Jamani Hapa Mapenzi yapo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani Hapa Mapenzi yapo?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by laussane, Oct 27, 2009.

 1. laussane

  laussane JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inapotokea umetokewa na kijana, mpole, mkarimu, mpenda dini na anakuambia direct kw alikw na mpenzi lakn hayupo tz na hataki kurudi tena, nayy umri wake una mruhusu kuoa sshivi kwaiyo anatafuta mwanamke alokuwa serious maana hataki kupoteza mda, na ww unaetokewa haupo katika mahusiano kwa takriban miaka 3 na unajipa moyo na kufurah kuwa ukiloliomba siku zote limetimia, mnakuwa pamoja kama 6 months hivi, then anakuambia yule mpenzi ambae alikuwa hataki kurudi amepiga cm kwao kuwa atarudi kabla ya January na kwao wanaleta salaam upande wa huyo kijana kuwa waliongea na binti na kakubali kurud, na huyu kaka anakuja kwa ww mpenzi mpya na anakuambia yote yaliyojili na mbaya zaid huyo mchumba anaekuja ni mchumba ndugu yani dada binamu, wakati huohuo ww unampenda sana na hapo nyuma kabla hujawa na ukaribu nae zaidi mlishaenda clinic kutest hiv na hiyo yote mlifanya kwa malengo ya kuingia katika mahusiano ya kudumu,
  Kwa bahati mbaya pia umeshika ujauzito una kama mwezi mmoja tu ukitaka suluhu ya hili anakushauri mfunge ndoa ya siri kana kwamba tayari alishaoa! Unakabiliana nayo vp hali kama hii? Na je hapa mapenzi yalikuwepo au? Ata hivo bado anaonyesha ana upendo na ww na wakati huohuo anaonesha ana upendo na dada binam kwa kuona sms wanazotumiana! Comments zenu muhimu sana jamani karibun tuchangie mada
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,014
  Likes Received: 23,934
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa matatizo yaliyokukuta dada. Kwa bahati mbaya Sina la kukushauri.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Unajua mimi nina plan yangu ya kuweka ndani 2012 maombi yanaruhusiwa kama huko umetoswa na mm ni mcha Mungu kweli kweli
   
 4. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  sasa wewe unacholaumu ni nini, ninyi akina dada kazi yenu ni kulalamika tu, sasa kwa nini usikubali hiyo ndoa ya siri ili akija amwambie kuwa alishaoa? Ukikataa upuuzi wako mwenzio atakuja kukunya'anya huyo jamaa na mtoto hatakua na malezi ya wazazi wote wawili, fanya hima funga ndoa, wacha kujishauri shauri
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kwanza dada ulikosea......hukupaswa kujiachia kushika mimba kabla ya kufunga ndoa ( kwa sie watu wazamani, naweza kukwambia hukutakiwa kukutana nae kimwili kabla ya kufunga ndoa)

  ushauri kwako ni kukaa chini na mwanamme mzungumze kwa upana na urefu kuwa mkishaoana kwa siri, huyo mchumba wake ndo inakuwaje? na uhusiano wake nae unakuwaje?
   
 6. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  kama huyo mpenzi alikuwa hataki kurudi imekuwaje akapata wazo la kurudi ghafla? kuna namna hapo, huyo mchumba alikudanganya kwa hilo ndio mana alijuitunza muda wote huo akimsubria huyo mchumba wake wa huko na wewe ulivyoingiliwa kwa gia ya ndoa bac ukajisahau, na hata kama mlipima mkajikuta wazima kwanini ubebe mimba bila kujua muelekeo wa kijana upo wapi? nashukuru cna mdogo wa kike mana ningemtwaga kila kukicha.
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
   
 8. JS

  JS JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kwa nini ulikubali in the first place kuwa na huyo jamaa ambaye alikuwa na mchumba already??ulikuwa na hakika gani kwamba hatarudi kabisa mpaka uchukue uamuzi wa kuwa naye huyo kaka??mwenye mali kasharudi na kma anampenda bado achia ngazi shosti.
   
 9. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama kweli jamaa alikua serious yani miezi sita yote hata mawifi hawakujui? hapo inaonekana kuna ka ukweli unaficha isije kua hiyo mimba ni mtego wako tu wa kuhalisha kuolewa sasa naona inakula kwako!
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hapendwi mtu hapo bana...kwani wanaopenda hamwajui jamani?
  Huyo ni mtu wa saundi, na mbaya kama kinyonga!
   
