Jamani, eti mtu ambaye hana CPA anaweza kufundisha CPA class review? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani, eti mtu ambaye hana CPA anaweza kufundisha CPA class review?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Kikomelo, Dec 17, 2011.

 1. K

  Kikomelo Senior Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kuna mkoa mmoja nimeenda nikakuta kuna watu wanafundisha watu wanaotafuta CPA lakini hao walimu wenyewe hawana CPA, inakubalika hii? Au kama mtu amesoma finance anaijua vyema anaweza kufundisha? au kama mtu ana postgraduate ya taxation anaweza kuwa anafundisha somo la kodi hata kama hana CPA?

  wadau mi sielewi, naomba kufaamishwa!
   
 2. SUPERUSER

  SUPERUSER JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  we unaonaje?
   
 3. K

  Kikomelo Senior Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mi sijui na ndo mana nimeamua kulileta hapa jamvini hili tujuzane.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  anaweza... Kwani cpa ni somo moja? Kuna various experts wasio na cpa lakini wana ujuzi maalum kwenye specific subject


  funguka na punguza mgando mkuu
   
 5. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  CPA siyo fani. Ukisomea udereva wa abiria kuna wataalam wa huduma ya kwanza wanafundisha first aid, je wakiwa hawajui kuendesha gari hutaelewa fisrt aid wanayokufundisha ili uwe dereva wa abiria. Ukiona jambo dogo namna hii limekushinda kulibaini wewe mwenyewe, basi hilo darasa la CPA usiingie unajaza wingi bure...ah nimekumbuka, wasomi wetu ndio hivyo hivyo ban. We ingia tu ukakariri upewe cheti uende
   
 6. N

  Naitwa Nani Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeah hiyo inawezekana kabisa kwani kwenye CPA kuna masoma mbalimbali, hivyo kila mtu ana uwanja wake wa kujidai!!
  Mfano mzuri mimi nimehitimu katika chuo fulani hapa DSM, Kuna baadhi ya LECTURERS wapo nondo vibaya mno wanafundisha CPA lakini wao hawana!!
  Ndo hivyo Kaka!!
  Halafu kumbuka Teaching ni kipaji pia kwani unaweza ukawa na CPA lakini kwenye kudeliver Material ukawa hauko vizuri!!
   
 7. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ili centre ya CPA iweze fanya kazi na itambuliwe na NBAA lazima kuwe na walimu wenye CPA, hata kama wewe ni mkali kama huna CPA you are nothing, chunguza vizuri hiyo centre yaweza kuwa haitambuliki
   
 8. K

  Kikomelo Senior Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hapo nimekupata! lakini kama mtu anafull module E lakini hajamaliza module F, mtu huyo mi nadhani anakuwa na uwezo wa kufundisha module E, mana alishaifaulu hiyo module.
  Nimeambiwa eti waliosajiri vituo ndo wenye CPA lakini si lazima walimu wote wawe na CPA. eti kama mtu anajua na wanafunzi wanamuelewa akifundusha, basi inatosha.
   
 9. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja.
   
 10. ANKOJEI

  ANKOJEI JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  kisheria wote wafundishao CPA class review lazima wawe na CPA, ila ci unajua bongo kuchakachua then hao wenye CPA ni wachache.
  Kabla hujaanzisha darasa la CPA kuna form zinajazwa ili jamaa wa bodi wajue uwezo wa wakufunzi, CPA ikiwa ni MUST kigezo. then every year b4 you start classes lazima ujaze form flani ivi ili jamaa wa_weze kuchambua na kuchanganua uwezo wa wakufunzi wako. issue apa ni kuprotect public interest na kulinda professional isije ingiliwa na VILAZA! au watu wasiokuwa responsible. and also to allow traceability. darasa gani la nani wanafeli sana, na kwa nini?
  Ila wakati flan kuna jamaa ambao hawana CPA but they are so specialised in such a way that there is no doubt wanao uwezo wa kudeliver kama CPA gradutes or more then wanafunza kama kawa! Hamjasikia semina zao uko dsm na znbr utasikia semina ya wahasibu alafu utakuta anayetoa mada hana cpa ila amespecialise kwenye International money laundering(kusafisha pesa chafu)?
  Sasa ni wajibu wa mwenye kijiwe kuona mambo yote hayo yanaenda sawa lasivo darasa lake litakimbiwa au watu ndio unasikia wanakimbilia kwa msasiri_APT.
   
 11. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 792
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mhh uko tunakoelekea form 4 leaver atakujamfundisha student wa pre form 5!
   
 12. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yeah its pocbo Mbona hata PADRI anafundisha mafundisho ya ndo japo wao hawaoiiiiii!!!
   
 13. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ebu rudi nyuma na jikumbushe enzi ya Mwalimu Nyerere kulikuwa na mpango wa elmu ulikuwan unaitwa UPE... yaani ukifika darasa la saba na kufelli unaruhusiwa kuwa mwalimu wa UPE...
   
 14. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Unajua ulivyoliweka swali lako ni vigumu sana kupata majibu ya uhakika. Kwa sababu kwanza kuomba kufundishwa na mtu yeyote yule ni suala la mtu binafsi. Lakini kama alivyokwambia mchangiaji mmoja hapo juu, kuanzisha Centre ya Review Classes ni lazima wahusika wawe na CPA. Hapo ni suala la kucomply na NBAA regulations.

