Jamani Dr. Bilal kushika tu madaraka na kuvunja katiba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani Dr. Bilal kushika tu madaraka na kuvunja katiba!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mwanamayu, Nov 24, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Makamu wa Rais, Dr. Ghalib Bilal
  Wakati akiongea kwenye maazimisho/ sherehe/ sala ya Idd El Hajj ya kitaifa kwenye Msikiti wa Simbambali uliopo wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 17/11/2010, alitoa ahadi kwa umma wa waislamu ya kushughulikia kwa kuanzishwa kwa mahama ya kadhi Tanzania Bara (Mwananchi/ Majira/Mtanzania, 18/11/2010)

  Katiba inasema:
  Ibara ya 3
  (1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa

  Ibara ya 6
  ...neno ‘serikali' maana yake ni ... na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya serikali yoyote

  Ibara ya 19
  (2) kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi
  (4) kila palipotajwa neon ‘dini' katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake in pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neon hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo

  Ibara ya 20
  (2) ...haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba au sera yake:
  (a) Kukusudia kukuza au kupigania maslahi ya:
  (i) Imani au kundi lolote la dini

  Ibara ya 26
  (1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano


  [Maswali ya Msingi: Katiba kama isemavyo na ahadi ya Makamu wa Rais kwa Umma wa Waislamu kwa niaba ya serikali ya CCM na Chama cha Mapinduzi sio kuvunja katiba huko? Huyu Kiongozi si amevunja katiba ndani ya kama wiki mbili baada ya kushika madaraka na kuapa kuilinda, kuitetea na kuhifadhi katiba hii, je baada ya miaka miwili itakuaje? Je, serikali ya CCM na Chama Cha Mapinduzi au mamlaka ya nchi ina dini?]
   
 2. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu huyu jamaa ni nuksi imeletwa bara baada ya wazenj kuikwepa mara kadhaa. Hatasababisha migogoro tu hivi karibuni.
   
 3. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Mambo ya CCM mtu anapewa uongozi for convenience tu. Ukweli ni kwamba ndani ya moya wa Dr Bilali hakuwahi kujipangaa kuwa Makamu wa raisi Muungano. Hili limekuja tu kwa sababu ya kufanyiana mtimanyongo ZNZ ikaonekana ni vyema hakapachikwa bara.

  Mimi sitashangaa kuona alivyoanza kujichanganya na swala la mahakama ya kadhi kwa sababu hana utashi hata kidogo na wala hataangaika kuyafahamu maswala kwa undani kwa alipachikwa katika hiyo fursa na haikuwa mapenzi yake. Naamini. Wote tunajua shida ya kuwa na bora kiongozi na kiongozi bora.
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  hana hata sifa moja ya kuwa kiongozi isipokuwa ccm wameamua kumuwekas karibu kwani jamaa ni mbaya kwa kumwaga sumu na kupandikiza mambo so...ccm wameona wawe naye karibu zaidi ...kwa hakika yeye yupo kwa ajili ya zanzibar kujitenga ...na mambo ya kipumbavu km mahakama ya kadhi na oic...........
   
 5. K

  KINA New Member

  #5
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunahitaji Katiba mpya. Hivyo suala la Mahakama ya Kadhi na OIC halina mjadala. Nchi hii ni ya Watu wa dini zote. Haiwezekani tena mtindo wa dini moja kuiba na kukwapua rasilimali na nchi.
   
 6. K

  Kachest Senior Member

  #6
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu wakati wa Idd el haji sijasikiliza hiyo hotuba thank you for informing me and other JF team
   
 7. v

  vibuchu Member

  #7
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kina, kuwa muwazi kwa kujibu maswali yafuatayo:
  Dini ipi hiyo inayokwapua rasilimali na nchi? na ni watu wa dini gani ambao wananufaika na "katiba ya sasa"?Ni watu wa dini ipi ambao wapo mstari wa mbele kupigania upatikanaji wa katiba mpya?
   
Loading...