Jamani bongo ulaya! mpo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani bongo ulaya! mpo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 19, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,536
  Likes Received: 5,753
  Trophy Points: 280
  Watu wamiminika Shoprite kununua mkate Sh 340
  Mwandishi Wetu
  Daily News; Monday,May 19, 2008 @00:03


  WATU wengi wamekuwa wakimiminika katika maduka makubwa ya Shoprite Dar es Salaam kununua mikate inayouzwa kwa bei nafuu ya Sh 340 wakati sehemu nyingine inauzwa hadi Sh 900.

  Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, HabariLeo imekuwa ikishuhudia wateja wengi wakimiminika kwenye maduka hayo na kupanga foleni kwenye kaunta ya mikate kujipatia mikate hiyo.

  Baadhi ya wateja waliohojiwa katika maduka hayo, walisema wanakimbilia kununua mikate kwenye maduka hayo kwa sababu ni bei nafuu na inakuwa bado ya moto. Maduka hayo hutengeneza mikate yake papo hapo.

  “Naipenda mikate hii kwa sababu ni bei nafuu, lakini pia tunaipata ikiwa ya moto, mtaani wakati mwingine wanatuuzia mikate ya juzi,” alisema Juma Kisoki ambaye alikuwa katika duka la eneo la Kamata. Kisoki ni Meneja Masoko wa kampuni ya DCD Dar es Salaam.

  Hassan Said ambaye alisema ni mteja wa muda mrefu wa mikate hiyo, alisema kinachomfanya anunue ni ubora wa mikate hiyo kwa sababu inapikwa vizuri na inaweza kukaa muda mrefu bila kuharibika.

  Wakati bei ya mikate katika maduka ya Shoprite ni nafuu, bei katika mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam ni kubwa maradufu ya ile inayouzwa na maduka ya Shoprite.

  Katika maeneo mengi ya jiji mkate unauzwa kati ya Sh 600 na Sh 900 kitu ambacho kimesababisha wengine kuacha kuitumia na badala yake wanatumia maandazi na vitafunwa vingine kwa ajili ya kifungua kinywa.

  Katika duka la City Supermarket lililopo Mtaa wa Samora, bei ya mkate ambao ni wa ukubwa sawa na ule wa Shoprite ni Sh 700 na mikate mikubwa Sh 900. Nao wanatengeneza wenyewe papo hapo dukani.

  Katika duka la Pamba House Supermarket ambalo lipo Mtaa wa Garden ni Sh 800 kwa mkate mmoja wa ujazo wa kawaida na mikate mikubwa ni Sh 1,100 wakati Shoprite mkate mkubwa ni Sh 550 tu.

  Hata hivyo, unafuu wa bei ya mikate kwenye maduka ya Shoprite umezua maswali mengi kutokana na bei ya mikate katika maduka mengine ni zaidi ya mara mbili ya hiyo.

  Maswali hayo yanatokana na hisia kwamba huenda wauzaji wengine wa mikate wanawaibia wananchi au kuna tatizo la biashara ambalo linasababisha wauze bei juu.

  Juhudi za kumpata Meneja Mkuu, Fredrick Skein wa Shoprite kueleza unafuu wa bei hiyo hazikuzaa matunda, lakini HabariLeo ilizungumza na Meneja Masoko Mathew Kaubo ambaye alisema yeye hana ruhusa ya kuzungumza na waandishi hadi apewe kibali cha kuzungumza.
   
 2. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji nadhani hili ni tangazo la biashara, tufanye utaratibu wa malipo kidogo kwa matangazo kama haya! Au?
   
 3. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  loh dis technique is quite impressive esp if forum hii yatembelewa na wa tz wengi walioko bongo..as ni tangazo la biashara toshaaa!

  on the other hand nimepata mshtuko kidooogo as wakati naondoka bongo kama sikosei mwaka unusu nyuma mkate was just 250 tshs now mwaniambia mingini ni hadi 700 kwa mia 9??
   
 4. M

  Mama JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa, nilishaque hapo madakika kadhaa kisa mkate! na utaona watu wengi wanamiminika shoprite mida ya jioni ukadhani kuwa duka hilo lina wateja wengi sana lkn majority hufuata mikate! kazi kwao bakery zingine.

  Lakini 'heading' ya kuwa bongo ni ulaya haiendani na haya maelezo!
   