 11. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  hizi ndoa za siri zinaweza kugeuka balaa tupu...
  usiingie kichwa kichwa kwenye shimo ambalo hujui urefu wake..
  mtu ana mchumba halafu inakuwaje anaanzisha uhusiano mwingine serious kabla ya kuvunja huo uchumba?
  kwa kifupi huyo bwana haeleweki...

  mi nashauri bora awe wazi kuchagua kati yako na huyo binamu, then muweke mambo wazi kwa ndugu, kama mnakubaliana kuoana muoane waziwazi ili wote muwe responsible na kitakachotokea

  vile vile kukubali kumzunguka mwenzio (binamu dada) sio vyema hata kama una mtoto, sio vizuri kusema akija ndio akute hiyo suprise ya ndoa na mtoto, itamuuma sana..bora aambiwe kabisa na ndoa iwekwe wazi...lakini huyo bwana anaweza kufanya hivyo kama kweli kaamua kumuacha binamu na kuwa na wewe tu

  vinginevyo wewe shika hamsini zako utafute ustaarabu wa kulea mwanao kimya kimya, siku nyingine uwe more careful..tunajifunza kutokana na makosa
   
 12. naima79

  naima79 Senior Member

  #12
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 186
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Unajuaje kama ana dada? labda wamezaliwa wakaka tupu? Huyu mwaname anaonesha hapa msimamo tu labda alikuwa na tamaa za kimwili! Dada kama limekukuta wewe au umelileta lipo katika jamii zetu, kama ww ni muislam funga ndoa ya siri, mawifi, mashangazi utawajua baadae hapa unatafuta uhalali wa ndoa!"wanaume tuwapumzishe wadada jaman, mapenzi yenu ya uwongo ndio yanayopelekea matatizo siku zote"
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Dada ni akili yako tu inayokudanganya kuwa unapendwa sasa kama umeshaona na sms wanatumiana zinazoashiria mapenzi kwa nini ujitie jakamoyo? achana naye usikubali kufunga ndoa kwanza kama mwanaume anatakiwa awe na msimamo na aonyeshe kwa kila mtu kuwa ana msimamo asihitaji msaada wako katika hilo.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  shost hapa hakuna ndoa angalia namna ya kutunza mtoto wako tu hayo mengine usitegemee
   
 15. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kwanza hii sifa ya ushika dini ina walakini,iweje akukabidhi mimba?Sidhani kama huyo alikuwa na lengo zuri kwako ila tatizo lako ulimfungilia moyo wako.Huyo alikuwa anatafuta mapozeo tu kipindi hicho mchumbake yupo mbali.Usilazimishe mambo,tulia ,tafakari,na ufanye uamuzi sahihi kwa maisha yako ili usije juta the rest of your life.Huyo anaonekana hana msimamo kwa sababu haonyeshi ujasiri wa kukulinda(kama kweli anakupenda atakulinda).Kwa nini asiende kwao na kueleza the whole situation kama alivyopata ujasiri wa kukueleza?Take care.,bora nusu shari kuliko shari kamili.
   
 16. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #16
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Imekula kwako dada, pole sana kwa hilo. ndo mambo ya mjini hayo. hata kama mlipima HIV hukupaswa kujiachia hivihivi bila kinga. hakuna ndoa hapo.
   
 17. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  jamani wadada mimi huwa nawambia hizi spidi zenu za kubeba mimba ndo mnatanguliza ili mpate ndoa hazifai kabisa, mwenzio huyo according to your maelezo anampenda huyo binamu yake. kataa habari ya ndoa ya siri, si ndoa hiyo ni wizi na kukudhibiti tu ili yeye akishaoa binamu yake kwa dini aendelee kucheza rafu kwako kwa kigezo hicho kwamba kakuoa, cha msingi wewe lea mwanao aliyeko tumboni, kama unampenda sana nendeni kwa wazazi pande zote mbili alipe mahali na mfunge ndoa ambayo itashuhudiwa pande zote. lakini ni bora usiwe desperate maana hata ukifunga ndoa kuna potential problems na huyu bwana na binamu yake.
   
 18. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #18
  Oct 27, 2009
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Pole sana.
  swali la msingi; huyo mchumba umeongea naye kuhusu hiyo mchumba wake? ana mtazamo gani, i.e. bado anampenda? kama bado anampenda achana naye, usikubali hiyo ndoa ya siri maana hawezi kuwa anakupenda pia. kuna wadada wengi tu wana watoto na hawajaolewa, kwa hiyo huo ujauzito usikuumize kichwa, utalea tu.
  akikuambia hampendi basi mwambie hutaki ndoa ya siri.
   
 19. l

  lambie Member

  #19
  Oct 27, 2009
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inshort dada achana na huyo jamaa kabisa atakuharibia zaidi.... jiamini tulia na zaa mtoto na ukiona kuzaa shida sana abort kama ujauzito haujazidi 2months. ni hayo tu
   
 20. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Kwani lazima mfunge ndoa? Mungu amekubariki kupata ujauzito huenda ukapata pia mtoto.Ukizaa mtoto wako endelea na maisha yako na mwanao. kama mungu alikuandikia kuolewa utaolewa tu tumeshaona wanawake wameolewa akiwa ameshazaa watoto watatu.......makosa yapo..futa hilo songa mbele!!
   
Loading...