  Lakini suala la kwamba mtu mwenye postgraduate ya taxation hawezi kumfundisha mwenye CPA hapo ndipo unapokosea. Kama nilivyosema hao wanaotaka kufanya CPA wanaweza kuona labda somo la tax linawasumbua na kuna jamaa ni mtaalamu wa tax mwenye postgraduate diploma na anafanya kazi TRA, wanaweza kujikusanya na wakaomba awe anawafundisha sasa hapo utasemaje kwamba jamaa hastahili kuwafundisha? Na usisahau huyo jamaa hata sema kuwa akishawafundisha basi hao jamaa wamepata CPA, mpaka pale watakapofaulu mitihani ya NBAA. Kwa hiyo hilo swali lako lilitakiwa liwe clear.
   
 15. L

  Levim New Member

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka ualimu ni wito! Na wat matters ni nini umepata kutoka kwa anayekufundisha kuwa macho kilaza anaonekana na jembe linaonekana take care. Ishu za kufundishwa na mwenye CPA na asiye na CPA azimati sana kuna watu wanaCPA na they cant deliver, ila kuna asiye na CPA ila akawa ni nondo katika moja ya masomo cha msingi we kuwa makini na anayefundisha.
   
 16. P

  Paul S.S Verified User

  #16
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  CPA msingi wake hauko sana darasani zaidi ya bodi kutoa mtaala na material, lakini kwa kuelewa umuhimu wa ufundishaji bodi ikataka waonata wanaweza kusajili classes review na watakaoomba lazima wawe na CPA.
  Kwakuwa ili upate CPA si lazima upitie review class fulani basi unaweza kufundishwa na yeyote mwenye uelewa na hiyo topki anayofundisha.
  As long umejisajili na kulipia ada ya mtiahani bodi haiwajibi wala kukutaka lazima usome sehemu fulani kukolifai kufanya mtihani wao, sana itashauri utumie class review zilizo sajiliwa.
  Ni wajibu wa mtahiniwa kusaka na kuhakikisha anakover topiki zote za mtaala hata kama utafundishwa na mtu mwenye certificate ili mradi ajue kitu anacho kufundisha.
  So mkuu usihofu kabisa kama walivyosema wadau hapo juu mtaalamu wa tax mwenye bachela anaweza kufundisha somo la tax na mtaalamu mwingine wa costing atafundisha tu somo hili kama nauelewa nalo vizuri na atacover mtaala wote wa somo husika.
  Piga shule acha kutafuta visingizio
   
 17. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Kujifunza kunaweza kuwa "formal" au "informal". Kwa hiyo mtu yeyote mwenye ujuzi/taaluma ya kutosha anaweza kufundisha somo lolote katika mitaala ya Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA). Lakini kwa sababu kuna international standards zinazohusu elimu na quality ya uhasibu NBAA inalazimika kuwa na taratibu za kuhakiki ubora wa watu au taasisi zinazotoa mafunzo ya uhasibu. Hii inaitwa accreditation. Mtahiniwa hawezi kufanya mitihani ya NBAA kama hajapitia kwenye Training Provider mwenye accreditation ya NBAA na hiyo accreditation inatolewa baada ya NBAA kujiridhisha kwamba Trainer (chuo) kina waaalimu wazuri na vifaa vingine vya kujifunza na kufundishia. Lakini waalimu wote katika chuo siyo lazima wawe na CPA. Kwa mfano mwalimu mwenye degree ya sheria anaweza kufundisha somo kama commercial law kwa sababu hilo siyo somo la kihasibu hasa. Au mtaalamu wa Human Resource anaweza kufundisha kozi ya HR Management bila kuwa na CPA. Lakini kwanza ni lazima NBAA ijiridhishe kuwa hao watu wana uwezo wa kuwapika watu ili waje kuwa wahasibu wazuri. Kwa maelezo zaidi tembelea website ya NBAA. Unaweza pia kutembelea website ya International Federation of Accountants (IFAC) na ku-access pages za International Education Standards Board for Accountants (ISEBA) na Internatinal Ethical Standards Board for Accountants (IESBA). Utapata elimu ya kutosha kuhusu elimu ya uhasibu. Siyo swala la kitaifa tu bali ni la kimataifa.
   
 18. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 792
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Plz 4 harsh language, je waweza kuingia choon na kujitawaza kabla ya shughuli?
   
 19. m

  mbweta JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hivi Yohana mbatizaji alibatizwa na nani? Mbona ye alibatiza watu?
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Murphy's Law inasema "Anything that can go wrong, will go wrong"

  Interpretation nyingine ya hili ni kwamba, kisichokatazwa, kimehalalishwa.

  Kwa msingi huo, pengine swali la kuulizwa hapa ni, je, imekatazwa kwa mtu ambaye hana CPA kufundisha CPA review?

  Kwa sababu ujue kufundisha si sawa na kufanya, wenyewe wanasema "Those who can't do, teach". Ndiyo maana sio kila mwalimu anaweza kufanya anayofundisha, na sio kila anayefanya anaweza kufundisha.
   
Loading...