 5. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2008
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Je Ubora Wa Mikate Hiyo Ipo Sawa Manake Isije Ikawa Bei Poa Na Kiwango Chake Powa Tena
   
 6. M

  Mama JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  sijui viwango vya mikate lakini nikilinganisha na mikate mingine niliyonunua hapo dar, ambayo mingine inakuwa imeshaanza kuota fungi, ninaopt kwa mikate fresh from the oven hapo shoprite
   
 7. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2008
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  GOOD MANAKE HAWA JAMAA KUKU WAKISHINDIKANA SOUTH WANAWALETA BONGO NA KUPGA SALE BASI WATU WANAMIMINIKA MADUKANI.WATU HAWA ISHI KUHALISHA.
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  May 24, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Bongo nyuyok
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Zenj wao bado wapo na boflo za moto, asubuhi na jioni
   
 10. K

  Kokolo JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2008
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 487
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  VYA BEI POA NI GHARI SANA SANA
  HIYO NGANO YA KUTENGENEZA MIKATE NI YA MWAKA 1955 KWA HIYO UTAONA WATU WATAKAVYOKUWA NA UTINDIO WA UBONGO, KISA MIKATE BEI POA. JIULIZE KWANZA KABLA YA KUNUNUA. KAMA NI BREAKFAST TUMIA MIHOGO, NDIZI, VIAZI NA NGANO YA HAPO NYUMBANI. HIYO NGANO YA KUTOKA INDIA NA SOUTH AFRICA ILIYOKWISHA MUDA WAKE, MTAKUWA VICHAA, NA CCM HAPO NDO WANAPENDA MAANA WENGI WATAKUWA MAZEZETA. UNAJUA JINSI MOHAMED ENTERPRISES ALIVYOUA MKEMIA MKUU WA TANZANIA NA BAADHI YA WAKEMIA, KISA MREMA KACHOMA NGANO ILIYOKUWA IUZWE KWA WATU. KWA HIYO MIKATE JARIBU KUULIZA UNGA WA NGANO NI WA MWAKA GANI? LA SIVYO WENGI WATAENDELEA KUWA MAZEZETA, NDIYO NDIYO NDIYO CCM MPAKA UNAKUFA MAANA UBONGO UMESHAOZA KWA HIYO MIKATE YA BEI NAFUU.
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,536
  Likes Received: 5,753
  Trophy Points: 280
  WANANDUGU HAWA JAMAA WA SUPERMARKET NI WA KUANGALIA SASA KWA INFO TU NA ZA UHAKIKA NAWAPA HII.......ILA NAPENDA KUELEZA HAP[A TATIZO NI KWA WATANZANIA TUNAUANA WENYE KWA WENYEWE.........

  SUPERMARKET NYINGI HIVI SASA ZINACHUKUA MATUNDA TOKA NJE MENGI NI KUTOKA KWA NDUGU ZETU WA SOUTH....KUNA MATUNDA YANAFUNGWA MAENEO YA BARABARA YA KUTOKA MJINI KWENDA UBUNGO NA UKITOKA UBUNGO KWQENDA BUGURUNI
  VIJANA WAMEKUUWA WAKIUZA MIKONONI MFUKO YAKO MATANO MATANO
  WANANDUGU YALE YAMETUPWA NA HAWA NDUGU ZETU SUPERMARKET NA WATANZANIA KUAMUA KUWFUNGIA WENZAO KUONYESHA KWAMBA SISI HAKUNA KITU KINACHO EXPIRE HUKU BONGO KWA HIYO HIYO MIKATE NAYO MMHhhhhhhhhhhhh???????????!!!!1111111 kunani tuwaulize wanatumia nini tofauti..maana ukija angalia utaona hii sehemu serikali waanze kuwafawatilia viwanda vya mikate wanapata faida sana kama ni kweli hatulishwi vilivyo expire...kama wanavyosema wanaunda tume kwa ajili ya mafuta kuchunguza uletaji wake na faida yake waangali na hivi viwanda ...nahisi huu ndio wakati wa TBS kwenda pale supermarket kucheck ubora wa hiyo mikate waje JF KUTUJULISHA nasi tuunde tume yetu ya kupunguza umasikini tanzania.....
   
 12. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Bei sasa ni Tsh 500 badala ya 340
  This could just be a marketing strategy


  .
   
Loading...