanyakazi wanataka kulipwa zile figures za mwanzo na waajiri hawakubali kwani wanajuwa zimekwishabadilishwa. Sasa mimi sielewi kwamba maamuzi yanafanyika bila ushirikishwaji kiasi serikali inakuwa haijui isimamie wapi hili linasikitisha kwa kweli.

Kichekesho kingine,Chiligati alipotangaza mara ya kwanza alitaka mishahara mipya ianze kulipwa the next two months sasa sijui kwa bageti ipi hiyo na mwisho wa mwaka ulikuwa bado,then ikabidi abadilishe tarehe-hii serikali uchwara? Serikali imeomba miezi 6 ili kuongeza hiyo elfu 20 watu binafsi mnawapa 2 months kuongeza 100,000-are you crazy?
 

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,016
2,000
Hawa wafanyakazi kwanza waligoma wakidai 150,000-ndo akaenda Mkuu wa Mkoa- akawasihi warudi kazini- kwanza wasiendelee na mgomo wakakataa!

Sunflug iliomba barua kwa Chiligati walipe 80,000 kwani ni labour intensive na kama itakuwa 150,000 basi watafunga kiwanda au wapunguze wafanyakazi. Chiligati akawapa barua waendelee na 80,000. Kwa hiyo wakaanza fujo-kama hawalipwi 150,000- Mkuu wa Mkoa akaita FFU- na kusema wanaotaka kuendelea na kazi waingie kiwandani- na wasiotaka- basi waondoke- ndo naskia kiwanda kikafungwa!

Kama alivyosema Susuviri- huu sii Ujamaa- ni Capitalism- hii inaweza kuwafukuza wawekezaji! Wanasema the same work kama ya Sunflug India hulipwa 70,000, na China 80,000 , Vietnam 60,000.

JK asiingize siasa ktk uzalishaji! Naskia hawa wafanyakazi walikuwa wanaimba nyimbo za kumkumbuka Nyerere!

Wafanyakazi wengi wataachishwa kazi- serikali ispokuwa makini. Mimi ni bora niwe na kazi nilipwe hata 60,000 kuliko kutokuwa na kazi kabisa! Chiligati amekosa Economits kumshauri?
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,046
2,000
Katika hili ninauliza, kwanini wafanyakazi wa viwanda na makampuni ya IPP hawagomi kudai mishahara mipya?
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,046
2,000
Katika hili ninauliza, kwanini wafanyakazi wa viwanda na makampuni ya IPP hawagomi kudai mishahara mipya?
 

Democrasia

Member
Feb 1, 2008
79
95
Mimi naona kauli aliyoitoa mkuuwa mkoa babu Shirima ndio imefikisha hapa tulipo, i mean kwamba ndio amewapa wahindi kichwa ngumu. kilichopo yeye nawaziri mhusika ambaye pia msemaji wa Mafisadi mzee Chiligati naye achomoke kwa kuwa wanatuletea matatizo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom